JE UTAMTAMBUAJE MGONJWA MWENYE TATIZO LA KIHARUSI (STROKE)

 Ukifahamu nini kinatokea kwa mtu aliyepatwa na kiharusi basi unaweza kuwa na mchango mkubwa sana katika kupunguza athari zitokanazo na tatizo hili. Dalili za kiharusi mara nyingi hutokea ghafla na huweza kupungua makali au kuwa mbaya zaidi kulingana na aina ipi na sehemu ya ubongo iliyoathirika. 

Mtu aliyepatwa na kiharusi huonesha wigo mpana wa dalili kulingana na kiasi cha sehemu ya ubongo iliyoathiriwa. Dalili hizi ni pamoja na;

1. Kupoza au ganzi katika maeneo ya mwili.

-Hali hii huweza kutokea kwenye maeneo ya uso, mikono au migu. Mara nyingi huathiri upande mmoja wa mwili yani upande mmoja wa uso au mikono au miguu au vyote (miguu na mikono). 

-Kushindwa kutembea, kunyong'onyea upande mmoja wa uso anapotabasamu, pamoja na kushindwa kunyanyua mikono juu ya kichwa ni viashiria vya kupooza.

2. Kushindwa kuongea na kuelewa vizuri.

-Endapo sehemu ya ubongo inayohusika na uelewa na kufanya mawasiliano ya kuongea imeathirika basi mgonjwa hujikuta hawezi kuongea au hakuelewi kabisa. Ikitokea anatoa sauti basi zinaweza kuwa sauti ambazo hazieleweki na uongeaji kama mtu aliyelewa lakini pia mgonjwa huyu anaweza kuwa nakuelewa ila anashindwa kujibu au hajibu kwa usahihi.


3. Kupoteza au kupungua kwa ufahamu.

-Mara kadhaa mtu aliyepatwa na kiharusi huweza kujikuta anashindwa kutambua watu wanaomzunguka, majira katika siku (asubuhi, mchana au usiku) na hata mahali alipo wakati huo. Hali hii inaweza kwenda zaidi hadi kupoteza fahamu kabisa kwa muda mrefu mpaka pale atakapopata matibabu sahihi

4. Kushindwa kutembea

-Kutokana na udhaifu au kupoza kwa miguu wagonjwa wengi hushindwa kutembea wakati huo mpaka pale watakapoonza tiba sahihi hasa ya mazoezi kutoka kwa wataalamu wa fiziotherapi.

         

4. Kundishwa kuona vizuri

-Tatizo hili linaweza kupelekea kuona maruerue au kiza ghafla katika jicho moja au yote mawili. Pia inawezekana mtu kuona vitu viwiliviwili.

6. Kichwa kuuma sana

-Hii ni moja ya dalili ya kiharusi ambayo si mahususi ila mara kadhaa imewatokea watu wengi wanaopatwa na kiharusi huku ikiambatana na hali ya kichefuchefu au kutapika au kizunguzungu.

Ikumbukwe tu kuwa Kiharusi ni tatizo la dharura na madhara yake yanendana sambamba na ucheleweshwajiwa tiba sahihi. Hivyo uonapo dalili hizi kwa mtu ni vyema kuonana na daktari haraka sana ili uchunguzi na matibabu yaweze kufanyika mapema zaidi.


Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.