Unapokuwa katika programu ya mazoezi kumbuka kuwa ni lazima kufuata mtiririko sahihi wa mazoezi yani kuanza na kupasha mwili, mazoezi yenyewe kisha kupoza mwili. Taratibu hizi ni za muhimu sana katika kusaidia kufikia malengo yako na kuwa imara huku ukijiepusha na athari ndogo ndogo za mazoezi. Inapofikia hatua ya kufanya mazoezi yenyewe ambapo ndio muda sahihi mwili unatumika zaidi, hivyo unaweza kuwa imara katika sehemu kwa kuzingatia maboresho ya mambo haya;
1. Ongeza idadi ya siku za mazoezi katika wiki
-Ili kuweza kuona ubora wako unakuwa mkubwa ni pamoja na kuongeza idadi ya siku za kufanya mazoezi mfano kutoka siku 1 mpaka kwenda siku 3 au 4 katika wiki. Hii itakupatia muda wa kutosha wa kuendelea kujiimarisha zaidi na zaidi.
-Siku hizi unaweza kuziachanisha ili kuweza kuupa muda mwili kupumzika pia. Kuendelea kufanya mazoezi kwa idadi ya siku zile zile kwa kipindi kirefu sana si ishara nzuri ya maendeleo katika mazoezi.
2. Ongeza kiasi au ukubwa wa mazoezi.
-Kama ndio unaanza si vyema kuanza na mazoezi magumu bali ni muhimu sana kuanza na mazoezi mepesi ili kujiepusha na kujiumiza wakati wa mazoezi.
-Ili kujiimarisha zaidi inabidi uweze kutoka katika mazoezi mepesi kwenda katika mazoezi ya wastani na mwisho kufanya yale magumu. Uzuri ni kwamba kadiri unavyofanya mazoezi mwili huimarika na huweza kwenda katika hatua zingine.
-Kwa mazoezi ya kunyanyua vitu vizito basi unaanza na uzito mwepesi kwa siku za awali kisha ziku za mbeleni unaongeza uzito
-Usigande eneo moja kwa muda mrefu sana kwani haitakujengea ubora wowote.
3. Ongeza muda unaofanya mazoezi katika siku.
-Katika mazoezi kila dakika ina dhamani kubwa na kadiri mwili unavyoendelea kufanya mazoezi unaimarika na kuzoea mazoezi husika
-Badala ya kuendelea kutumia dakika 30 kwa mazoezi ya aerobiki basi ongeza hadi dakika 60, badala ya kufanya dk 75 za kunyanyua uzito basi unaongeza mpaka dk 100.
-Ongezeko la muda hukufanya uweze kuendelea kuimarika zaidi na zaidi tofauti na muda wa awali.
4. Lenga kufanya aina husika ya mazoezi kwa wakati mmoja.
-Kuchanganyachanganya mazoezi hakushauri kwani kunakufanya unakosa kumakini zaidi katika aina ya mazoezi na hivyo kutofanya mazoezi kwa ufasaha na kushindwa kuendelea.
-Jambo la msingi ni kufanya aina ya mazoezi husika kwa wakati unaotakiwa na kisha kuhamia aina nyingine ya mazoezi. Mfano fanya mazoezi ya nguvu za misuli kwa dk 30 kisha hamia kwenye mazoezi ya aerobiki kwa dk 30 tena
-Hii husaidia kutendea haki aina ya mazoezi na kuwa imara kwa haraka zaidi katika mazoezi husika.
Kufuata kanuni na taratibu za mazoezi kwa ujumla wake husaidia sana kupata kunufaika na matokeo ya kiafya ya mazoezi lakini pia huweza kupata ujuzi utokanao na mazoezi haya. Siku zote lenga katika kufika mbali zaidi katika mazoezi kwa kuboresha angalau kimoja wapo au vyote vilivyotajwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni