Siko seli ni ugonjwa wa urithi wa vinasaba (DNA) vya protini ya hemoglobini (Hb) yenye hitilafu iliyoko katika chembe nyekundu za damu kutoka kwa wazazi wawili. Protini hii hufanya kazi ya kubeba na kusafirisha hewa ya oksijeni kutoka katika mapafu kwenda sehemu mbalimbali za mwili ili kutumika katika kutengeneza nguvu mwilini.
Kwa kawaida protini hii inapokuwa haina hitilafu basi hufanya chembe nyekundu kuwa na umbo la duara na endapo protini hii inapokuwa na hitilafu katika ugonjwa wa siko seli basi chembe nyekundu hizi huwa na umbo la nusu mwezi au kifaa kiitwacho mundu au kama ndizi .
Katika suala la urithi wa vinasaba kutoka kwa wazazi, mtoto hupokea kinasaba kimoja cha kutengeneza protini ya hemoglobini kutoka baba na kimoja kutoka kwa mama na hivyo kujenga pea (pair) ya vinasaba vya protini hii.
Zifuatazo ni alama ambazo hutumika katika kuelezea urithi wa vinasaba katika ugonjwa wa siko seli
- HbA- Hii ni alama inayowakilisha protini ya hemoglobini ya kawaida
- HbS- Hii ni alama inayowakilisha protini ya hemoglobini iliyo na hitilafu (yenye dosari)
Muhimu: Ili kupata mtoto wenye ugonjwa wa siko seli ni lazima wazazi wote wawili wawe wamebeba vinasaba vya ugonjwa wa siko seli yani (HbS)
Hizi ndio namna ambazo mtu anaweza kupata ugonjwa wa siko seli kutoka kwa wazazi1. Endapo baba atakuwa ana vinasaba vya HbAS na mama atakuwa na vinasaba vya HbAS
-Baba mwenye HbAS tafsiri yake ni kuwa amebeba vinasaba vya ugonjwa wa siko seli ila si mgonjwa vilevile mama mwenye HbAS amebeba vinasababa vya ugonjwa wa siko seli ila si mgonjwa.
-Ili kupata mtoto mwenye ugonjwa wa siko seli basi baba atakuwa amehusika wa kutoa HbS moja na mama atahusika kutoa HbS moja na hivyo kumrithisha mtoto HbSS
- Wazazi hawa wana uwezekano wa kupata mtoto mwenye ugonjwa wa siko seli kwa asilimia 25 miongoni mwa watoto wanne watakao zaa. |
Urithi wa siko seli kutoka kwenye wazazi waliobeba vinasaba vya ugonjwa |
Tafsiri ya watoto waliopatikana ni kama ifuatavyo i/ AA-Huyu ni mtoto ambaye mwenye protini za hemoglobini za kawaida kabisa (Kwanza kushoto)
ii/ AS- Hawa ni watoto ambao wamebeba vinasaba vya ugonjwa wa siko seli lakini si wagonjwa (Wawili katikati).
iii/ SS- Huyu ni mtoto ambaye ni mgonjwa wa siko seli (Mwisho kulia)
2. Endapo mzazi mmoja ana vinasaba vya HbAS na mzazi mwingine ana vinasaba vya HbSS.
-Inapotokea mzazi mmoja amebeba vinasaba vya ugonjwa yani ni HbAS na mzazi mwingine ni mgonjwa tayari yani HbSS basi nafasi ya kupata mtoto mwenye ugonjwa wa siko seli ni asilimia 50 miongoni mwa watoto wanne watakaozaa.-Watoto wawili wenye SS wakiwa na ugonjwa wa siko seli huku watoto wawili wenye AS wakiwa wamebeba vinasaba vya ugonjwa.
3. Endapo wazazi wote wana ugonjwa wa siko seli
-Ikitokea wazazi wote wana ugonjwa wa siko seli yani baba ana HbSS na mama ana HbSS basi ni lazima watoto wote watakuwa na ugonjwa ugonjwa wa siko seli kwa nafasi ya asilimia 100.
|
Wazazi wa katikati (nyekundu) wenye ugonjwa siko seli wanazaa watoto wote wenye ugonjwa wa siko seli pia (wanne wenye nyekundu zote) |
Ni muhimu sana kuna kutambua hali yako ya umiliki wa vinasaba vya ugonjwa wa siko seli ikoje ili kuweza kupata ushauri bora kutoka kwa daktari. Hii husaidia katika kufanya maamuzi sahihi hata katika kupata mwenza anayekufaa lakini zaidi husaidia katika kupunguza kasi ya urithishaji wa vinasaba vya ugonjwa huu ambavyo hupelekea katika ongezeko la wagonjwa wengi wenye siko seli. Endapo kuna historia ya ugonjwa wa selimundu katika familia au ukoo basi ni muda sahihi wa kufika katika hospitali ili kupata vipimo vya uchunguzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni