-Shinikizo la damu ni mgandamizo wa damu katika kuta za mishipa ya damu iitwayo arteri ambayo safirisha damu kutoka katika moyo na kupelekea sehemu zingine za mwili. Mgandamizo huu katika kuta za mishipa ya damu hupimwa kwa kifaa maalumu kiitwa sphygmomanomita AU mashine ya kidijitali (BP mchine) huku kwa wastani shinikizo la damu la kawaida likiwa ni milimita za Mekyuri 120/80.
-Namba ya juu (120) ni presha katika mishipa ya damu wakati chemba za moyo zinasukuma damu (Kusinyaa) huku 80 ni presha wakati chemba za moyo zinapokea damu (Kutanuka).
-Kwa matumizi ya nyumba ni vyema kutumia mashine ya kidijitali katika kujipima kuliko kutumia sphygmomanomita kutoka na ukweli kuwa sphygmomanomita huhitaji utaalamu zaidi wa mtu ili kupima kwa usahihi ukilinganisha na mashine ya kidijitali.
-Mashine za kidijitali ni nyingi sana siku hizi kutoka katika kampuni tofauti tofauti huku zikija na maelekezo ya namna ya kutumia katika maboxi yake. Mashine hizi huwa na "cuff" (sehemu katika mashine ambayo huzungushwa katika mkono wako wa juu, cuff za mashine zingine huja kwa ajili ya kuzungushwa kwenye viwiko au miguu) na pia huwa na sehemu ya kusomea majibu.
-Ni muhimu kujipima shinikizo la damu nyumbani kwasababu zifuatazo kuu;
- Kujua ni kwa kiasi gani shinikizo la damu linakuwa kwa kupima nyumba ukilinganisha na hospitali. Na hii hutokana na ukweli kuwa kuna watu wengi presha huwa juu wakiwa hospitali na huwa kawaida wakiwa nyumbani
- Kujua kwa kiasi gani dawa za presha zinafanya kazi
- Kujua mabadiliko yoyote ya presha yanapotokea muda wowote
1. Fanya maandalizi sahihi
-Kabla kabisa ya kuanza upimaji ni muhimu kukumbuka kuwa unatakiwa kuepuka kutumia kinywaji chenye kafeini kama kahawa, mazoezi na uvutaji wa sigara nusu saa kabla ya kuanza upimaji
-Pia unataki uwe umeshakojoa na kuondoka nguo zote zinazoziba eneo la mkono ambalo utapima presha yako
-Vyote hivi huwa ni muhimu kuvitekeleza kwani huathiri usahihi wa matokeo ya presha yako baada ya kupima
2. Kaa kwa usahihi
-Ni muhimu sana kuzingatia suala la ukaaji, na hapa ukaaji unaotakiwa ni;
- kuhakikisha miguu yote imekanyaga chini na haijapishana,
- mgongo unapata sapoti kwa nyumba na
- mkono ambao utatumika kupima presha uko katika usawa wa moyo.
-Kukaa kwa usahihi huenda sambamba na kukaa kimya kabisa pasipo kuongea chochote na kujitahidi ukimya wa mazingira yanayokuzungua pia.
-Yote haya yasipozingatia yameonekana pia kuathiri majibu ya kipimo.
3. Funga "cuff" (mkanda katika mashine yako) katika mkono wako.
-Funga mkanda huu wa mashine eneo la kati la mkono moja kwa moja pasipokuwa na nguo yoyote kwa juu.
-Hakikisha makanda wa mashine haulegei kiasi cha kutoka eneo lake na wala haubani sana kiasi cha kutojisikia vizuri.
-Baada ya kuweka kila kitu sana, inashauriwa kutulia kwa muda wa dakika 3 mpaka 5 huku mkanda ukiwa umefungwa kwenye mkono
4. Pima presha yako sasa
-Mashine nyingi za kidijitali zinahusisha kubonyeza tufe kwenye sehemu ya mashine kwa ajili ya kuwasha na kisha kupima yenyewe.
-Wakati mashine inapima utahisi hali ya kujaa kwa hewa kwenye ule mkanda uliozungushwa katika mkono pamoja na hali ya kama mkono unafinywa na mashine inapomaliza utahisi hali ya kusinyaa kwa mkanda
-Ni muhimu kusoma maelekezo ya mashine baada ya kuinunua kwani mashine nyingi huja na maelekezo ya namna ya kutumia
5. Rekodi majibu yako katika daftari maalum.
-Baada ya mashine kumaliza kupima utaona namba zinatokea kwenye sehemu ya mashine huku baadhi ya mashine husoma majibu kwa kutoa sauti.
-Majibu huja na namba mbili yani; namba ya juu na ya chini kama iliyoelezwa hapo juu
-Andika majibu yako katika daftari maalumu ili kuweza kumuonesha daktari wako utakapoenda kuonana nae
-Tafsiri ya ujumla ya majibu ya shinikizo la damu ni;
- Shinikizo la juu la damu ni pale mashine inasoma milimita za Mekyuri 140/90 au zaidi
- Shiniko la chini la damu ni pale mashine inasoma chini ya milimita za Mekyuri 90/60
- Shinikizo la damu la kawaida huwa kati ya milimita za Mekyuri 90/60 mpaka 139/89