Mazoezi ni sehemu ya mtindo bora wa maisha ya kila siku ambayo inatakiwa kujengeka kwa kila mtu kulingana na umri, jinsia, shunguli pamoja na afya ya mtu kwa ujumla. Hii ni kutokana na kweli kuwa mazoezi husaidia kuimarisha afya ya mtu na kudhibiti magonjwa mbalimbali kama vile maradhi ya moyo, kisukari, shinikizo juu la damu, saratani n.k
Katika ufanyaji wa mazoezi watu wengi hujikuta katika ajali mbalimbali ambayo huathiri sehemu za mwili na hii huweza kuchangiwa na watu ;
- kutofuata kanuni na taratibu za mazoezi,
- kutofanya mazoezi kwa usahihi kama inavyotakiwa,
- kushindwa kutumia vifaa maalum vya mazoezi,
- kukosa umakini katika kipindi cha mazoezi n.k.
Matatizo haya huweza kumpelekea mwana mazoezi kushindwa kuendelea na mazoezi kwa siku nyingi sana na hivyo kurudi nyuma katika kuwa fiti. Yafuatayo ni matatizo yanayoweza kutokea kwa wafanya mazoezi wakiwa mazoezi;1. Kuchanika kwa misuli.
-Misuli ni tishu laini ya mwili ambayo kusinyaa na kutanuka na kupelekea mzunguko wa maungio ya mwili.
-Misuli mbalimbali ya mwili iko katika uhatari wa kuvutika sana wakati wa mazoezi na hivyo kupelekea kuchanika, hali hii husababisha maumivu makali, kuvimba, joto katika eneo lililoumia na hata kushindwa kutumia sehemu hiyo kwa muda.
-Moja ya sababu inayochangia kutokea kwa tatizo hili ni kutopasha mwili kabla ya kuanza mazoezi yenyewe.
-Misuli ya nyuma ya paja (hamstrings) na misuli ya ndani ya nyonga(hip adductors) ni moja ya misuli ambayo huathirika sana
2. Kuumia kwa tendoni ya Achilles
-Tendoni ni sehemu ngumu ambayo inafanya kazi ya kuunganisha msuli na mfupa ili kuweza kusaidia sehemu mbalimbali za mwili kuweza kutembea.
-Achilles ni jina la tendoni lenye asili ya Kigiriki ambapo tendoni hii huunganisha misuli ya nyuma ya mguu (calf) na mfupa wa kisigino.
-Tendoni hii iko sehemu ambayo ni rahisi kuumia kwa mtu yeyote ambaye atakuwa amesimama au kutembea kwa kunyooka kwa mfano kwa wakimbiaji, waendesha baiskeli, na hata wacheza tenesi hupata sana tatizo hili.
-Tendoni ya Achilles huweza kuchanika na hupelekea kuvimba, kuuma na hata kushindwa kukanyagia mguu.
3. Maumivu ya goti
-Goti ni moja ya maungio katika mwili ambalo limeundwa misuli, tendoni na ligamenti nyingi huku ikiwa na sehemu pia inayohusika katika kubeba uzito mkubwa wa mwili. Ligamenti ni sehemu ambayo inaunganisha mfupa na mfupa katika maungio.
-Goti limekuwa na sehemu ambayo ikitumika katika michezo na hivyo kulifanya kuwa katika nafasi kubwa ya kuumia ambapo inaweza kuhusisha misuli, tendoni au ligamenti.
-Maumivu makali ya goti mara nyingi hutokana na kurudia mara kwa mara aina fulani ya mazoezi kwa muda mrefu.
4. Mipasuko katika mifupa.-Tatizo hili limeonekana kwa wale wafanya mazoezi ambao hufanya mazoezi ya aina moja kwa kurudia rudia kwa kipindi cha muda mrefu na hivyo kupelekea mipasuko midogo katika mifupa inayotumika sana.
-Mifupa inayoathiriwa sana kwa tatizo hili ni ile ambayo huwa na kazi ya kubeba uzito wa mwili pia kama vile;
- Mifupa ya miguu
- Mifupa ya paja
- Mifupa ya nyonga
-Wacheza muziki na wakimbiaji wamekuwa wakikubwa na tatizo hili zaidi.
5. Maumivu ya mgongo wa chini.
-Kutofanya mazoezi kwa usahihi huweza kupelekea mgongo wa chini kuumia na kuanza hupatwa na maumivu makali ya mgongo
-Hii hutokea zaidi pale mtu anapobeba uzito na kisha kupinda mgongo badala ya miguu hali ambayo inaumiza misuli ya kwenye mgongo
-Maumivu ya mgongo huweza kutibiwa kwa kufanya mazoezi sahihi kutoka kwa mtaalamu bila hata ya kutumia dawa au matibabu mengine. 6. Maumivu ya shingo
-Shingo ni moja ya sehemu ambayo huathirika na mazoezi hasa inapotokea ufanyaji wa mazoezi pasipo usahihi kama vile kukunja au kukunjua shingo zaidi ya kawaida wakati wa mazoezi.
-Hali hii huweza kupelekea kuumiza misuli ya shingo na hivyo kusababisha shingo kushindwa kugeuka kawaida. 7. Maumivu ya kiwiko.
-Tatizo hili hutokana na mazoezi ya mara kwa mara kwa muda mrefu ya misuli ya mkono wa mbele kiasi cha kupelekea maumivu katika sehemu za maungio ya kiwiko. 8. Kuchanika kwa misuli ya bega
-Kundi la misuli ya bega ambalo limekuwa kwenye uhatari mkubwa wa kuumia au kuchanika huitwa "rotator-cuffs"
-Misuli hii husaidia katika kurusha, kushika na kuinua mkono wote pande mbalimbali na ni misuli muhimu sana katika kuimarisha maungio ya bega.
-Mazoezi ya mara kwa mara yanayohusisha misuli hii kama kuongelea, kurusha vitu vizito au kubeba uzito mkubwa katika jimu huchangia sana kwa kuumia na kuchanika kwa misuli hii.
9. Mikwaruzo ya ngozi sehemu za mikunjo
-Tatizo hii hutokea sana kwa wafanya mazoezi hasa kipindi cha joto kali ambapo jasho la mwili ni jingi kiasi cha kupelekea msuguano wa maeneo ya mikunjo na hivyo kusababisha michubuko, kuwasha na hata damu kuvilia kwenye ngozi
-Maeneo yanayoathirika sana ni kama kwenye mapaja, makwapa, shingo na makalio
Ni muhimu kuzingatia usalama wako kwanza kabla ya kuanza kufanya mazoezi yoyote kwani hii itakusaidia kujiepusha na ajali zisizo za lazima na kukufanya ufurahie mazoezi yako kila siku. Kumbuka mara zote inapotokea ajali wakati wa mazoezi na vizuri kuzingatia zile njia nne za kufanya awali (angalia post ya nyuma)kwani husaidia kwa asilimia kubwa katika kupata huduma ya kwanza na hata kutibu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni