MAKUNDI SABA (7) YA MISULI AMBAYO UNATAKIWA KUFANYIA MAZOEZI KATIKA RATIBA YAKO

Mwili wa binadamu una misuli mingi katika mfumo wake wa mifupa ambayo inawezakufanyishwa mazoezi na kukuletea mabadiliko chanya katika afya yako kwa ujumla. Mbali na kuwa na uwepo wa misuli mingi ya kufanyika mazoezi bado watu wengi wamekufanya mazoezi yanayogusa misuli michache kutokana na kutofahamu umuhimu na makundi hayo ya misuli ambapo mwisho wa siku huishia kujiumiza na kujenga mwili ambao hauna uwiano. Unapoandaa ratiba yako ya mazoezi basi ni muhimu sana kujumuisha makundi yote ya misuli katika nyakati tofauti tofauti, makundi hayo ya misuli ni:

1. Misuli ya mgongo

-Misuli hii imegawanyika katika makundi mawili yani misuli ya mgongo wa juu na misuli ya mgongo wa chini.

-Kwa ujumla kazi ya misuli hii ni pamoja na kukusaidia kuimarisha mifupa ya uti wa mgongo hivyo kuepukana na maumivu ya mgongo yasiyo ya lazima, kukupa nguvu ya kuweza kuvuta vitu katika shughuli zako za kila siku na pia kuimarisha uwezo wa shingo lako katika kuelekeo wote.

-Vijana wengi wamekuwa wakipenda muonekana na kuwa na mbawa (wings) au umbile la V, basi misuli hii ya mgongo ndio yenyewe hasa misuli ya mgonjwa wa juu. Lakini pia kuna wanapenda kuwa na misuli ya shingo iliyojaa (Traps) basi usishau kufanya mazoezi ya misuli hii.

-Mfano wa mazoezi ya misuli ya mgongo ni pamoja na; "pulldowns na pullups", rows, pullovers, n.k

2. Misuli ya kifua

-Moja ya mazoezi ambayo yanafahamika na kufanywa na watu wengi katika jimu ni mazoezi ya kifua kwa vijana wengi wamekuwa wakitamani muonekana mzuri wa kifua.

-Kifua kimejengwa na misuli miwili ambao mmoja uko juu kabisa (pectoris major) na mwingine uko chini ya wa juu (pectoris minor), misuli hii ndio wahusika wakuu kwa mazoezi yote yanayohusu kifua.

-Misuli hii ya kifua ni kati ya misuli mikubwa mwili, hivyo inashauri kuifanyisha mapema kabla hujachoka na kwa kiwango kikubwa cha "reps"

-Mfano wa mazoezi ya misuli ya kifua ni pamoja na; Pushups za aina mbalimbali, bench press, dumbbell chest press, verical dips n.k

3. Misuli ya bega

-Misuli ya bega ni kati ya misuli muhimu sana kufanya katika mazoezi ukizingatia kwamba mazoezi mengi sana yanategemea uimara wa misuli hii katika kufanya mazoezi. 

-Bega ni moja ya maungio katika mwili wa binadamu lenye uwezo wa kuzunguka katika uelekeo mbalimbali likiwa limezungukwa na misuli mbalimbali yani "deltoids" na "rotator cuffs"

-Msuli wa deltoid ambao upo sehemu ya juu ya bega midhiri ya mfuniko umegawanyika sehemu kuu tatu yani; sehemu ya mbele, sehemu ya kati na sehemu ya nyuma. Katika mzoezi sehemu hizi ni muhimu kufanyiwa mazoezi.

-Misuli ya bega ambayo husahaulika mara nyingi katika mazoezi ni hiyo inayoitwa "rotator cuffs" ambayo ni muhimu sana kwani husaidia kuimarisha ungio la bega.

-Mfano wa mazoezi ya misuli ya bega ni pamoja na ; overhead press, front rise, lateral rise n.k

4. Misuli ya mikono

-Kati ya misuli inayopendelewa na vijana wengi katika jimu ni misuli ya mikono kwani mtu yuko tayari kuacha mazoezi mengine na kufanya mazoezi ya mkono tu.

-Misuli ya imegawanyika katika sehemu kuu tatu yani: 

  • Misuli ya mbele ya mkono wa juu iitwayo Biceps (Bai kama ilivyozoeleka na watu wengi)- Hii ina sehemu (vichwa) kuu mbili
  • Misuli ya nyuma ya mkono wa juu iitwayo Triceps (Trai kama iliyozoeleka na watu wengi)- Hii ina sehemu (vichwa) kuu tatu
  • Misuli ya kwenye kiwiko (Foream)- Ikizoeleka kama misuli ya kuvalia saa😅
-Msuli wa Biceps na Triceps hufanya kazi kwa kutofautiana ambapo biceps husaidia kukunja mkono huku triceps husaidia kukunjua mkono. Hivyo ni muhimu kufanya mazoezi ya misuli yote ili kuleta uwiano mzuri wa misuli hii. 

-Misuli ya kwenye kiwiko (foreams) husahaulika sana na watu wengi kama sehemu ya misuli ya mkono yenye kazi ya kuimarisha mikono hata katika kushika kitu kwa nguvu pamoja na kiganja cha mkono kuzunguka katika uelekeo tofauti tofauti.

-Mfano wa mazoezi ya misuli ya mikono ni; Biceps curl, triceps extension n.k

5. Misuli ya tumbo

-Misuli mbalimbali imejenga sehemu ya tumbo na hivyo kama sehemu nyingine za mwili ni muhimu kufanya mazoezi ya misuli hii. 

-Moja ya misuli ya tumbo (rectus abdominis) ikifanyishwa mazoezi vizuri  hupelekea pingili pingili katika idadi tofauti tofauti kulinga na mazoezi huku 6-packs ikiwa ni muonekano unaofahamika zaidi.

-Uimara wa misuli hii husaidia kuboresha uwiano mzuri wa mwili na kuufanya mwili kwa ujumla kuwa imara wakati wowote.

-Ikumbukwe tu sehemu ya tumbo hubeba mafuta mengi chini ya ngozi na hali hii huu hupelekea watu wengi wanene kuona ugumu wa mazoezi ya tumbo. Lakini pia ni moja ya misuli ambayo 

-Mfano wa mazoezi misuli ya tumbo ni pamoja na; cruches, sit-ups, planks

6. Misuli ya makalio na miguu.

-Makalio na miguu ndio sehemu katika mwili ambazo zina misuli mikubwa katika mwili kuliko sehemu nyingine ya mwili .

-Misuli hii hufanya kazi kubwa sana katika mwili ikiwa ni pamoja na; kutembea, kuamka kutoka katika kiti, kuchuchumaa chooni, kukimbia, kupanda kwenye chombo cha usafiri.

-HIivyo misuli hii inabidi ipewe uzito mkubwa katika programu ya mazoezi ingawa kwa uhalisi ndio misuli ambayo watu wengi wamekuwa wakiogopa mazoezi yake, kama ni ratiba ya jimu basi siku ya mazoezi ya miguu huwezi kuona watu😆

-Pamoja na faida zote hizo kuna baadhi ya wafanya mazoezi hasa wa kiume wamekuwa na fikra potofu ya kufanya mazoezi ya misuli ya makalio wakidhani ni kwa ajili ya wanawake tu, si kweli.

-Katika mazoezi ya misuli hii ni muhimu kuanza na msuli mkubwa (msuli wa makalio-glutes) kisha na kumaliza na msuli mdogo (misuli ya kwenye miguu).

-Mfano wa mazoezi ya misuli ya makalio na miguu ni; squats, lunges, leg extensions n.k

7. Misuli ya eneo la kati la mwili wote (core)

-Misuli hii ya "core" huchanganywa haswa na misuli ya tumbo kitu ambacho si kweli. Misuli ya "core" ni mingi sana na husaidia zaidi katika kuimarisha mwili na kuupa msawazo mzuri. 

-Misuli ya eneo hili la kati la mwili (core) kuanza kutazamiwa kuanzia kwenye ngazi ya mabega kushuka chini hadi kwenye nyonga.  Hivyo ni muhimu kufanya mazoezi ya moja kwa moja kuimarisha eneo hili kwa ujumla wake.

-Mazoezi mbalimbali ya "core" ni pamoja na; planks, reverse planks, slide n.k

Kufahamu misuli hii haitoshi bali unatakiwa kujua zaidi pia mazoezi mbalimbali ya msingi kwa kila kundi la misuli, namna sahihi ya kufanya, mambo gani ya kuepuka na hata mpangilio mzuri wa mazoezi yako kulingana na misuli hii ya mwilini. Kwa kufanya hivi utafanikiwa kwa kiasi kikubwa katika mazoezi yako, kanuni na taratibu za mazoezi muhimu kuzingatia🙏

 





Share:

Maoni 1 :

  1. One of the very nice sources of health tips.Congratulations kijana

    JibuFuta

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.