MLO UPI WA CHAKULA UMEKUWA UKIUTUMIA MARA KWA MARA KATI YA AINA HIZI NNE (4) ZA MILO YA CHAKULA?

 Kumekuwa na uandaji wa aina mbalimbali za milo ya chakula hasa kulingana na malengo fulani kama vile kupunguza uzito, kuongeza uzito, kupambana na magonjwa fulani n.k. Kwa ujumla mlo bora hutusaidia kuwa na afya bora na hivyo kuepukana na magonjwa. Shirika la Afya Duniani (WHO) linasisitiza ulaji bora ambao unadhibiti matumizi ya mafuta mengi na yasiyo salama mwilini,  sukari nyingi (ya kuongeza) pamoja na chumvi nyingi lakini kuongeza ulaji wa matunda, mboga za majani, mboga za mimea jamii ya kunde, karanga na nafaka zisizokobolewa. Kutokana na kuzingatia ulaji bora wa chakula, zifuatazo ni aina nne (4) ambazo zimeandaliwa ili kupata matokeo mazuri kiafya

1. Mlo wenye mafuta kidogo

-Mlo huu ni mzuri sana kwa watu wenye kutaka kupunguza uzito au kudumisha uzito wa kawaida walionao.

-Vyakula vyenye mafuta huchangia sana kwa lishe-nguvu mwilini na hivyo kupelekea kukusanyika kwa mafuta.Hali hii hupelekea ongezeka la uzito na kuongeza uhatari wa magonjwa ya moyo, kisukari na presha.

-Njia bora ya kufanikiwa katika mlo huu ni pamoja na kupata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa lishe kuweza kuandaa menyu (ratiba) maalamu kwa mlo huu kulingana na mwili.

-Kama chakula chako unaweza kukipima kwa usahihi basi ili kufanikisha mlo huu unatakiwa kutumia mafuta asilimia 30 au pungufu ya nishati katika chakula chote ambapo mafuta huwa na nguvu ya kilocalori 9.4 kwa kila gramu 1 (9.4Kcal/g).

2. Mlo wa vyakula vya mimea.

-Maana halisi ya mlo huu ni kuhusisha ulaji wa nafaka, matunda, mboga mboga, mboga jamii ya kunde na karanga wakati vyakula kutoka katika vyanzo wa wanyama huondolewa.

-Ulaji wa mlo huu huonekana na matokeo chanya katika kupunguza magonjwa ya moyo, shinikizo la juu la damu, kisukari, unene na pamoja na baadhi ya saratani.

-Kutokana na maana halisi ya aina ya mlo huu, kuna uwezekana wa kupata upungufu wa madini ya Calcium pamoja na vitamini B12 endapo hatatumia kabisa vyakula katika vyanzo vya mimea. Hivyo ni muhimu kuwa na kiasi kidogo cha vyakula hivi au kutumia virutubisho mbadala vya vitamini


3. Mlo wa DASH. 

-Je, unasumbuliwa na shinikizo la juu la damu? Basi huu ndio mlo wako sahihi kabisa kwani ni bora kabisa kwa afya lakini pia husaidia kudhibiti shinikizo la juu la damu, hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya utumbo mpana, maradhi ya moyo, gauti n.k

-DASH (Dietary Approches to Stop Hypertension) ni mlo ulioandaliwa ukihusisha 

  • Ulaji wa matunda mara 4 hadi 5 katika siku
  • Ulaji wa mboga za majani mara 4 hadi 5 katika siku
  • Utumiaji wa maziwa au zao la maziwa mara 2 hadi 3 kwa siku pamoja na
  • Utumiaji wa mafuta asilimia 25 au pungufu
-Matumizi ya mlo huu yamekuwa ya msaada mkubwa sana kwa wagonjwa wenye tatizo la shinikizo la juu la damu (presha) kwani tafiti zimeonyesha mafanikio makubwa ya mlo huu kwa kupunguza na kudhibiti presha.

4. Mlo wa Kimediterrania

-Mlo huu wa Kimediterrania unahusisha zaidi utumiaji wa vyakula vifuatavyo;

  • Matunda kwa wingi
  • Mboga za majani kwa sana
  • Nafaka zisizokobolewa
  • Maharagwe na mafuta ya mbegu kama vile olive na alizeti
  • Utumiaji kidogo au wastani wa mvinyo
-Vyakula vingine vinavyohusishwa katika mlo huu ni kiwango kidogo vya samaki, nyama nyeupe, mazima  na nyama nyekundu kwa kiwango kidogo mno.

-Aina hii ya mlo imechangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa saratani mbalimbali kama utumbo mpana, tezi dume n.k lakini pia umepunguza maradhi ya mfumo ya fahamu kama vile Parkinson ambao huwapata sana wazee na kuwafanya wana kuwa na mitetemo ya mwili.

Hii ni baadhi ya aina ya milo ambayo unaweza ukaandaa nyumba ili kuweza kujenga afya bora.Ni muhimu sana kuweza kuwasiliana na mtaalam wa lishe ili kuweza kupata mpangilio sahihi wa vyakula vyako katika mlo kulingana na wewe binafsi kutokana kuwa na utofauti wa mtu na mtu.






  

Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.