WASILIANA NA DAKTARI UONAPO DALILI HIZI MARA BAADA YA KUANZA KUTUMIA DAWA ZA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU (PRESHA YA KUPANDA)

 Utumiaji wa dawa za shinikizo la juu la damu ni moja ya matibabu ya tatizo hili sambamba na kuzingatia mtindo bora wa maisha. Lengo kuu ni kuweza kudhibiti vizuri shinikizo la juu la damu katika kiwango kinachotakiwa ili kuepuka madhara makubwa yatokanayo na shinikizo la juu la damu. Dawa mbalimbali zimekuwa zikitolewa kwa wagonjwa wa shinikizo la juu la damu kwa mafanikio makubwa sana huku wagonjwa wengi wakitumia dawa hizi kwa muda mrefu sana bila ya kuacha. 

Dawa hizi kama ilivyo kwa dawa zingine zinaweza kukuleta madhara madogo madogo hadi makubwa licha ya kukutibu vyema shinikizo la juu la damu, baadhi ya madhara haya unayoweza kurudi na kuripoti kwa daktari ni pamoja na;

1. Kupungua kwa nguvu ya uume.

-Hii imekuwa ni changamoto kubwa sana kwa baadhi ya wagonjwa kutokana na baadhi ya watu kupatwa na tatizo hili la uume kulegea kutokana na matumizi ya dawa za presha ya kupanda. 

-Si dawa zote ambazo zinapelekea hali hii bali ni baadhi tu na hali hii ya kupungua kwa nguvu za kiume si wagonjwa wote hupatwa licha ya dawa ile ile inayotumika kwa wengine pia.

2. Kikohozi kikavu 

-Baadhi ya dawa za presha ya kupanda hupelekea baadhi ya wagonjwa wa shinikizo la juu la damu kuanza kupata kikohozi kikavu ndani ya siku hadi wiki chache tangu kuanza kutumia. 

-Hali hii inakuwa ni usumbufu kwa mgonjwa na kumkosesha amani. Ni vizuri mtumiaji wa dawa kuweza kuwa na utambuzi wa karibu sana wa dawa zote anazotumia na kuona ni dawa ipi inamletea shida hii ili kuweza kubadilishiwa. 


3.  Kuvimba macho na mdomo

-Hali hii huweza kuwatokea baadhi ya wagonjwa mara baada ya kumeza dawa za shinikizo la juu la damu. Hii hutokana na uzio katika dawa hizo ambapo kimiminika hujikusanya baadhi ya maeneo ya mwili hasa mdomoni, machoni, kwenye koo, kwenye korodani n.k

-Upatapo hali hii mara baada ya matumizi ya dawa, onana haraka na mtaalamu wa afya kwa matibabu sahihi na kuweza kupata dawa mbadala.

4.  Kichwa kuuma sana.

-Maumivu makali sana ya kichwa hasa mara baada ya kumeza baadhi ya dawa za presha ya kupenda huwasumbua baadhi ya wagonjwa. 

-Hali hii inaweza kupoa kwa muda tu mara baada ya kutumia dawa za kutuliza maumivu na kisha kurudi. Endapo usipomeza dawa hizo huwezi kusikia maumivu yoyote ya kichwa.

5. Kutopata usingizi .

-Ikiwa kabla ya matumizi ya dawa za shinikizo la juu la damu, mgonjwa ulikuwa unapata usingizi vizuri kabisa kisha ukaanza kuona mabadiliko makubwa zaidi ya kutopata usingizi hasa baada ya kuanza kutumia dawa. Inawezekana ikawa inachangiwa na umezaji wa baadhi ya dawa za presha ya kupanda. 

-Usingizi bora ni afya, rudi kwa mtaalamu wa afya na ripoti hali hii kuweza kujadiliana na daktari.

6. Miguu kuvimba

-Moja ya madhara ya dawa hizi yameweza kuonekana kwa wagonjwa wengi ni kuvimba miguu baada ya kuanza kutumia dawa za shinikizo la juu la damu. 

-Wengine miguu hujaa kiasi cha kuwa shida katika kutembea, hivyo usikae kimya  bali fika kwa mtaalamu wa afya na kutoa taarifa.

Matumizi ya dawa kudhibiti shinikizo la juu la damu yana faida kubwa sana kuliko madhara yake kwani hukuepusha na magonjwa ya kiharusi, shambulizi la moyo, na hata kifo katika umri wa mapema. Madhara haya ya dawa ni muhimu kuyaripoti kwa daktari kwa uchunguz zaidi na tiba sahihi kwani  madhara haya si mahususi kwa dawa hizi pekee.

Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.