NINI SABABU AU VYANZO VYA UGONJWA WA KIHARUSI (STROKE) ?

Kiharusi ni tatizo ambalo linatokea pale sehemu ya ubongo  inapopata hitiafu kwa kukosa virutubisho na hewa ya oksijeni kwa muda mrefu kutoka na sababu mbalimbali. Tatizo hili hushika nafasi ya pili duniani kwa kusababisha vifo na nafasi ya tatu duniani  kwa kupelekea ulemavu miongoni mwa wagonjwa.  Kulingana na sehemu gani ya ubongo iliyoathirika basi mgonjwa huonesha dalili na ishara mbalimbali.

Takribani asilimia 25 ya watu wazima yani wanaume na wanawake wenye umri wa miaka 25 na kuendelea wako kwenye uwezekano wa kupata tatizo hili kipindi cha uhai wao. 

AINA ZA KIHARUSI

-Kuna aina kuu mbili (2) za Kiharusi kulingana na namna hitilafu katika ubongo ilivyotokea;

i. Kiharusi cha iskemia (Ischemic stroke)

-Takribani asilimia 80 ya wagonjwa wenye tatizo la kiharusi huathiriwa na aina hii. Katika aina hii, hali inayotokea ni kuwepo kwa ukinzania wa mtiririko wa damu katika mishipa inayopeleka damu sehemu mbalimbali za ubongo na hivyo kusababisha damu kutofika sehemu husika na kusababisha kifo cha seli za eneo lile la ubongo.

-Ukinzani wa mtiririko wa damu kwenye mishipa unaweza kutokana na ; utando katika kuta za mishipa ya damu (plaque) au kipande cha damu au mafuta kinachosafiri ndani ya mishipa ya damu.

SABABU ZA KIHARUSI CHA ISKEMIA

a. Hitilafu katika mishipa ya damu kama vile atheroskelosisi

-Atheroskelosisi ni tatizo ambalo linahusisha kutengenezeka kwa utando katika mishipa ya damu ambapo utando huo huwa na mafuta, lehemu (cholesterol), madini pamoja na vitu vingine kutoka kwenye damu. Utando huu hufanya mishipa ya damu kupungua kipenyo taratibu na mwisho kupelekea damu kutotiririkaa vizuri.

b. Maradhi mbalimbali ya moyo kama vile "atrial fibrillation"

-Atrial fibrillation ni neno la kiingereza ambapo ni ugonjwa wa moyo utokanao na hitilafu katika usafirishaji wa umeme na hii hupelekea usafirishaji wa damu katika moyo kuwa katika mtiririko hovyo ambao unaweza kupelekea kujengeka kwa vipande(mabonge) vya damu zinavyoweza kuziba mishipa ya damu kuelekea kwenye ubongo

c. Maradhi ya damu kama vile selimundu, 'polycethermia vera' n.k

-Maradhi haya yote yanahusishwa na kupelekea ukinzani (au kuziba kabisa) katika mtiririko wa damu katika mishipa yake na hiyo damu kushindwa kufika kwa usahihi sehemu za ubongo.

ii. Kiharusi cha mvilio wa damu (Hemmorrhagic stroke)

-Aina hii ya kiharusi huathiri takribani asilimia 20 ya wagonjwa wapatao tatizo hili kwa ujumla. Hali katika tatizo hili hutokea pale mishipa ya damu inayopeleka virutubisho na hewa safi katika ubongo inapopasuka au kuvuja na hivyo kusababisha seli za ubongo kufa kwa kukosa damu. 

Aina hii ya kiharusi imeonekana kupoteza sana maisha ya watu ukilinganisha na aina ya iskemia. 


SABABU ZA KIHARUSI CHA MVILIO WA DAMU

a. Shinikizo la juu la damu

-Shinikizo la juu la damu kwa muda mrefu bila ya kudhibitiwa huweza kuepelekea hitilafu katika mishipa ya damu ikiwemo kupasuka kwa mishipa midogo midogo ya kwenye ubongo na hivyo damu kuvilia na kuathiri ubongo

b. Ajali ya kichwa 

-Hii huweza kupelekea kwa kupasuka kwa mishipa mikubwa ya damu na hivyo kusababisha kiharusi

c. Hitilafu za mishipa ya damu 

-Huwa inaweza kutoka mishipa inayopeleka damu katika ubongo kuwa dhaifu hasa kuta zake na kufanya mishipa ya damu kutengeneza umbo la nundu (aneurysm). Nundu hii huwa dhaifu kiasi kwamba huweza kupasuka muda wowote. 

d. Maradhi ya kuvuja damu

-Kuna magonjwa mbalimbali ambayo hupelekea damu kushindwa kuganda mapema na hivyo hupelekea hali ya uhatari kwa kuvuja katika mishipa ya damu. Magonjwa haya mengi huwa ni ya kurithi.

e. Matumizi ya madawa.

-Baadhi ya madawa wanayotumia wagonjwa kama warfarin yanaweza kupelekea damu kuvuja kwenye mishipa ya damu kwani dawa hizi hufanya kazi ya kuzuia damu isitengeneze mambo ya damu (isigande) 

Tatizo la kiharusi humtokea mtu hasa ambaye ana vihatarishi  ambavyo huchangia kutokea kwa ugonjwa huu na ukizingatia vyanzo vyake lakini aghalabu linaweza kumtokea mtu asiye na vihatarishi hivyo. Fanya uzidi kufuatilia ufahamu vihatarishi vya tatizo la kiharusi ni vipi.

Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.