• This is default featured slide 1 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 2 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 3 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 4 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 5 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

ATHARI KUMI (10) ZA KIAFYA ZA UVUTAJI WA SIGARA KWA MWANAMKE KABLA, WAKATI NA BAADA YA UJAUZITO.

 Uvutaji wa sigara ni moja ya mambo hatarishi ambayo huweza kuathiri moja kwa moja mfumo wa uzazi wa mwanamke kuanzia katika kushika mimba, wakati wa mimba yenyewe na hata baada ya mimba. Moshi wa sigara umekuwa ukivutwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kama sigara za kuwasha na moto, sigara za umeme, sisha n.k. Moshi wa sigara umekuwa ukiwaathiri hadi watu wa pembeni ambao hawavuti moja kwa moja, na hii pia imechangia kwa madhara ya kiafya kwa watu hawa. Takribani wanawake milioni 250 huvuta sigara duniani huku asilimia 22 ikiwa ni wanawake katika nchi zilizoendelea na aslimia 9 ni wanawake kutoka nchi zinazoendelea. 

Zifuatazo ni athari mbalimbali za kiafya katika mfumo wa uzazi wa mwanamke zitokanazo na uvutaji wa sigara 

1. Kutoshika mimba kirahisi (Ugumba)

-Kemikali mbalimbali zinazopatikana katika moshi wa sigara zimeonekana kuwa hatari katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kupelekea kupunguza utengenezaji wa mayai ya kike na pia hupelekea utengenezaji wa mayai ambayo hayajakomaa.

- Hali hii imechangia kwa wanawake wengi kushindwa kushika ujauzito kama awali kabla hawajaanza uvutaji wa sigara.

2. Kuharibika kwa mimba.

-Uvutaji wa sigara umeonekana kuwa na mchango katika kuharibika (kutoka) kwa mimba hasa kabla ya kufikisha wiki 28 (kwa Tanzania). Hii pia imeonekana kuwaathiri hata kwa wale wanawake ambao huvuta moshi kutoka pembeni.

-Kemikali sumu katika sigara zimekuwa na madhara makubwa katika mfumo mzima wa kondo (placenta) ambao huweza kupelekea mimba kuharibika

3. Kusababisha kifo cha mtoto akiwa tumbo au baada ya kuzaliwa.

-Sumu mbalimbali katika sigara kupelekea kuathiri ukuaji wa mtoto tumboni na hivyo kusababisha kifo cha mtoto angali tumboni au mara baada ya kuzaliwa. 

-Tafiti zimeonesha kuwa uvutaji wa sigara huchangia kwa asilimia 50 ya watoto kufia tumboni huku asilimia 20 ikichangia watoto wengi kufa ndani ya siku 28 baada ya kuzaliwa.

4. Kupasuka kwa chupa la uzazi kabla ya mimba kutimia muda wake.

-Tafiti zimebaini kuwa uvutaji wa sigara huweza kuchangia kwa kiasi kikubwa chupa au mfuko wa uzazi kabla ya wiki 37 (sawa na miezi 9) ambapo mtoto anakuwa bado hajakomaa ipasavyo.

-Athari hii huenda sambamba na kadiri idadi ya sigara inayovutwa kwa siku inavyoongezeka huku ikibainika kuwa utumiaji wa sigara kuanzia 10 na kuendelea kwa siku huwa na athari kubwa katika suala hili.

5. Kujifungua watoto wenye uzito mdogo (Njiti)

-Kemikali sumu husababisha athari katika ukuaji wa mtoto pindi anapokuwa bado yuko tumboni na hivyo hupelekea kujifungua mtoto ambaye uzito wake ni mdogo (chini ya kilo 2.5) ukilinganisha na umri wake.

-Mwanamke anayevuta sigara moja kwa moja na yule ambaye huvuta moshi wa mtu wa pembeni wote huwa katika uhatari wa kuzaa watoto wa aina hii.

6. Hitilafu ya kondo wakati wa ujauzito.

-Matatizo ya kuvuja damu katika uke kipindi cha ujauzito baada ya wiki 20 ya mimba hutokea kutokana na hitilafu tofauti tofauti za kondo la mimba ambapo hitilafu hii imeonekana kuchangiwa na matumizi ya sigara.

-Hitilafu hizi za kondo zipo za aina tofauti tofauti ambapo zingine ambapo;

  • Kondo linawezaka kutokuwa eneo lake sahihi (eneo la siku zote kwenye mimba ya kawaida)-Pracenta previa
  • Kondo linaweza kung'atuka katika eneo lake-Placental abruption, na zingine ambazo ni aghalabu

-Hitilafu hii inapotokea ikihusisha upotezaji mkubwa wa damu basi huweza kupelekea mimba kuharibika hivyo kupoteza mtoto tumboni.


7. Kujifungua kabla ya wiki 37 (miezi 9)

-Tafiti zimeonesha kuwa uvutaji wa sigara umechangia kwa wanawake wengi kujingua kabla ya muda wa mimba kutimia hukuwa uwezekano wa kujifungua ukionekana hasa kabla ya wiki 32 ya ujauzito. 

-Tatizo hili huchangia kwa kuzaa watoto ambao hawajakomaa vizuri baadhi ya viungo, wenye uzito mdogo n.k hivyo kuwaweka katika mazingira ya kupata maradhi kirahisi.

-Ikumbukwe tu kujifungua kabla ya wiki 37 inaweza ikasababishwa na mambo mengine mengi tu.    

8. Kujifungua mtoto wenye kasoro mbalimbali.

-Uvutaji wa sigara huweza kuchangia kwa kasoro mbalimbali za mtoto atakayezaliwa huku kazi ya vinasaba ikihusishwa katika kutokea kwa kasoro hizo.

-Kasoro kama midomo ya sungura, mkundu kutojengeka, uwazi wa ukuta wa tumbo, vidole vya ziada, hitilafu katika moyo n.k

-Utokeaji wa kasoro umeonekana kwenda sambamba na kadiri unavyowahi kuvuta sigara yani uvutaji wa sigara katika miezi mitatu ya mwanzo huongeza uwezekano wa kupata kasoro katika viungo vya mtoto.

9. Huchangia kwa Kisukari cha ujauzito.
-Pamoja na vihatarishi vingine, uvutaji wa sigara huchangia katika kuibuka kwa maradhi ya kisukari wakati wa ujauzito ukilinganisha na wanawake ambao hawatumii sigara.
10. Kutopata maziwa ya kutosha.
-Kiwango cha maziwa ya mama baada ya kujifungua hupungua sana kutoka na uvutaji wa sigara kipindi cha ujauzito na hii hupelekea unyonyeshaji hafifu wa mtoto na ndani ya muda mfupi.

Mwanamke ambaye anatarajia kupata ujauzto na mama mjamzito hatakiwi kutumia sigara kabisa na anatakiwa kujiepusha na moshi wa sigara kutoka kwa wavutaji wa pembeni hasa wazazi wenza. Hii itasaidia sana kuepuka madhara mbalimbali zaidi ya yaliyotajwa hapo juu. Na kama mwanamke ameshaanza uvutaji basi sasa hivi ni muda sahihi wa kuacha kwa kuoana na daktari atakaye kusaidia.

Share:

NAMNA MGONJWA WA KISUKARI ANAVYOWEZA KUJIPIMA KIWANGO CHA SUKARI YAKE KATIKA DAMU AKIWA NYUMBANI

 Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa sugu ambao unahitaji ufuatiliaji wa mara kwa mara kuanzia kwenye mtindo wa maisha hadi kwenye matibabu yake. Moja ya sehemu muhimu ambayo mgonjwa hutakiwa kuhusika moja kwa moja ni katika suala la upimaji wa kiwango chake cha sukari anapokuwa nyumbani ili kuhakikisha kiwango chake cha sukari katika damu kinakuwa sawa (kawaida). Tafiti zinaonesha wazi kuwa kadiri udhibiti wa kiwango cha sukari katika damu unapokuwa dhabiti uwezekano wa kupata madhara ya ugonjwa wa kisukari hupungua zaidi.

Vifaa mbalimbali vimekuwa vikitumika katika kuhakikisha upimaji wa sukari katika damu unafanyika kwa ufasaha, hivi ni pamoja na; mashine za kupima sukari ya papo kwa papo (Glucometers) na mashine za kupima sukari endelevu katika damu (Continous Glucose Monitors).

Mashine za kupima sukari papo kwa papo (Glucometers).

-Mashine hizi hutengenezwa na kampuni mbalimbali na hakuna mashine inayosemekena kuwa bora zaidi ya mwingine.

-Mashine hizi huwa na stripu (strips) zake ambazo huendana na mashine husika, stripu hufanya kazi ya kupokea sampuli ya damu na kisha kuwekwa kwenye mashine kwa ajili ya kutoa majibu.

-Mashine hizi hutegemea sampuli ya damu ambayo kuchukuliwa hasa maeneo ya vidoleni.

Mashine za kupima sukari endelevu katika damu (Continous Glucose Monitors)

-Hizi ni mashine ambazo hutumika kufuatilia kiwango cha sukari katika damu muda wote kwa kutumia sensa maalumu na husoma majibu kila baada ya dakika 5 mpaka 15 ndani ya masaa 24.

-Mashine hizi ni nzuri kutumika kwa wagonjwa hasa wa ambao wako kwenye dawa za sindano ya Insulini kama wale wa kisukari aina ya kwanza kwani wanakuwa kwenye hatari ya kushuka kwa kiwango cha sukari mwilini. 

-Lakini pia mashine za kupima sukari ya papo kwa papo zinaruhusiwa kwa wagonjwa hawa wanaotumia sindano ya Insulini.

HATUA ZA UPIMAJI WA KIWANGO CHA SUKARI KATIKA DAMU KWA KUTUMIA MASHINE ZA PAPO KWA PAPO

Hizi ni hatua za jumla katika suala zima la upimaji ukizingatia mashine nyingi huja na maelekezo tofauti tofauti katika utumiaji, hivyo ni muhimu sana kusoma maelekezo ya mashine husika

1. Safisha mikono yako kwa maji safi. 

-Maji ya uvugu vugu na sabuni hushauriwa zaidi na kisha kausha mikono kwa kitamba safi.

2. Andaa sindano maalumu kwa kuchoma kwenye kidole.

-Sindano hizi hupatikana katika vituo vya afya na kwenye maduka ya madawa, kazi kubwa ni kuchoma kwenye ngozi kwa ajili ya kuchukua sampuli kidogo ya damu.

-Epuka kutumia sindano iliyokwisha kutumika na pia epuka kuchangia sindano.

3.Andaa mashine ya sukari pamoja na stripu zake.

-Hapa maelekezo ya uandaaji yanaweza kutofautiana kulingana na aina ya mashine, hivyo muhimu kusoma maelekzo.

4. Choma kwenye ncha ya kidole kwa kutumia sindano maalumu

-Sehemu ambayo hutumika zaidi ni kwenye ncha za vidole vya mikono kwani ndio maeneo yameyoonekana kutoa majibu ya uhakika zaidi ukilinganisha na sehemu zingine.

5. Weka tone la damu katika stripu ya mashine.

-Baada ya sekunde kadhaa tu, majibu yataonekana katika mashine katika kizio cha mmo/L au mg/L kulingana na mashine.

6. Tupa sindano iliyotumika katika chombo maalum cha vitu vya ncha kali.

-Usitupe sindano hizi kwenye sehemu za taka za nyumbani kwani sindano hizi huweza kusababisha maambukizi kutokea.

Suala la muhimu kukumbuka katika upimaji wa sukari ukiwa nyumbani ni kuwa maambo mbalimbali yanaweza kuchangia kupata majibu yasiyo sahihi kutoka katika mashine yako ikiwemo; kutumia stripu zilizoisha muda wake wa matumizi,  utunzaji mbovu wa stripu, eneo la kuchoma sindano kuwa chafu n.k. Hivyo unashauri kuweza kuonana na mtaalamu wa afya pale unapoona unapata matokeo ambayo hayaendani na hali ya mgonjwa ili kuweza kujadiliana, kuoana shida iko wapi na kutatua tatizo.

Share:

HATUA TANO (5) MUHIMU ZA KUZINGATIA ILI KUPIMA KWA USAHIHI SHINIKIZO LA DAMU (PRESHA) UKIWA NYUMBANI

 -Shinikizo la damu ni mgandamizo wa damu katika kuta za mishipa ya damu iitwayo arteri ambayo safirisha damu  kutoka katika moyo na kupelekea sehemu zingine za mwili.  Mgandamizo huu katika kuta za mishipa ya damu hupimwa kwa kifaa maalumu kiitwa sphygmomanomita AU mashine ya kidijitali (BP mchine) huku kwa wastani shinikizo la damu la kawaida likiwa ni milimita za Mekyuri 120/80. 

-Namba ya juu (120) ni presha katika mishipa ya damu wakati chemba za moyo zinasukuma damu (Kusinyaa) huku 80 ni presha wakati chemba za moyo zinapokea damu (Kutanuka).

-Kwa matumizi ya nyumba ni vyema kutumia mashine ya kidijitali katika kujipima kuliko kutumia sphygmomanomita kutoka na ukweli kuwa sphygmomanomita huhitaji utaalamu zaidi wa mtu ili kupima kwa usahihi ukilinganisha na mashine ya kidijitali.

-Mashine za kidijitali ni nyingi sana siku hizi kutoka katika kampuni tofauti tofauti huku zikija na maelekezo ya namna ya kutumia  katika maboxi yake. Mashine hizi huwa na "cuff" (sehemu katika mashine ambayo huzungushwa katika mkono wako wa juu, cuff za mashine zingine huja kwa ajili ya kuzungushwa kwenye viwiko au miguu) na pia huwa na sehemu ya kusomea majibu.

-Ni muhimu kujipima shinikizo la damu nyumbani kwasababu zifuatazo kuu;

  • Kujua ni kwa kiasi gani shinikizo la damu linakuwa kwa kupima nyumba ukilinganisha na hospitali. Na hii hutokana na ukweli kuwa kuna watu wengi presha huwa juu wakiwa hospitali na huwa kawaida wakiwa nyumbani
  • Kujua kwa kiasi gani dawa za presha zinafanya kazi
  • Kujua mabadiliko yoyote ya presha yanapotokea muda wowote
Zifuatazo ni hatua za kuzingatia wakati wa kupima kwa usahihi shinikizo la damu kwa kutumia mashine ya kidijitali

1. Fanya maandalizi sahihi

-Kabla kabisa ya kuanza upimaji ni muhimu kukumbuka kuwa unatakiwa kuepuka kutumia kinywaji chenye kafeini kama kahawa, mazoezi na uvutaji wa sigara nusu saa kabla ya kuanza upimaji

-Pia unataki uwe umeshakojoa na kuondoka nguo zote zinazoziba eneo la mkono ambalo utapima presha yako

-Vyote hivi huwa ni muhimu kuvitekeleza kwani huathiri usahihi wa matokeo ya presha yako baada ya kupima

2. Kaa kwa usahihi

-Ni muhimu sana kuzingatia suala la ukaaji, na hapa ukaaji unaotakiwa ni;

  •  kuhakikisha miguu yote imekanyaga chini na haijapishana, 
  • mgongo unapata sapoti kwa nyumba na 
  • mkono ambao utatumika kupima presha uko katika usawa wa moyo.

-Kukaa kwa usahihi huenda sambamba na kukaa kimya kabisa pasipo kuongea chochote na kujitahidi ukimya wa mazingira yanayokuzungua pia.

-Yote haya yasipozingatia yameonekana pia kuathiri majibu ya kipimo.

3. Funga "cuff" (mkanda katika mashine yako) katika mkono wako.

-Funga mkanda huu wa mashine eneo la kati la mkono moja kwa moja pasipokuwa na nguo  yoyote kwa juu.

-Hakikisha makanda wa mashine haulegei kiasi cha kutoka eneo lake na wala haubani sana kiasi cha kutojisikia vizuri.

-Baada ya kuweka kila kitu sana, inashauriwa kutulia kwa muda wa dakika 3 mpaka 5 huku mkanda ukiwa umefungwa kwenye mkono

4. Pima presha yako sasa

-Mashine nyingi za kidijitali zinahusisha kubonyeza tufe kwenye sehemu ya mashine kwa ajili ya kuwasha na  kisha kupima yenyewe. 

-Wakati mashine inapima utahisi hali ya kujaa kwa hewa kwenye ule mkanda uliozungushwa katika mkono  pamoja na hali ya kama mkono unafinywa na mashine inapomaliza utahisi hali ya kusinyaa kwa mkanda

-Ni muhimu kusoma maelekezo ya mashine baada ya kuinunua kwani mashine nyingi huja na maelekezo  ya namna ya kutumia 

5. Rekodi majibu yako katika daftari maalum.

-Baada ya mashine kumaliza kupima utaona namba zinatokea kwenye sehemu ya mashine huku baadhi ya mashine husoma majibu kwa kutoa sauti.

-Majibu huja na namba mbili yani; namba ya juu na ya chini kama iliyoelezwa hapo juu

-Andika majibu yako katika daftari maalumu ili kuweza kumuonesha daktari wako utakapoenda kuonana nae 

-Tafsiri ya ujumla ya majibu ya shinikizo la damu ni;

  • Shinikizo la juu la damu ni pale mashine inasoma milimita za Mekyuri 140/90 au zaidi
  • Shiniko la chini la damu ni pale mashine inasoma chini ya milimita za Mekyuri 90/60
  • Shinikizo la damu la kawaida huwa kati ya milimita za Mekyuri  90/60 mpaka 139/89

Kwa kawaida mtu ana shauri kupima presha yake mara mbili katika siku yani asubuhi na jioni kwa muda wa siku tatu mpaka saba mfululizo kwa ajili ya kufanya tathmini na daktari. Idadi ya upimaji huu inaweza kubadilika kutoka na mwenendo wa presha yako chini ya tathmini ya daktari. Ni muda sahihi wa kupata hapa mashine ya kupima presha ili kuweza kujua maendeleo ya presha yako




Share:

FAHAMU NAMNA TATU (3) AMBAVYO UGONJWA WA SIKO SELI (SELIMUNDU) UNAVYOWEZA KURITHIWA KUTOKA KWA WAZAZI

 Siko seli ni ugonjwa wa urithi wa vinasaba (DNA) vya protini ya hemoglobini (Hb) yenye hitilafu iliyoko katika chembe nyekundu za damu kutoka kwa wazazi wawili.  Protini hii hufanya kazi ya kubeba na kusafirisha hewa ya oksijeni kutoka katika mapafu kwenda sehemu mbalimbali za mwili ili kutumika katika kutengeneza nguvu mwilini. 

Kwa kawaida protini hii inapokuwa haina hitilafu basi hufanya chembe nyekundu kuwa na umbo la duara na endapo protini hii inapokuwa na hitilafu katika ugonjwa wa siko seli basi chembe nyekundu hizi huwa na umbo la nusu mwezi au kifaa kiitwacho mundu au kama ndizi

Katika suala la urithi wa vinasaba kutoka kwa wazazi, mtoto hupokea kinasaba kimoja cha kutengeneza protini ya hemoglobini kutoka baba na kimoja kutoka kwa mama na hivyo kujenga pea (pair) ya vinasaba vya protini hii.

Zifuatazo ni alama ambazo hutumika katika kuelezea urithi wa vinasaba katika ugonjwa wa siko seli 

  • HbA- Hii ni alama inayowakilisha protini ya hemoglobini ya kawaida 
  • HbS- Hii ni alama inayowakilisha protini ya hemoglobini iliyo na hitilafu (yenye dosari)

Muhimu: Ili kupata mtoto wenye ugonjwa wa siko seli ni lazima wazazi wote wawili wawe wamebeba vinasaba vya ugonjwa wa siko seli yani (HbS)
Hizi ndio namna ambazo mtu anaweza kupata ugonjwa wa siko seli kutoka kwa wazazi

1. Endapo baba atakuwa ana vinasaba vya HbAS na mama atakuwa na vinasaba vya HbAS
-Baba mwenye HbAS tafsiri yake ni kuwa amebeba vinasaba vya ugonjwa wa siko seli ila si mgonjwa vilevile mama mwenye HbAS amebeba vinasababa vya ugonjwa wa siko seli ila si mgonjwa.
-Ili kupata mtoto mwenye ugonjwa wa siko seli basi baba atakuwa amehusika wa kutoa HbS moja na mama atahusika kutoa HbS moja na hivyo kumrithisha mtoto HbSS
- Wazazi hawa wana uwezekano wa kupata mtoto mwenye ugonjwa wa siko seli kwa asilimia 25 miongoni mwa watoto wanne watakao zaa.
Urithi wa siko seli kutoka kwenye wazazi waliobeba vinasaba vya ugonjwa
Tafsiri ya watoto waliopatikana ni kama ifuatavyo
i/ AA-Huyu ni mtoto ambaye mwenye protini za hemoglobini za kawaida kabisa (Kwanza kushoto)
ii/ AS- Hawa ni watoto ambao wamebeba vinasaba vya ugonjwa wa siko seli lakini si wagonjwa (Wawili katikati). 
iii/ SS- Huyu ni mtoto ambaye ni mgonjwa wa siko seli (Mwisho kulia)

2. Endapo mzazi mmoja ana vinasaba vya HbAS na mzazi mwingine ana vinasaba vya HbSS.
-Inapotokea mzazi mmoja amebeba vinasaba vya ugonjwa yani ni HbAS na mzazi mwingine ni mgonjwa tayari yani HbSS basi nafasi ya kupata mtoto mwenye ugonjwa wa siko seli ni asilimia 50 miongoni mwa  watoto wanne watakaozaa.
-Watoto  wawili wenye SS wakiwa na ugonjwa wa siko seli huku watoto wawili wenye AS wakiwa wamebeba vinasaba vya ugonjwa.

3. Endapo wazazi wote wana ugonjwa wa siko seli 

-Ikitokea wazazi wote wana ugonjwa wa siko seli yani baba ana HbSS na mama ana HbSS basi ni lazima watoto wote watakuwa na ugonjwa ugonjwa wa siko seli kwa nafasi ya asilimia 100.

Wazazi wa katikati (nyekundu) wenye ugonjwa siko seli wanazaa watoto wote wenye ugonjwa wa siko seli pia (wanne wenye nyekundu zote)

Ni muhimu sana kuna kutambua hali yako ya umiliki wa vinasaba vya ugonjwa wa siko seli ikoje ili kuweza kupata ushauri bora kutoka kwa daktari. Hii husaidia katika kufanya maamuzi sahihi hata katika kupata mwenza anayekufaa lakini zaidi husaidia katika kupunguza kasi ya urithishaji wa vinasaba vya ugonjwa huu ambavyo hupelekea katika ongezeko la wagonjwa wengi wenye siko seli. Endapo kuna historia ya ugonjwa wa selimundu katika familia au ukoo basi ni muda sahihi wa kufika katika hospitali ili kupata vipimo vya uchunguzi.
Share:

HAUNA SABABU YA KUKOSA FAIDA TISA (9) MUHIMU ZA KIAFYA ZITOKANAZO NA ULAJI WA MBOGA ZA MAJANI NA MATUNDA KILA SIKU

Mboga za majani na matunda ni sehemu muhimu sana kwenye milo yetu ya kila siku kutokana na faida nyingi za kiafya zinazopatikana na hii hutokana na upatikanaji wa virutubisho mbalimbali katika vyakula hivi kama vile  vitamini, madini, makapi-mlo n.k. Kulingana na tafiti iliyofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) imeonekana kuwa watu wengi hatutumii mboga za majani na matunda kwa kiwango kinachotakiwa na hivyo kusababisha vifo takribani milioni 3.9 duniani. Inakadiriwa kuwa 14% ya vifo hutokana na saratani za mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, 11% hutokana na maradhi ya mishipa ya moyo na 9% hupelekea vifo kutokana na kiharusi. Ili kuweza kuchota faida nyingi za kiafya kutokana na ulaji wa mboga za majani na matunda basi Shirika la Afya Duniani (WHO) linashauri utumiaji wa angalau gramu 400 kila siku (sawa na kula milo mitano yenye sawa na gramu 80 ya mboga za majani na matunda). Manufaa haya ya kiafya yatokanayo na ulaji wa mboga za majani na matunda ni kama ifuatavyo;

1. Husaidia katika ukuaji na maendeleo ya watoto

-Mboga za maji na matunda mbalimbali huwa na virutubisho kama vile vitamini A, vitamini Foliki asidi, madini ya Calcium na ya chuma (Iron), virutubisho vyote hivi husaidia katika kukujenga afya bora ya watoto kwa kuwezesha ukuaji bora.

- Pia huboresha mfumo wa fahamu wa watoto kwa kuwafanya kuwa wenye uwezo mkubwa katika kufikiria, kufanya maamuzi, kujifunza na kujitambua vizuri.


2. Kuboresha afya ya moyo na mishipa ya damu

-Tafiti nyingi sana zimeweza kuonyesha matokeo bora ya mfumo wa moyo na mishipa ya damu kutokana na ulaji wa kutosha wa mboga za majani na matunda ambayo yana virtubisho vya makapi-mlo kwa wingi.

-Kwa ulaji wa vyakula hivi huweza kukuepusha na maradhi ya shinikizo la juu la damu, maradhi ya mishipa ya damu ya moyo, na hata kukuepusha na kupatwa na kiharusi.

3. Hupunguza maradhi ya saratani.

-Zaidi ya tafiti 128 zilizofanya zimeweza kuonyesha kuwa ulaji wa kutosha wa mboga za majani na matunda husaidia katika kupunguza uhatarishi wa kupata na saratani mbalimbali zikiwemo za mapafu, mdomo, umio, tumbo, utumbo mpana, tezi dume, matiti, mlango wa uzazi, kongosho, kibofu cha mkojo na ovari.

-Hii hutakana na kemikali (antoxidants) mbalimbali katika vyakula hivi zenye uwezo wa kupambana na kemikali hatarishi mwilini.

4. Huboresha afya ya akili.

-Tafiti zimeonesha kuwa utumiaji wa mboga za majani na matunda kwa wingi yani milo mitano (5) au zaidi husaidia katika kupunguza maradhi ya akili kama vile sonona na wasiwasi.

5. Hupunguza unene 

-Ulaji wa mboga za majani na matunda kwa wingi husaidi katika kudhibiti unene kutokana na ukweli kuwa uchakataji wa sukari asili katika vyakula hivi mwilini hufanyika taratibu bila ya kuathiri kwa haraka kiwango cha sukari katika damu. 

-Pia mboga za maji na matunda humfanya mtu kupunguza ulaji wa vyakula vingi vya wanga na mafuta

6. Hupunguza uwezekano wa kupata kisukari

-Tafiti za kisayansi zimeonyesha wazi kabisa kuwa ulaji wa mboga mboga za majani pamoja na matunda wa wingi kunachangia kupunguza athari ya kupata ugonjwa wa kisukari na hii inaendana sambamba na faida ya kupunguza unene kwa matumizi ya vyakula hivi

7. Huboresha mfumo wa chakula

-Kutoka na uwepo wa wingi wa makapi-mlo katika vyakula vya mboga za majani na matunda, mfumo wa mmeng'enyo wa chakula umeweza kuboreka na hii imesaidia kuzuia matatizo kama vile gasi katika tumbo na utumbo, kupata choo kigumu, na kuepuka maradhi ya utumbo mpana.

8. Huimarisha kinga ya mwili

-Mboga za majani na matunda hubeba virutubisho na kemikali nyingi zenye umuhimu katika mwili ambazo husaidia kuboresha kinga ya mwili na hivyo mwili kuwa na uwezo wa kupambana dhidi ya magonjwa mbslimbali (magonjwa ya kuambukizwa na yasiyo ya kuambukizwa) 

9. Huongeza miaka ya kuishi.

-Moja ya siri ya kuishi muda mrefu ni pamoja na kuzingatia ulaji wa mboga za majani na matunda ya kutosha na hii imedhibitika katika tafiti zilizofanywa katika nchi za magharibi. 

-Watu waliokuwa wanatumia mboga na matunda kwa wingi walionekana kuishi kwa muda mrefu ukilinganisha na ambao walikuwa hawatumii matunda na mboga za majani za kutosha.

Linapokuja suala la ulaji wa mboga za majani na matunda watu wengi hupata na kigugumizi kutokana na kuona ni gharama kubwa kupata milo mitano ya vyakula hivi kwa siku lakini pia watu wengi wanashindwa kuona dhamani ya vyakula hivi katika afya zao. Ukweli ni kuwa afya imara ni kula mboga za majani na matunda kwa wingi na kinga ni bora kuliko tiba.

Share:

NAMNA KUMI NA NNE (14) AMBAVYO UNYWAJI WA POMBE UNAWEZA KUATHIRI AFYA YAKO .

 Unywaji wa pombe hasa unywaji wa kupitiliza ni hatari kwa afya kwani unywaji huu umekuwa ukihusishwa na madhara mbalimbali ya kiafya.  Unywaji wa pombe huchangia kwa vifo vya watu takribani milioni 3 duniani pia kudhoofisha afya ya watu wengi kwa ujmla. Pombe imekuwa ikiathiri hasa watu katika umri wa miaka 15 mpaka 49 huku wanaume (7.1%) wakiathiriwa zaidi  kuliko wanawake(2.2%).

Kiuhalisia ni kuwa pombe imekuwa moja ya vyanzo vya aidha moja kwa moja au visivyo moja kwa moja vya magonjwa mbalimbali katika mwili wa binadamu takribani zaidi ya magonjwa 30. Zaidi unywaji wa pombe unaweza kupelekea hata madhara kwa watu wengine ambao si wahusika wa kutumia pombe hiyo. Madhara ya kiafya yatokana na unywajiwa kupitiliza wa pombe ni kama ifuatavyo katika makundi yake.

1. Saratani

-Tafiti mbalimbali zimeonesha uwepo wa uhusiano wa unywaji wa kupitliza wa pombe na baadhi ya saratani. 

-Saratani ambazo zimeweza kuripotiwa zikiwa na uhusiano na matumizi ya pombe ni pamoja na saratani ya; Koo, Mdomo, Tumbo,Ini, Utumbo mpana,Matiti, tezi dume, n.k

Saratani ya Ini

2. Ugonjwa wa kisukari

-Unywaji wa pombe kupindukia kumechanga sana kwa ugonjwa wa kisukari ambapo ugonjwa huu unaibuka kwa kiasi miongoni mwa watu

-Tafiti mbalimbali zimeweza kufanyika kwa makundi mbalimbali na kuweza kubaini kuwa watu waliokuwa na unywaji wa pombe kupita kiasi walikuwa na nafasi kubwa ya kupata ugonjwa huu . Hii inaweza pia kuchangiwa na madhara ya pombe kuongeza uzito na mafuta mwili

3. Shinikizo la juu la damu

-Unywaji wa pombe kupitiliza umehusishwa na kuibuka kwa tatizo la shinikizo la juu la damu na kuendelea kuwa moja ya changamoto zinazoathiri udhibiti wake kwa wagonjwa hawa wenye shinikizo la juu la damu

-Kwa mgonjwa mwenye shinikizo la juu la damu ni muhimu kuepuka pombe au kunywa kwa kiwango cha wastani kinachoshauriwa.

4. Shambulio la moyo

- Pombe imeweza kuhusishwa na matukio ya shambulio la moyo ambapo mishipa ya damu ya moyo inashindwa kupata damu ya kutosha na hivyo kufanya moyo kushindwa kufanya kazi. Hii inawezekana inatokana na kupanuka kwa moyo kutoka na shinikizo la juu la damu la muda mrefu.

-Pia kumekuwa na uhusiano wa kiwango cha unywaji pombe na suala la kuathiri  mfumo wa umeme  wa moyo ambapo huweza  kupelekea moyo kushindwa kudunda inavyotakiwa na kusababisha kifo cha ghafla.


5. Kiharusi

-Pombe huwa athari katika shinikizo la damu ambalo huathiri kwa kiasi kikubwa mishipa ya damu sehemu mbalimbali katika mwili ikiwemo mishipa ya kwenye ubongo. 

-Kuathirika kwa mishipa ya damu katika ubongo huweza kuepekea kupata kiharusi.

6. Maradhi ya akili

-Matumizi ya pombe kupitiliza yameweza kuhusishwa na kuibuka kwa magonjwa ya akili huku hali ya utegemezi wa pombe ikiwa inahusishwa sana kama chanzo cha baadhi ya dalili.

-Pombe huweza kupelekea mtu kupata hali ya sonona na wasiwasi ambavyo vyote mwisho wa siku huathiri utendaji wa kazi za kila siku wa muhusika.

-Unywaji wa pombe kupindukia kwa muda mrefu huweza kupelekea magonjwa ya akili ambapo mtu hupatwa na hali ya kuchanganyikiwa, lakini pia pombe imeonekana kusababisha kupatwa na degedege.

7. Kuharibu Ini na Kongosho

-Ini na kongosho ni viungo muhimu sana katika mwili wa binadamu kutokana na kazi kubwa zinazofanywa na viungo hivi. 

-Unywaji wa pombe kupitiliza unaweza kupelekea ini na kongosho kuumia moja kwa moja na kufanya viungo hivi kushindwa kufanya kazi na kuhatarisha maisha ya mtu.

-Baadhi ya matokeo ya muda mrefu ya athari za pombe kwenye ini na kongosho ni kupelekea saratani za viungo hivi lakini ini inaweza kuathirika kwa kunywea (kupungua ujazo) hali ambayo kwa kiingereza inaitwa Cirrhosis. 

8. Mawe kwenye mfuko wa nyongo

-Matumizi ya pombe kupitiliza huchangia kwa ongezeko la wagonjwa wenye mawe katika mfuko wa nyongo hali ambayo hupelekea maumivu ya makali sana upande wa kulia wa juu wa tumbo.

9. Udhaifu wa mifupa

--Tafiti zimeonyesha  unywaji wa pombe kupitiliza humeonekana kuathiri mifupa kwa kuifanya kuwa dhaifu na hivyo kuweza kusababisha uwezekano mkubwa wa kuvunjika mifupa hiyo.

10. Gauti 

-Kunywa pombe kupindukia imeoneka kuchochea kwa ugonjwa wa gauti (baridi yabisi) ambao huathiri maungio mbalimbali ya mwili kwenye miguu na hata mikono kwa kusababisha maumivu makali na kuvimba kwa maungio haya.

-Kama tayari una tatizo hili ni vyema basi kuacha pombe au kupunguza unywaji wa pombe kama inavyoshauriwa.

12. Kuathiri mtoto tumboni kwa mama mjamzito

-Unywaji wa pombe kwa mama mjamzito ni hatari mno kwani athari yake kwa mtoto haiwezeki kurekebishwa.

-Pombe kwa mama mjamzito hupelekea kuathiri ubongo wa mtoto na hata kusababisha kutojengeka vizuri kwa viungo vya kichwa. 

-Mtoto hupata shida katika ukuaji na kuwa na matatizo ya akili kutoka na athari ya pombe katika mfumo wa fahamu.

-Athari kubwa ya pombe hutokea katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ambapo mtoto ndio anajengeka 

-Acha pombe sana ewe mama mjamzito kwa ustawi bora wa mtoto.

13. Kupoteza kumbukumbu

-Tafiti zimeonesha kuwa unywaji wa pombe wa kupindukia unaweza kuathiri ubongo na hivyo kupelekea tatizo la kupoteza kumbukumbu mara kwa mara.

-Hali hii huweza kuchangia hata katika kupunguza ufanisi wa kazi za kila siku ofisi au shuleni.

14. Kujiumiza kwa ajali au vurugu.

-Moja ya mambo ambayo pombe husababisha ni kupoteza uwezo wa kudhibiti mazingira ya nje ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi sahihi, hii huendana sambamba na kiwango cha pombe unachokunywa.

-Hali hii huweza kupelekea mambo mbalimbali kutoka kama vile ugomvi, ajali ya gari n.k ambapo hupelekea kujiumiza sehemu za mwili au kupata ulemavu wa kudumu.

Suala la kuacha pombe ni muhimu sana kwa afya bora kutokana na ukweli ni kwamba athari ni nyingi zaidi ya hizi zilizotajwa hapa zikigusa nyanja mbalimbali za kiafya, kiuchumu, kisaikolojia na kijamii. Kama umeshaanza unywaji wa pombe kwa muda mrefu basi ni vyema kuonana na daktari kwa ajili ya kujadili namna bora ya kuacha na kama hujaanza kunywa basi unashauriwa usijaribu kuanza. 

Share:

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.