Ni ukweli kuwa watu wengi ambao wako kwenye matibabu ya dawa za shinikizo la juu la damu hutakiwa kutumia dawa zao siku zote katika kipindi cha maisha yao ukizingatia kuwa tatizo hili huwa na madhara makubwa katika moyo, figo, ubongo na macho. Suala la lini kuacha kumeza dawa za shinikizo la juu la damu miongoni mwa wagonjwa limekuwa likiulizwa sana huku matumaini ya wagonjwa wengi ni kupata muda sahihi wa lini ataacha kumeza dawa. Tafiti mbalimbali zimefanyika kuhusiana na suala la wagonjwa kuacha kumeza dawa kwa wagonjwa ambao presha zao ziko kawaida na mambo mbalimbali yameonekana.
1. Mgonjwa anaweza akasimama kumeza dawa kwa muda katika mazingira kama ;
- Dawa anazotumia kwa sasa zinamletea madhara makubwa yasiyoweza kuvumilika.
- Kipindi cha majaribio ya dawa mpya kwa matumizi ya mgonjwa.
-Moja ya mambo yameyoweza kuonekana ni pamoja na kutokuwa na uhakika wa kipindi kirefu cha wagonjwa hawa kukaa bila ya kutumia dawa huku shinikizo la dawa likiwa kawaida.
-Hii ina maana kuwa ni watu wachache sana (takribani 1/4 ya wagonjwa) wameweza kukaa kwa kipindi cha angalau miaka miwili (2) baada ya kuachishwa dawa bila ya kurudi kwenye dawa lakini wengi wao walilazimika kurudi kwenye dawa.
3. Mafanikizo makubwa ya kuacha dawa za presha yameoneka katika sifa hizi
-Tafiti zimeonesha kuwa mtu anaweza kuwa na mafanikio makubwa ya kuacha dawa endapo atakuwa na sifa zifuatazo
- Matumizi ya dozi ndogo na dawa moja ya presha ya kupanda-Hii imeonekana kutoa matumaini makubwa ya mafanikio kwa mtu anayetaraji kuacha dawa huku ikienda sambamba na ukweli kwamba mtu huyu alikuwa na presha ya kupanda kiasi wakati anaanza dawa.
- Kuanza na kutekeleza mtindo bora wa maisha- Kupunguza kiasi cha chumvi, kupunguza uzito na kuacha pombe
- Umri mdogo- Wenye umri mdogo wameonekana kuwa na muitiko mzuri endapo wataacha dawa kuliko wale wenye umri mkubwa yani miaka 65 na kuendelea.
- Baadhi ya madhara ya kuacha dawa ambayo si ya kutisha kama; kichwa na maungio kuuma,mapigo ya moyo kukimbia haraka, kuvimba miguu, na kujihis mchovu kwa ujumla yameweza kuwatokea zaidi wale watu walioacha dawa hizi za presha ukilinganisha na wanaoendelea.
Suala la kuacha kumeza dawa bado ni la mvutano kutokana na kuwepo kwa tofauti mbalimbali kama zilivyotajwa hapo huku zikiwa hazina kauli ya moja kwa moja ya kuruhusu kuacha dawa kama sehemu ya matibabu ya wagonjwa wenye presha ya kupanda.Hivyo ni muhimu sana kuendelea kuzingatia umezaji wa dawa za presha ya kupanda kama unavyoelezwa na mtaalamu wa afya na ikitokea unataka kuacha kumeza dawa basi jitahidi sana kuonana na daktari kwa tathmini zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni