Matatizo mengi ya kiafaya yamekuwa yakichangiwa na lishe ambayo si sahihi na hii hutokana na watu wengi kutofahamu nini cha kufanya ili kufanikisha mlo kamili. Kufanikiwa katika ulaji bora ni pamoja na kuzingatia vidokezo mbalimbali vya ulaji vinavyopendekezwa na wataalamu wa lishe. Hii husaidia katika kufanikisha malengo yako mengi ya kiafya yatokanayo na lishe bora.
Kupata matokeo bora katika lishe yako ni vyema kuzingatia mambo yafuatayo;
1. Andaa mlo wenye angalau chakula kimoja kutoka katika kila kundi la vyakula.
-Vyakula viko katika makundi tofauti tofauti na kila kundi likiwa na umuhimu wake kiafya. Kupata virutubisho vyote na sahihi inatakiwa kuchukua chakula angalau kimoja katika makundi haya na kuandaa mlo wako, makundi haya ni;
- Nafaka isiyokobolewa, ndizi na vyakula vya mizizi
-Vyakula vya mizizi ni pamoja na mihogo, magimbi, viazi vitamu, viazi mviringo na vikuu.
-Vyakula hivi huwa na kiasi kikubwa cha makapi na vina sukari iliyo salama zaidi.
- Mboga za majani na Matunda
-Kuna matunda mbalimbali unawez akuyaanda katika mlo wako ikiwemo; ndizi, maembe, nanasi, parachichi, tikitimaji, mapapai, mapesheni, machungwa n.k
- Vyakula vya jamii ya kunde
- Vyakula vya asili ya wanyama
-Hapa hujumisha haswa vyakula kama maziwa, nyama isiyo nyekundu (bata, kuku), samaki, mayai,mayai, karanga n.k
- Mafuta na sukari
2. Epuka vyakula vyenye mafuta mengi yasiyo salama kiafya.
-Mafuta kutoka kwenye siagi, mafuta ya nazi na mchikichi pamoja na vyakula vya kukaanga, piza, keki, biskuti n.k si salama kwani huchangia kwa maradhi ya moyo na mishipa ya damu.
-Badala ya kukaanga unaweza kuoka au kuchemsha vyakula.
3. Nusu ya sahani yako iwe ni mboga za majani na matunda.
-Vyakula hivi ni vizuri sana kiafya kwani huwa na virutubisho vingi vya vitamini, madini, sukari asili na makapi ambavyo vyote kwa pamoja husaidia kuulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo, saratani, kisukari n.k
4. Nusu ya nafaka unayoitumia iwe ni nafaka isiyokobolewa.
-Nafaka iliyokobolewa hupoteza ubora wake kwa kupungukiwa na virutubisho kama makapi ambayo ni muhimu sana mwilini.
-Pia nafaka iliyokobolewa hubaki kuwa na kiwango kingi cha sukari na hivyo kutokuwa salama sana kwa matumizi.
-Nafaka isiyokobolewa kama unga wa dona na unga wa ngano ni bora kiafya siku zote.
5. Epuka matumizi ya chumvi kupita kiasi.
-Kiasi kingi cha chumvi huingizwa mwilini kupitia ulaji wa vyakula kutoka viwandani kama nyama za makopo, maharagwe ya makopo n.k,
-Pia kupindi cha upishi majumbani na wakati wa kula, chumvi nyingi huweza kutumika.
-Punguza kiwango cha chumvi hadi kijiko kimoja cha chai au chini ya hapo kwa siku ili kuwa salama dhidi ya maradhi ya moyo.
6. Epuka ulaji wa sukari ya kuongezwa.
-Siku hizi vyakula ni vingi sana vinavyoongezewa sukari huko viwandani kama vile; soda, jamu, biskuti, juisi, keki, chokoleti n.k.
-Aina hii ya vyakula ni ya kuepuka kwani huwa na sukari ambayo si salama kifya dhidi ya magonjwa yakuambukizwa kutokana na kuwa chanzo cha uzito wa uliopitiliza au unene kwa watu wengi.
7. Kunywa maji safi na salama.
-Maji ni muhimu sana kuwa sehemu vya mlo wako kila siku ingawa si sehemu ya virutubisho. Bila ya maji mwili hauwezi kufanya kazi ipasavyo. Kunywa maji ya kutosha kila siku kulingana na uzito wako, hali ya hewa, shunguli zako n.k.
Mambo yaliyotajwa hapo juu yote yanajumuisha suala la mtindo wa ulaji bora , na kwa kuzingatia hayo ni wazi kabisa utakuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kuepuka maradhi sugu yasiyoambukizwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni