Unywaji wa pombe hasa unywaji wa kupitiliza ni hatari kwa afya kwani unywaji huu umekuwa ukihusishwa na madhara mbalimbali ya kiafya. Unywaji wa pombe huchangia kwa vifo vya watu takribani milioni 3 duniani pia kudhoofisha afya ya watu wengi kwa ujmla. Pombe imekuwa ikiathiri hasa watu katika umri wa miaka 15 mpaka 49 huku wanaume (7.1%) wakiathiriwa zaidi kuliko wanawake(2.2%).
Kiuhalisia ni kuwa pombe imekuwa moja ya vyanzo vya aidha moja kwa moja au visivyo moja kwa moja vya magonjwa mbalimbali katika mwili wa binadamu takribani zaidi ya magonjwa 30. Zaidi unywaji wa pombe unaweza kupelekea hata madhara kwa watu wengine ambao si wahusika wa kutumia pombe hiyo. Madhara ya kiafya yatokana na unywajiwa kupitiliza wa pombe ni kama ifuatavyo katika makundi yake.
1. Saratani
-Tafiti mbalimbali zimeonesha uwepo wa uhusiano wa unywaji wa kupitliza wa pombe na baadhi ya saratani.
-Saratani ambazo zimeweza kuripotiwa zikiwa na uhusiano na matumizi ya pombe ni pamoja na saratani ya; Koo, Mdomo, Tumbo,Ini, Utumbo mpana,Matiti, tezi dume, n.k
Saratani ya Ini |
2. Ugonjwa wa kisukari
-Unywaji wa pombe kupindukia kumechanga sana kwa ugonjwa wa kisukari ambapo ugonjwa huu unaibuka kwa kiasi miongoni mwa watu
-Tafiti mbalimbali zimeweza kufanyika kwa makundi mbalimbali na kuweza kubaini kuwa watu waliokuwa na unywaji wa pombe kupita kiasi walikuwa na nafasi kubwa ya kupata ugonjwa huu . Hii inaweza pia kuchangiwa na madhara ya pombe kuongeza uzito na mafuta mwili
3. Shinikizo la juu la damu
-Unywaji wa pombe kupitiliza umehusishwa na kuibuka kwa tatizo la shinikizo la juu la damu na kuendelea kuwa moja ya changamoto zinazoathiri udhibiti wake kwa wagonjwa hawa wenye shinikizo la juu la damu
-Kwa mgonjwa mwenye shinikizo la juu la damu ni muhimu kuepuka pombe au kunywa kwa kiwango cha wastani kinachoshauriwa.
4. Shambulio la moyo
- Pombe imeweza kuhusishwa na matukio ya shambulio la moyo ambapo mishipa ya damu ya moyo inashindwa kupata damu ya kutosha na hivyo kufanya moyo kushindwa kufanya kazi. Hii inawezekana inatokana na kupanuka kwa moyo kutoka na shinikizo la juu la damu la muda mrefu.
-Pia kumekuwa na uhusiano wa kiwango cha unywaji pombe na suala la kuathiri mfumo wa umeme wa moyo ambapo huweza kupelekea moyo kushindwa kudunda inavyotakiwa na kusababisha kifo cha ghafla.
5. Kiharusi
-Pombe huwa athari katika shinikizo la damu ambalo huathiri kwa kiasi kikubwa mishipa ya damu sehemu mbalimbali katika mwili ikiwemo mishipa ya kwenye ubongo.
-Kuathirika kwa mishipa ya damu katika ubongo huweza kuepekea kupata kiharusi.
6. Maradhi ya akili
-Matumizi ya pombe kupitiliza yameweza kuhusishwa na kuibuka kwa magonjwa ya akili huku hali ya utegemezi wa pombe ikiwa inahusishwa sana kama chanzo cha baadhi ya dalili.
-Pombe huweza kupelekea mtu kupata hali ya sonona na wasiwasi ambavyo vyote mwisho wa siku huathiri utendaji wa kazi za kila siku wa muhusika.
-Unywaji wa pombe kupindukia kwa muda mrefu huweza kupelekea magonjwa ya akili ambapo mtu hupatwa na hali ya kuchanganyikiwa, lakini pia pombe imeonekana kusababisha kupatwa na degedege.
7. Kuharibu Ini na Kongosho
-Ini na kongosho ni viungo muhimu sana katika mwili wa binadamu kutokana na kazi kubwa zinazofanywa na viungo hivi.
-Unywaji wa pombe kupitiliza unaweza kupelekea ini na kongosho kuumia moja kwa moja na kufanya viungo hivi kushindwa kufanya kazi na kuhatarisha maisha ya mtu.
-Baadhi ya matokeo ya muda mrefu ya athari za pombe kwenye ini na kongosho ni kupelekea saratani za viungo hivi lakini ini inaweza kuathirika kwa kunywea (kupungua ujazo) hali ambayo kwa kiingereza inaitwa Cirrhosis.
8. Mawe kwenye mfuko wa nyongo
-Matumizi ya pombe kupitiliza huchangia kwa ongezeko la wagonjwa wenye mawe katika mfuko wa nyongo hali ambayo hupelekea maumivu ya makali sana upande wa kulia wa juu wa tumbo.
9. Udhaifu wa mifupa
--Tafiti zimeonyesha unywaji wa pombe kupitiliza humeonekana kuathiri mifupa kwa kuifanya kuwa dhaifu na hivyo kuweza kusababisha uwezekano mkubwa wa kuvunjika mifupa hiyo.
10. Gauti
-Kunywa pombe kupindukia imeoneka kuchochea kwa ugonjwa wa gauti (baridi yabisi) ambao huathiri maungio mbalimbali ya mwili kwenye miguu na hata mikono kwa kusababisha maumivu makali na kuvimba kwa maungio haya.
-Kama tayari una tatizo hili ni vyema basi kuacha pombe au kupunguza unywaji wa pombe kama inavyoshauriwa.
12. Kuathiri mtoto tumboni kwa mama mjamzito
-Unywaji wa pombe kwa mama mjamzito ni hatari mno kwani athari yake kwa mtoto haiwezeki kurekebishwa.
-Pombe kwa mama mjamzito hupelekea kuathiri ubongo wa mtoto na hata kusababisha kutojengeka vizuri kwa viungo vya kichwa.
-Mtoto hupata shida katika ukuaji na kuwa na matatizo ya akili kutoka na athari ya pombe katika mfumo wa fahamu.
-Athari kubwa ya pombe hutokea katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ambapo mtoto ndio anajengeka
-Acha pombe sana ewe mama mjamzito kwa ustawi bora wa mtoto.
13. Kupoteza kumbukumbu
-Tafiti zimeonesha kuwa unywaji wa pombe wa kupindukia unaweza kuathiri ubongo na hivyo kupelekea tatizo la kupoteza kumbukumbu mara kwa mara.
-Hali hii huweza kuchangia hata katika kupunguza ufanisi wa kazi za kila siku ofisi au shuleni.
14. Kujiumiza kwa ajali au vurugu.
-Moja ya mambo ambayo pombe husababisha ni kupoteza uwezo wa kudhibiti mazingira ya nje ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi sahihi, hii huendana sambamba na kiwango cha pombe unachokunywa.
-Hali hii huweza kupelekea mambo mbalimbali kutoka kama vile ugomvi, ajali ya gari n.k ambapo hupelekea kujiumiza sehemu za mwili au kupata ulemavu wa kudumu.
Suala la kuacha pombe ni muhimu sana kwa afya bora kutokana na ukweli ni kwamba athari ni nyingi zaidi ya hizi zilizotajwa hapa zikigusa nyanja mbalimbali za kiafya, kiuchumu, kisaikolojia na kijamii. Kama umeshaanza unywaji wa pombe kwa muda mrefu basi ni vyema kuonana na daktari kwa ajili ya kujadili namna bora ya kuacha na kama hujaanza kunywa basi unashauriwa usijaribu kuanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni