Seli mundu ni chembechembe yekundu ya damu ambayo inakuwa katika umbo la mfano wa kifaa kinachoitwa mundu(hutumika kukatia nyasi) au mfano wa umbo la ndizi tofauti na chembechembe nyekundu za kawaida. Seli mundu hizi hutokana na hitilafu kwenye vinasaba ambapo hupelekea uzalishaji wa protini yenye kasoro iitwayo himoglobini ambayo husaidia kubeba oksijeni katika damu. Protini hii inapokuwa katika mazingira yasiyona na oksijeni hupelekea seli mundu ambazo hushikana shikana na kutengeneza molekyuli kubwa na nzito yenye uwezo wa kuathiri mtiririko wa damu katika mishipa.
Baadhi ya sifa za seli mundu hizi ni pamoja na;
- Zinakuwa zina uwezo wa kunasa katika kuta za mishipa ya damu na kuziba mishipa.
- Zinakuwa ngumu kubadilika maumbile hivyo zinashindwa kupenya vizuri katika mishipa ya damu
- Zinakuwa na siku chache za kuishi yani siku 10 mpaka 20 yani huvunjwa vunjwa.
Kuziba kwa mishipa ya damu pamoja na kuvunjwa kwa seli mundu ndio misingi mikubwa ya dalili mbalimbali vya ugonjwa huu ambazo si hususani kwa ugonjwa huu pekee, dalili hizo ni pamoja;
1. Maumivu ya maungio
-Moja ya dalili za awali za ugonjwa huu ni maumivu ya sehemu tofauti tofauti katika mwili na hii inaweza ikaendana na umri wa mgonjwa mfano;
- Watoto wadogo miezi 6 na kuendelea huweza kuwa na maumivu haya kwenye maungio ya mikono na miguu yanayoambatana na kuvimba pamoja na wekundu wa maungio haya.
- Watoto miaka 2 kuendelea na wakubwa huweza kuwa na maumivu kwenye kifua, tumbo na mifupa
2. Kuchoka sana kutoka na upungufu wa damu.
-Upungufu wa damu mwili kutokana na seli mundu kuvunjwa vunjwa mwilini huweza kupelekea mtu kuwa mwenye uchovu sana na dhaifu.
3. Kupumua(kuhema) kwa shida
-Hii huweza kutokana na sababu mbalimbali kama vile maumbukizi katika mapafu, upungufu wa damu mkubwa, pamoja na seli mundu kuathiri mishipa ya damu katika mapafu. Hali inaweza kuendana sabambana na maumivu ya kifua au kukohoa au vyote.
4. Manjano katika mwili
-Sehemu za mwili kama macho, ngozi na mdomoni kuwa na rangi ya manjano ni moja na dalili ambazo mgonjwa mwenye seli mundu anaweza kupata. Hali hii hutokana na kuvunjwa vunjwa kwa seli mundu na mfumo wa mwili ikiwa ikifanywa zaidi na bandama na ini.
5. Kuvimba tumbo
-Moja ya dalili inayoonekana kwa watoto wenye ugonjwa wa selimundu ni kuvimba kwa tumbo zaidi upande wa kushoto na kama uvimbe ni mkubwa sana basi tumbo lote hujaa.
-Hii ni kutokana na kuvimba kwa bandama ambapo bandama huvimba kwa sababu seli mundu nyingi hunashwa humo na kupelekea bandama kuwa kubwa zaidi.
- Wagonjwa wengi wenye seli mundu hadi kufika miaka 6 na kuendelea huwa na uwezekano mkubwa wa kutokua na bandama.
Dalili ni nyingi na tofauti tofauti za mtoto mwenye ugonjwa huu wa selimundu huku nyingi zikiwa zinatokana na madhara ya muda mrefu ya ugonjwa huu. Ikumbukwe kuwa dalili za ugonjwa huu si za kipekee au hususani hivyo ni muhimu sana kwa mtoto kufikishwa hospitali na kufanyiwa uchunguzi zaidi na kupata tiba sahihi. Sio kila mwenye dalili tajwa hapo juu anatakuwa na ugonjwa wa selimundu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni