Kila mara wanasayansi wanazidi wanaleta matokeo mapya ya tafiti yakionesha faida za kiafya za ulaji wa matunda kila siku katika mwili hasa katika kupunguza kuibuka kwa magonjwa sugu kama vile kisukari, saratani, maradhi ya moyo, kiharusi, shinikizo la juu la damu n.k. Kiwango cha ulaji wa matunda na mboga za majani kwa siku hutofauti mtu na mtu kulingana na umri, jinsi, kiwango cha shughuli katika siku pamoja na afya ya mtu kwa ujumla.
Pamoja na yote hayo, namna nyingine ambayo imeonekana ni nzuri katika ulaji wa matunda na mboga za majani ni kuchanganya rangi tofauti tofauti za vyakula hivi ili kuweza kupata matokeo makubwa zaidi kiafya kutokana na ukweli kwamba rangi hizi zimebeba uzito mkubwa kwenye afya ya binadamu. Hii inaweza kuonekana kama ifuatavyo;
1. Mboga za majani na matunda yenye rangi NYEKUNDU.
-Wekundu wa vyakula hivi umeundwa kutokana na pigmenti (kemikali) zinazoitwa "lycopene" na "anthrocyanins"
-Pigmenti hizi husaidia katika kuulinda mwili dhidi ya maradhi ya saratani (lycopene) pamoja na kuimarisha afya ya moyo(anthrocyanins)
-Mfano wa mboga za majani na matunda mekundu ni pamoja na;
- Tikiti maji
- Nyanya
- Apple nyekundu
- Mapera mekundu
- Zabibu
- Komamanga
- Hoho na pilipili nyekundu n.k
2. Mboga za majani na matunda yenye rangi ya ZAMBARAU
-Pigment (kemikali-anthrocyanins) katika rangi za matunda haya husaidia sana kulinda seli za mwili na hivyo husaidia kupunguza uhatarishi wa maradhi ya saratani, kiharusi na maradhi ya moyo
-Mfano wa matunda na mboga hizi ni pamoja na;
- Biringanya
- Matunda ya pesheni
- Beetroots
- Plums
- Kabeji
- Beri n.k
-Rangi ya kijana katika matunda na mboga hujengwa na pigmenti iitwayo "chlorophyll" na baadhi ya matunda na mboga huwa na kemikali iitwayo "Lutein". Kemikali hizi kwa ujumla husaidia kuulinda mwili dhidi ya matatizo ya macho
-Pia kemikali "indole" iliyopo katika baadhi ya mboga za majani kama vile; broccoli, cauliflower na kabeji husaidia katika kulinda miili dhidi ya saratani mbalimbali.
-Pia vyakula hivi ni vyanzo vizuri vya Vitamin Foliki asidi ambayo husaidia kuzuia kasoro za kimaumbile kwa mtoto aliye tumboni kwa mama mjamzito (kama vile mgongo wazi)
-Mfano wa kundi hili ni;
- Matango
- Spinachi
- Chainizi
- Sukumawiki
- Parachichi n.k
- Kuimarisha uwezo wa kuona na kuzia magonjwa ya macho; kutokana na vitamini A katika vyakula hivi
- Kupunguza uwezekano wa kupatwa na maradhi ya moyo na saratani.
- Kuimarisha kinga ya mwili
- Kuboresha afya ya ngozi na kuta mbalimbali katika viungo vyenye uwazi mwili (mishipa ya damu, mfumo wa chakula n.k)
- Kuzuia kasoro za kuzaliwa za mtoto tumboni kwa mama mjamzito.
- kupunguza lehemu (cholesterol) mwilini
- Kudhibiti shinikizo la damu
- Kupunguza nafasi ya kupatwa na saratani ya tumbo pamoja na maradhi ya moyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni