ATHARI KUMI (10) ZA KIAFYA ZA UVUTAJI WA SIGARA KWA MWANAMKE KABLA, WAKATI NA BAADA YA UJAUZITO.

 Uvutaji wa sigara ni moja ya mambo hatarishi ambayo huweza kuathiri moja kwa moja mfumo wa uzazi wa mwanamke kuanzia katika kushika mimba, wakati wa mimba yenyewe na hata baada ya mimba. Moshi wa sigara umekuwa ukivutwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kama sigara za kuwasha na moto, sigara za umeme, sisha n.k. Moshi wa sigara umekuwa ukiwaathiri hadi watu wa pembeni ambao hawavuti moja kwa moja, na hii pia imechangia kwa madhara ya kiafya kwa watu hawa. Takribani wanawake milioni 250 huvuta sigara duniani huku asilimia 22 ikiwa ni wanawake katika nchi zilizoendelea na aslimia 9 ni wanawake kutoka nchi zinazoendelea. 

Zifuatazo ni athari mbalimbali za kiafya katika mfumo wa uzazi wa mwanamke zitokanazo na uvutaji wa sigara 

1. Kutoshika mimba kirahisi (Ugumba)

-Kemikali mbalimbali zinazopatikana katika moshi wa sigara zimeonekana kuwa hatari katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kupelekea kupunguza utengenezaji wa mayai ya kike na pia hupelekea utengenezaji wa mayai ambayo hayajakomaa.

- Hali hii imechangia kwa wanawake wengi kushindwa kushika ujauzito kama awali kabla hawajaanza uvutaji wa sigara.

2. Kuharibika kwa mimba.

-Uvutaji wa sigara umeonekana kuwa na mchango katika kuharibika (kutoka) kwa mimba hasa kabla ya kufikisha wiki 28 (kwa Tanzania). Hii pia imeonekana kuwaathiri hata kwa wale wanawake ambao huvuta moshi kutoka pembeni.

-Kemikali sumu katika sigara zimekuwa na madhara makubwa katika mfumo mzima wa kondo (placenta) ambao huweza kupelekea mimba kuharibika

3. Kusababisha kifo cha mtoto akiwa tumbo au baada ya kuzaliwa.

-Sumu mbalimbali katika sigara kupelekea kuathiri ukuaji wa mtoto tumboni na hivyo kusababisha kifo cha mtoto angali tumboni au mara baada ya kuzaliwa. 

-Tafiti zimeonesha kuwa uvutaji wa sigara huchangia kwa asilimia 50 ya watoto kufia tumboni huku asilimia 20 ikichangia watoto wengi kufa ndani ya siku 28 baada ya kuzaliwa.

4. Kupasuka kwa chupa la uzazi kabla ya mimba kutimia muda wake.

-Tafiti zimebaini kuwa uvutaji wa sigara huweza kuchangia kwa kiasi kikubwa chupa au mfuko wa uzazi kabla ya wiki 37 (sawa na miezi 9) ambapo mtoto anakuwa bado hajakomaa ipasavyo.

-Athari hii huenda sambamba na kadiri idadi ya sigara inayovutwa kwa siku inavyoongezeka huku ikibainika kuwa utumiaji wa sigara kuanzia 10 na kuendelea kwa siku huwa na athari kubwa katika suala hili.

5. Kujifungua watoto wenye uzito mdogo (Njiti)

-Kemikali sumu husababisha athari katika ukuaji wa mtoto pindi anapokuwa bado yuko tumboni na hivyo hupelekea kujifungua mtoto ambaye uzito wake ni mdogo (chini ya kilo 2.5) ukilinganisha na umri wake.

-Mwanamke anayevuta sigara moja kwa moja na yule ambaye huvuta moshi wa mtu wa pembeni wote huwa katika uhatari wa kuzaa watoto wa aina hii.

6. Hitilafu ya kondo wakati wa ujauzito.

-Matatizo ya kuvuja damu katika uke kipindi cha ujauzito baada ya wiki 20 ya mimba hutokea kutokana na hitilafu tofauti tofauti za kondo la mimba ambapo hitilafu hii imeonekana kuchangiwa na matumizi ya sigara.

-Hitilafu hizi za kondo zipo za aina tofauti tofauti ambapo zingine ambapo;

  • Kondo linawezaka kutokuwa eneo lake sahihi (eneo la siku zote kwenye mimba ya kawaida)-Pracenta previa
  • Kondo linaweza kung'atuka katika eneo lake-Placental abruption, na zingine ambazo ni aghalabu

-Hitilafu hii inapotokea ikihusisha upotezaji mkubwa wa damu basi huweza kupelekea mimba kuharibika hivyo kupoteza mtoto tumboni.


7. Kujifungua kabla ya wiki 37 (miezi 9)

-Tafiti zimeonesha kuwa uvutaji wa sigara umechangia kwa wanawake wengi kujingua kabla ya muda wa mimba kutimia hukuwa uwezekano wa kujifungua ukionekana hasa kabla ya wiki 32 ya ujauzito. 

-Tatizo hili huchangia kwa kuzaa watoto ambao hawajakomaa vizuri baadhi ya viungo, wenye uzito mdogo n.k hivyo kuwaweka katika mazingira ya kupata maradhi kirahisi.

-Ikumbukwe tu kujifungua kabla ya wiki 37 inaweza ikasababishwa na mambo mengine mengi tu.    

8. Kujifungua mtoto wenye kasoro mbalimbali.

-Uvutaji wa sigara huweza kuchangia kwa kasoro mbalimbali za mtoto atakayezaliwa huku kazi ya vinasaba ikihusishwa katika kutokea kwa kasoro hizo.

-Kasoro kama midomo ya sungura, mkundu kutojengeka, uwazi wa ukuta wa tumbo, vidole vya ziada, hitilafu katika moyo n.k

-Utokeaji wa kasoro umeonekana kwenda sambamba na kadiri unavyowahi kuvuta sigara yani uvutaji wa sigara katika miezi mitatu ya mwanzo huongeza uwezekano wa kupata kasoro katika viungo vya mtoto.

9. Huchangia kwa Kisukari cha ujauzito.
-Pamoja na vihatarishi vingine, uvutaji wa sigara huchangia katika kuibuka kwa maradhi ya kisukari wakati wa ujauzito ukilinganisha na wanawake ambao hawatumii sigara.
10. Kutopata maziwa ya kutosha.
-Kiwango cha maziwa ya mama baada ya kujifungua hupungua sana kutoka na uvutaji wa sigara kipindi cha ujauzito na hii hupelekea unyonyeshaji hafifu wa mtoto na ndani ya muda mfupi.

Mwanamke ambaye anatarajia kupata ujauzto na mama mjamzito hatakiwi kutumia sigara kabisa na anatakiwa kujiepusha na moshi wa sigara kutoka kwa wavutaji wa pembeni hasa wazazi wenza. Hii itasaidia sana kuepuka madhara mbalimbali zaidi ya yaliyotajwa hapo juu. Na kama mwanamke ameshaanza uvutaji basi sasa hivi ni muda sahihi wa kuacha kwa kuoana na daktari atakaye kusaidia.

Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.