MADHARA KUMI NA NNE (14) YA KIAFYA YATOKANAYO NA UVUTAJI WA SIGARA AU TUMBAKU.

 Uvitaji wa sigara au tumbaku ni moja ya mtindo wa maisha usio salama katika jamii kwani huchangia kwa kiasi kikubwa kwa magonjwa yasioyoambukiza yani maradhi ya mapafu, moyo, kisukari na saratani. Tafiti zimeonesha kuwa wastani wa 8.7% ya watu wazima Tanzania wanatumia tumbaku/sigara huku wanaume wakiongoza kwa asilimia 14.6 wakati  asilimia 3.2 ni wanawake. Wavutaji wa sigara wamekuwa wakiwaathiri watu wengi wasiovuta kutoka katika moshi huo pia katika maeneo ya kazi na manyumbani. Kutokana na vifo vitokanavyo na uvutaji wa sigara kuwa vingi, ni vyema jamii kupata hamasa ya kuepuka matumizi haya ya tumbaku ili kuwa na afya bora.Yafuatayo ni madhara ya kiafya yatokanayo na matumizi ya sigara/ tumbaku 

1. Hupelekea saratani mbalimbali.
-Uvutaji wa moshi wa tumbaku huathiri mifumo mbalimbali ya mwili ikiwemo mfumo wa upumuaji hasa mapafu. 
-Hii hutokana na kemikali sumu zilizomo katika moshi wa tumbaku kuumiza taratibu njia za hewa na kuanza kuleta mabadiliko ya saratani. 
-Saratani ya mapafu imekuwa ni moja ya saratani ambazo huathirika zaidi kutoka na moshi huu huku zingine zikiwa ni pamoja na saratani za mdomo, umio, tumbo, kongosho, utumbo mpana, figo na kibofu cha mkojo.
2. Huathiri mbegu za uzazi za mwanaume.
-Mabdiliko mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanaume yameweza kuonekana kutokana na athari ya kemikali sumu za tumbaku katika mfumo ikiwemo;
  • Kutengeneza shahawa zisizo na umbo kamili
  • Shahawa zenye uwezo mdogo wa kutembea
  • Kutengeneza shahawa chache na zisizojitosheleza n.k
-Yote haya ni huweza kumfanya mwanaume kutokuwa na uwezo wa kumpa mimba mwanamke na lakini zaidi huweza kupunguza nguvu za kiume pia.
3. Huathiri mfumo wa uzazi wa mwanamke
-Athari mbalimbali katika mfumo wa uzazi zimeweza kuonekana zikiwemo kama;
  • Kuharibu mzunguko wa hedhi kwa kutokuwa wa kuhakika katika siku
  • Kupunguza kiwango cha homoni za uzazi (Estrogeni) katika mwili.
  • Kupelekea kufunga mzungo katika umri wa mapema.
-Mabadiliko yote haya huweza kusababisha mwanamke kutokuwa na uwezo wa kushika mimba.
4. Kuharibu mimba na mtoto aliyeko tumboni.
-Uvutaji wa tumbaku kabla na wakati wa ujauzito hupelekea athari nyingi mengi zikiwemo;
  •  kuharibika kwa mimba katika miezi ya mapema 
  • kutungwa kwa mimba nje ya mfuko wa uzazi, 
  • kuzaa mtoto mwenye hitilaju nyingi sana zikiwemo za mtoto mwenye uzito mdogo sana kuliko kawaida
-Haishauri kutumia kabisa tumbaku au sigara kwa mama mjamzito kwani madhara yake ni mengi sana ya zaidi ya hayo yaliyotajwa.
5.  Kupata mivunjiko ya mifupa
-Madhara haya yameonekana sana kwa wanawake kutoka na athari ya tumbaku ya kupunguza homoni ya Estrogeni mabayo hupelekea mifupa kupungukiwa uimara wake na hiyo kuwa kwenye hatari ya kupata mivunjiko ya mifupa ya nyonga n.k
-Kuanza kuvuta sigara kwa zaidi ya miaka 10 hupunguza athari hii ya mifupa.
6. Huchangia kwa maradhi ya moyo.
-Athari za tumbaku ni nyingi sana katika mfumo mzima wa moyo na mishipa ya damu huku uvutaji wa sigara ukiwa unachangia kwa zaidi ya 10% ya vifo vyote vitokanavyo na maradhi ya moyo
-Na hii hutokana na moshi wa sigara/tumbaku kupelekea;
  • Kusinyanyaa kwa mishipa ya damu ya moyo
  • Kuongeza hali ya damu kuganda
  • Kuharibu kuta za mishipa ya damu n.k
-Mabadiliko hasi yote hayo hupelekea kwa ongezeko la shambulizi la moyo, kiharusi na hata vidonda sugu katika miguu huku matatizo haya yakionekana kuongezeka zaidi miongoni mwa wavuta sigara kuliko wasiovuta.
7. Kupelekea kwa maradhi sugu ya mapafu
-Mbali na saratani ya mapafu, wavutaji wa sigara huweza kupata athari ya moja kwa moja ya kwenye mapafu kw kuyafanya mapafu kushindwa kufanya kazi yake.
-Mababdiliko ya sehemu mbalimbali za mapafu ni moja ya chanzo cha maradhi haya na humfanya mtu kushindwa kuhema vizuri, kifua kupana na kupata kikohozi cha muda mrefu takribani miaka 2 pamoja na dalili zingine.
8. Kushambuliwa na vimelea vya magonjwa.
-Uvutaji wa tumbaku unapelekea watu wengi kupatwa na vimelea vya magonjwa hasa vya bakteria ambapo huweza kusababisha mtu kupata kirahis maradhi kama kifua kikuu, pneumonia, mafua ya mara kwa mara n.k 
8. Huchangia kwa vidonda vya tumbo.
-Tafiti zimeonesha kuwa vidonda vya tumbo na utumbo vimeoneka kutokea zaidi kwa watu wanaovuta sigara au tumbaku kuliko wasiovuta
-Lakini pia utumiaji wa sigara umeoneka kuchangia kwa kushindwa kwa matibabu ya dawa za vidonda vya tumbo.
9. Hupelekea ugonjwa wa Kisukari.
-Moja ya kemikali sumu iliyopo kwenye sigara inaitwa nikotini, kemikali hii imeoneka kuathari utendaji kazi wa homoni ya Insulini kiasi cha kupelekea ongezeko la sukari katika damu na hivyo kupata ugonjwa wa kisukari aina ya pili.

10. Maradhi ya kinywa na meno.
-Meno pamoja na fizi huaribika kutokana na uvutaji sigara na kupelekea kupoteza meno. Tafiti zimeonyesha waathirika wengi wa meno na fizi kuwa ni wavutaji sigara huku athari hii ikipungua kadiri miaka inavyoongezeka tangu kuacha uvutaji. 
11. Hupunguza uwezo wa macho kuona.
-Athari ya matumizi ya sigara au tumbaku ni pamoja na kuathiri lensi ya jicho (kuonekana kama yenye ukungu hivi) na sehemu ya retina ambapo kwa ujumla hupelekea macho kutoona vizuri na zaidi huweza kusababisha upofu.
12. Kuchelewa kwa vidonda kupona.
-Matumizi ya sigara au tumbuka  huchangia kwa kiasi kikubwa kuchelewa kwa vidonda kupona hasa mara baada ya kujiumiza au kufanyiwa upasuaji fulani. 
-Kuacha uvutaji wa sigara kumenonekana kusaidia kupona vidonda kwa haraka.
13. Kuatharika kwa maungio mwilini.
-Uvutaji wa tumbaku umehusishwa na kupata hitilafu ya maungio ya sehemu mbalimbali hasa mikononi. Hali hii hupelekea maumivu makali ya viungo pamoja na kuharibu muonekano wa maeneo hayo.
-Hii imeonekana kwa watumiaji wa sigara au tumbaku kwa zaidi ya miaka 20.

14. Kifo.
-Kutoka na maradha mengi yanayotokana na uvutaji wa sigara au tumbaku watu wengi hupoteza uhai katika umri mdogo kabisa kwani uvutaji wa sigara wenyewe tu hupunguza miaka ya kuishi ukilinganisha na mtu asiyevuta sigara.
Ni wajibu wa kila mtu kufahamu madhara haya makubwa ya uvutaji tumbaku ili kuweza kupata hamasa ya kuacha uvutaji au kutojaribu kabisa kuvuta kama hujaanza. Matumizi ya tumbaku ni hatari kwa afya yako.
-
Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.