Kujiumiza katika mazoezi ni suala ambalo huweza kutokea pasipokutarajia licha ya tahadhari mbalimbali zinazochukuliwa kipindi cha mazoezi. Kupasha mwili kabla ya mazoezi yoyote ni namana muhimu sana katika kupunguza nafasi ya kujiumiza pindi mazoezi yanafanyika. Endapo imetokea umejiumiza wakati wa mazoezi, jitahidi kufanya yafuatayo
1. Pumzika.
-Acha kuendelea na mazoezi mara tu ya kutambua umejiumiza katika sehemu fulani ya mwili kwani kuendelea na mazoezi huweza kupelekea maumivu zaidi, uvimbe kuongezeka na hata kuchochea damu kutoka eneo hilo.
-Katika kipindi hiki cha kupumzika unaweza kutumia magongo ili kupunguza uzito katika eneo lililoumia kama ni sehemu za mguuni na kumbuka kupumzisha eneo lililoumia kwa kuuzungushia chochote ili pasitikisike mara kwa mara.
-Tafiti pia zimeonesha katika kipindi hiki inatakiwa muda mwingi upumzishe eneo lililoumia lakini muda mwingine utumie kuuchezesha kidogo ili kusisimua uponaji wa haraka eneo hilo.
-Matumizi ya barafu ni muhimu pindi unapoumia kwani husaidia katika kupunguza maumivu na kuvimba kwa eneo hilo kutokana na uwezo wa barafu kupunguza mzunguko wa damu mahali palipoumia.
-Matumizi ya barafu ni kama ifuatavyo
- Chukua kipande cha wastani cha barafu kisha kiweke kwenye mfuko laini.
- Kipande hicho ndani ya mfuko laini kizungushie kwenye kitamba laini kisha weka na shikilia kwenye eneo liloumia kwa takribani dk 20 kisha toa
- Mara baada ya kutoa subiria baada ya dk 20 kisha rudia kuweka kwenye eneo hilo
- Rudia huu mzunguko ndani ya masaa matatu na endapo maumivu yatakuwa bado hayajapungua basi omba msaada kwa mtaalamu wa afya.
3. Kandamiza kiasi eneo lililoumia.
-Inashauriwa kutumia bandeji kuzungushia eneo lililoumia ili kupungua kiasi cha kuvimba eneo hilo kwani bandeji kuzui mkusanyiko mwingi wa damu katika shemu iliyoumia.
-Ni muhimu kuepuka kukandamiza sana ili kutozuia damu kufika eneo husika na hivyo kuleta madhara makubwa zaidi. Legeza bandeji wakati wa usiku.
-Dalili za kukandamiza sana hadi kuathiri mzunguko wa damu ni pamoja; ganzi, maumivu kuwa makali zaidi ya awali, kupauka kwa rangi eneo la mbele kutoka ulipofungia bandeji. Mara uonapo dalili hizi fungua bandeji haraka sana mpaka dalili hizo zitakapopotea kisha funga kwa kulegeza safari hii.
4. Inunua juu eneo lililoumia.
-Inashauri kuinua sehemu uliyoumia juu kutoka usawa wa moyo kwani ni moja ya njia ya kutuliza maumivu na kupunguza kuvimba hasa nyakati za usiku.
-Unaweza kutumia kitu chochote laini kama mto au taulo kuweza kuinua sehemu hii ambayo tayari imewekewa barafu na kukandamizwa vizuri.
Njoo hizi ni muhimu kwa huduma ya awali lakini pia endapo hujajiumiza sana kiasi cha kwenda hospitali kwa matibabu. Kumbuka endapo utakuwa umeteguka au kuvunjika sehemu fulani ni lazima kufika hospitali haraka sana kwa ajili ya matibabu zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni