• This is default featured slide 1 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 2 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 3 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 4 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 5 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

WASILIANA NA DAKTARI UONAPO DALILI HIZI MARA BAADA YA KUANZA KUTUMIA DAWA ZA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU (PRESHA YA KUPANDA)

 Utumiaji wa dawa za shinikizo la juu la damu ni moja ya matibabu ya tatizo hili sambamba na kuzingatia mtindo bora wa maisha. Lengo kuu ni kuweza kudhibiti vizuri shinikizo la juu la damu katika kiwango kinachotakiwa ili kuepuka madhara makubwa yatokanayo na shinikizo la juu la damu. Dawa mbalimbali zimekuwa zikitolewa kwa wagonjwa wa shinikizo la juu la damu kwa mafanikio makubwa sana huku wagonjwa wengi wakitumia dawa hizi kwa muda mrefu sana bila ya kuacha. 

Dawa hizi kama ilivyo kwa dawa zingine zinaweza kukuleta madhara madogo madogo hadi makubwa licha ya kukutibu vyema shinikizo la juu la damu, baadhi ya madhara haya unayoweza kurudi na kuripoti kwa daktari ni pamoja na;

1. Kupungua kwa nguvu ya uume.

-Hii imekuwa ni changamoto kubwa sana kwa baadhi ya wagonjwa kutokana na baadhi ya watu kupatwa na tatizo hili la uume kulegea kutokana na matumizi ya dawa za presha ya kupanda. 

-Si dawa zote ambazo zinapelekea hali hii bali ni baadhi tu na hali hii ya kupungua kwa nguvu za kiume si wagonjwa wote hupatwa licha ya dawa ile ile inayotumika kwa wengine pia.

2. Kikohozi kikavu 

-Baadhi ya dawa za presha ya kupanda hupelekea baadhi ya wagonjwa wa shinikizo la juu la damu kuanza kupata kikohozi kikavu ndani ya siku hadi wiki chache tangu kuanza kutumia. 

-Hali hii inakuwa ni usumbufu kwa mgonjwa na kumkosesha amani. Ni vizuri mtumiaji wa dawa kuweza kuwa na utambuzi wa karibu sana wa dawa zote anazotumia na kuona ni dawa ipi inamletea shida hii ili kuweza kubadilishiwa. 


3.  Kuvimba macho na mdomo

-Hali hii huweza kuwatokea baadhi ya wagonjwa mara baada ya kumeza dawa za shinikizo la juu la damu. Hii hutokana na uzio katika dawa hizo ambapo kimiminika hujikusanya baadhi ya maeneo ya mwili hasa mdomoni, machoni, kwenye koo, kwenye korodani n.k

-Upatapo hali hii mara baada ya matumizi ya dawa, onana haraka na mtaalamu wa afya kwa matibabu sahihi na kuweza kupata dawa mbadala.

4.  Kichwa kuuma sana.

-Maumivu makali sana ya kichwa hasa mara baada ya kumeza baadhi ya dawa za presha ya kupenda huwasumbua baadhi ya wagonjwa. 

-Hali hii inaweza kupoa kwa muda tu mara baada ya kutumia dawa za kutuliza maumivu na kisha kurudi. Endapo usipomeza dawa hizo huwezi kusikia maumivu yoyote ya kichwa.

5. Kutopata usingizi .

-Ikiwa kabla ya matumizi ya dawa za shinikizo la juu la damu, mgonjwa ulikuwa unapata usingizi vizuri kabisa kisha ukaanza kuona mabadiliko makubwa zaidi ya kutopata usingizi hasa baada ya kuanza kutumia dawa. Inawezekana ikawa inachangiwa na umezaji wa baadhi ya dawa za presha ya kupanda. 

-Usingizi bora ni afya, rudi kwa mtaalamu wa afya na ripoti hali hii kuweza kujadiliana na daktari.

6. Miguu kuvimba

-Moja ya madhara ya dawa hizi yameweza kuonekana kwa wagonjwa wengi ni kuvimba miguu baada ya kuanza kutumia dawa za shinikizo la juu la damu. 

-Wengine miguu hujaa kiasi cha kuwa shida katika kutembea, hivyo usikae kimya  bali fika kwa mtaalamu wa afya na kutoa taarifa.

Matumizi ya dawa kudhibiti shinikizo la juu la damu yana faida kubwa sana kuliko madhara yake kwani hukuepusha na magonjwa ya kiharusi, shambulizi la moyo, na hata kifo katika umri wa mapema. Madhara haya ya dawa ni muhimu kuyaripoti kwa daktari kwa uchunguz zaidi na tiba sahihi kwani  madhara haya si mahususi kwa dawa hizi pekee.

Share:

MAMBO SABA (7) YA KUZINGATIA ILI KUANDAA MLO ULIO KAMILI KWAKO NA FAMILIA YAKO.

Matatizo mengi ya kiafaya yamekuwa yakichangiwa na lishe ambayo si sahihi na hii hutokana na watu wengi kutofahamu nini cha kufanya ili kufanikisha mlo kamili. Kufanikiwa katika ulaji bora ni pamoja na kuzingatia vidokezo mbalimbali vya ulaji vinavyopendekezwa na wataalamu wa lishe. Hii husaidia katika kufanikisha malengo yako mengi ya kiafya yatokanayo na lishe bora. 

Kupata matokeo bora katika lishe yako ni vyema kuzingatia mambo yafuatayo;

1. Andaa mlo wenye angalau chakula kimoja kutoka katika kila kundi la vyakula.

-Vyakula viko katika makundi tofauti tofauti na kila kundi likiwa na umuhimu wake kiafya. Kupata virutubisho vyote na sahihi inatakiwa kuchukua chakula angalau kimoja katika makundi haya na kuandaa mlo wako, makundi haya ni;

  • Nafaka isiyokobolewa, ndizi na vyakula vya mizizi

-Vyakula hivi ni pamoja na mahindi, ngano, mchele, mtama na uwele. 

-Vyakula vya mizizi ni pamoja na mihogo, magimbi, viazi vitamu, viazi mviringo na vikuu.

-Vyakula hivi huwa na kiasi kikubwa cha makapi na vina sukari iliyo salama zaidi.

  • Mboga za majani na Matunda
-Mboga za majani ni pamoja na spinanchi, matembele, sukuma wiki, mlenda, mchicha, kisamvu bila ya kusahau mboga mboga kama bamia, nyanya, maboga, karoti, biringanya, hoho, nyanyachungu n.k

-Kuna matunda mbalimbali unawez akuyaanda katika mlo wako ikiwemo; ndizi, maembe, nanasi, parachichi, tikitimaji, mapapai, mapesheni, machungwa n.k

  • Vyakula vya jamii ya kunde
-Hivi vinajumuisha  maharagwe, njegere, kunde, mbaazi, njugu mawe, choroko n.k

  • Vyakula vya asili ya wanyama

-Hapa hujumisha haswa vyakula kama maziwa, nyama isiyo nyekundu (bata, kuku), samaki, mayai,mayai, karanga n.k

  • Mafuta na sukari
-Mafuta kutoka katika mimea ni salama zaidi kama vile ufuta, alizeti na karanga. Sukari nzuri ni ile ya asili kama ya kwenye asali lakini sukari zinazoongezwa kwenye vyakula au vinywaji ni za kupunguza kabisa katika matumizi.

2. Epuka vyakula vyenye mafuta mengi yasiyo salama kiafya.

-Mafuta kutoka kwenye siagi, mafuta ya nazi na mchikichi pamoja na vyakula vya kukaanga, piza, keki, biskuti n.k  si salama kwani huchangia kwa maradhi ya moyo na mishipa ya damu. 

-Badala ya kukaanga unaweza kuoka au kuchemsha vyakula.

3. Nusu ya sahani yako iwe ni mboga za majani na matunda.

-Vyakula hivi ni vizuri sana kiafya kwani huwa na virutubisho vingi vya vitamini, madini, sukari asili na makapi ambavyo vyote kwa pamoja husaidia kuulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo, saratani, kisukari n.k

4. Nusu ya nafaka unayoitumia iwe ni nafaka isiyokobolewa.

-Nafaka iliyokobolewa hupoteza ubora wake kwa kupungukiwa na virutubisho kama makapi ambayo ni muhimu sana mwilini.

-Pia nafaka iliyokobolewa hubaki kuwa na kiwango kingi cha sukari na hivyo kutokuwa salama sana kwa matumizi.

-Nafaka isiyokobolewa kama unga wa dona na unga wa ngano ni bora kiafya siku zote.

5. Epuka matumizi ya chumvi kupita kiasi.

-Kiasi kingi cha chumvi huingizwa mwilini kupitia ulaji wa vyakula kutoka viwandani kama nyama za makopo, maharagwe ya makopo n.k, 

-Pia kupindi cha upishi majumbani na wakati wa kula, chumvi nyingi huweza kutumika.

-Punguza kiwango cha chumvi hadi kijiko kimoja cha chai au chini ya hapo kwa siku ili kuwa salama dhidi ya maradhi ya moyo. 

                                 

6. Epuka ulaji wa sukari ya kuongezwa.

-Siku hizi vyakula ni vingi sana vinavyoongezewa sukari huko viwandani kama vile; soda, jamu, biskuti, juisi, keki, chokoleti n.k. 

-Aina hii ya vyakula ni ya kuepuka kwani huwa na sukari ambayo si salama kifya dhidi ya magonjwa yakuambukizwa kutokana na kuwa chanzo cha uzito wa uliopitiliza au unene kwa watu wengi.

7. Kunywa maji safi na salama.

-Maji ni muhimu sana kuwa sehemu vya mlo wako kila siku ingawa si sehemu ya virutubisho. Bila ya maji mwili hauwezi kufanya kazi ipasavyo. Kunywa maji ya kutosha kila siku kulingana na uzito wako, hali ya hewa, shunguli zako n.k.

Mambo yaliyotajwa hapo juu yote yanajumuisha suala la mtindo wa ulaji bora , na kwa kuzingatia hayo ni wazi kabisa utakuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kuepuka maradhi sugu yasiyoambukizwa. 

Share:

MADHARA KUMI NA NNE (14) YA KIAFYA YATOKANAYO NA UVUTAJI WA SIGARA AU TUMBAKU.

 Uvitaji wa sigara au tumbaku ni moja ya mtindo wa maisha usio salama katika jamii kwani huchangia kwa kiasi kikubwa kwa magonjwa yasioyoambukiza yani maradhi ya mapafu, moyo, kisukari na saratani. Tafiti zimeonesha kuwa wastani wa 8.7% ya watu wazima Tanzania wanatumia tumbaku/sigara huku wanaume wakiongoza kwa asilimia 14.6 wakati  asilimia 3.2 ni wanawake. Wavutaji wa sigara wamekuwa wakiwaathiri watu wengi wasiovuta kutoka katika moshi huo pia katika maeneo ya kazi na manyumbani. Kutokana na vifo vitokanavyo na uvutaji wa sigara kuwa vingi, ni vyema jamii kupata hamasa ya kuepuka matumizi haya ya tumbaku ili kuwa na afya bora.Yafuatayo ni madhara ya kiafya yatokanayo na matumizi ya sigara/ tumbaku 

1. Hupelekea saratani mbalimbali.
-Uvutaji wa moshi wa tumbaku huathiri mifumo mbalimbali ya mwili ikiwemo mfumo wa upumuaji hasa mapafu. 
-Hii hutokana na kemikali sumu zilizomo katika moshi wa tumbaku kuumiza taratibu njia za hewa na kuanza kuleta mabadiliko ya saratani. 
-Saratani ya mapafu imekuwa ni moja ya saratani ambazo huathirika zaidi kutoka na moshi huu huku zingine zikiwa ni pamoja na saratani za mdomo, umio, tumbo, kongosho, utumbo mpana, figo na kibofu cha mkojo.
2. Huathiri mbegu za uzazi za mwanaume.
-Mabdiliko mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanaume yameweza kuonekana kutokana na athari ya kemikali sumu za tumbaku katika mfumo ikiwemo;
  • Kutengeneza shahawa zisizo na umbo kamili
  • Shahawa zenye uwezo mdogo wa kutembea
  • Kutengeneza shahawa chache na zisizojitosheleza n.k
-Yote haya ni huweza kumfanya mwanaume kutokuwa na uwezo wa kumpa mimba mwanamke na lakini zaidi huweza kupunguza nguvu za kiume pia.
3. Huathiri mfumo wa uzazi wa mwanamke
-Athari mbalimbali katika mfumo wa uzazi zimeweza kuonekana zikiwemo kama;
  • Kuharibu mzunguko wa hedhi kwa kutokuwa wa kuhakika katika siku
  • Kupunguza kiwango cha homoni za uzazi (Estrogeni) katika mwili.
  • Kupelekea kufunga mzungo katika umri wa mapema.
-Mabadiliko yote haya huweza kusababisha mwanamke kutokuwa na uwezo wa kushika mimba.
4. Kuharibu mimba na mtoto aliyeko tumboni.
-Uvutaji wa tumbaku kabla na wakati wa ujauzito hupelekea athari nyingi mengi zikiwemo;
  •  kuharibika kwa mimba katika miezi ya mapema 
  • kutungwa kwa mimba nje ya mfuko wa uzazi, 
  • kuzaa mtoto mwenye hitilaju nyingi sana zikiwemo za mtoto mwenye uzito mdogo sana kuliko kawaida
-Haishauri kutumia kabisa tumbaku au sigara kwa mama mjamzito kwani madhara yake ni mengi sana ya zaidi ya hayo yaliyotajwa.
5.  Kupata mivunjiko ya mifupa
-Madhara haya yameonekana sana kwa wanawake kutoka na athari ya tumbaku ya kupunguza homoni ya Estrogeni mabayo hupelekea mifupa kupungukiwa uimara wake na hiyo kuwa kwenye hatari ya kupata mivunjiko ya mifupa ya nyonga n.k
-Kuanza kuvuta sigara kwa zaidi ya miaka 10 hupunguza athari hii ya mifupa.
6. Huchangia kwa maradhi ya moyo.
-Athari za tumbaku ni nyingi sana katika mfumo mzima wa moyo na mishipa ya damu huku uvutaji wa sigara ukiwa unachangia kwa zaidi ya 10% ya vifo vyote vitokanavyo na maradhi ya moyo
-Na hii hutokana na moshi wa sigara/tumbaku kupelekea;
  • Kusinyanyaa kwa mishipa ya damu ya moyo
  • Kuongeza hali ya damu kuganda
  • Kuharibu kuta za mishipa ya damu n.k
-Mabadiliko hasi yote hayo hupelekea kwa ongezeko la shambulizi la moyo, kiharusi na hata vidonda sugu katika miguu huku matatizo haya yakionekana kuongezeka zaidi miongoni mwa wavuta sigara kuliko wasiovuta.
7. Kupelekea kwa maradhi sugu ya mapafu
-Mbali na saratani ya mapafu, wavutaji wa sigara huweza kupata athari ya moja kwa moja ya kwenye mapafu kw kuyafanya mapafu kushindwa kufanya kazi yake.
-Mababdiliko ya sehemu mbalimbali za mapafu ni moja ya chanzo cha maradhi haya na humfanya mtu kushindwa kuhema vizuri, kifua kupana na kupata kikohozi cha muda mrefu takribani miaka 2 pamoja na dalili zingine.
8. Kushambuliwa na vimelea vya magonjwa.
-Uvutaji wa tumbaku unapelekea watu wengi kupatwa na vimelea vya magonjwa hasa vya bakteria ambapo huweza kusababisha mtu kupata kirahis maradhi kama kifua kikuu, pneumonia, mafua ya mara kwa mara n.k 
8. Huchangia kwa vidonda vya tumbo.
-Tafiti zimeonesha kuwa vidonda vya tumbo na utumbo vimeoneka kutokea zaidi kwa watu wanaovuta sigara au tumbaku kuliko wasiovuta
-Lakini pia utumiaji wa sigara umeoneka kuchangia kwa kushindwa kwa matibabu ya dawa za vidonda vya tumbo.
9. Hupelekea ugonjwa wa Kisukari.
-Moja ya kemikali sumu iliyopo kwenye sigara inaitwa nikotini, kemikali hii imeoneka kuathari utendaji kazi wa homoni ya Insulini kiasi cha kupelekea ongezeko la sukari katika damu na hivyo kupata ugonjwa wa kisukari aina ya pili.

10. Maradhi ya kinywa na meno.
-Meno pamoja na fizi huaribika kutokana na uvutaji sigara na kupelekea kupoteza meno. Tafiti zimeonyesha waathirika wengi wa meno na fizi kuwa ni wavutaji sigara huku athari hii ikipungua kadiri miaka inavyoongezeka tangu kuacha uvutaji. 
11. Hupunguza uwezo wa macho kuona.
-Athari ya matumizi ya sigara au tumbaku ni pamoja na kuathiri lensi ya jicho (kuonekana kama yenye ukungu hivi) na sehemu ya retina ambapo kwa ujumla hupelekea macho kutoona vizuri na zaidi huweza kusababisha upofu.
12. Kuchelewa kwa vidonda kupona.
-Matumizi ya sigara au tumbuka  huchangia kwa kiasi kikubwa kuchelewa kwa vidonda kupona hasa mara baada ya kujiumiza au kufanyiwa upasuaji fulani. 
-Kuacha uvutaji wa sigara kumenonekana kusaidia kupona vidonda kwa haraka.
13. Kuatharika kwa maungio mwilini.
-Uvutaji wa tumbaku umehusishwa na kupata hitilafu ya maungio ya sehemu mbalimbali hasa mikononi. Hali hii hupelekea maumivu makali ya viungo pamoja na kuharibu muonekano wa maeneo hayo.
-Hii imeonekana kwa watumiaji wa sigara au tumbaku kwa zaidi ya miaka 20.

14. Kifo.
-Kutoka na maradha mengi yanayotokana na uvutaji wa sigara au tumbaku watu wengi hupoteza uhai katika umri mdogo kabisa kwani uvutaji wa sigara wenyewe tu hupunguza miaka ya kuishi ukilinganisha na mtu asiyevuta sigara.
Ni wajibu wa kila mtu kufahamu madhara haya makubwa ya uvutaji tumbaku ili kuweza kupata hamasa ya kuacha uvutaji au kutojaribu kabisa kuvuta kama hujaanza. Matumizi ya tumbaku ni hatari kwa afya yako.
-
Share:

NIFANYAJE KUPUNGUZA MATUMIZI YA CHUMVI NYINGI KWA UDHIBITI IMARA WA SHINIKIZO LA DAMU (PRESHA)?

 Ni ukweli usiopingika kuwa matumizi ya kiwango kikubwa cha chumvi miongoni wa watu yamechangia kwa kiasi kikubwa ongezekeo la shinikizo la damu. Na zaidi ni kuwa matumizi haya makubwa yamekuwa yakichangia katika udhibiti hafifu wa tatizo la shinikizo la juu la damu kwa wagonjwa wengi aidha walioko katika tiba ya mtindo bora wa maisha au katika tiba ya dawa na mtindo bora wa maisha.  Ikumbukwe kuwa shinikizo la juu la damu ni moja ya sababu kuwa ya maradhi ya moyo ambayo hupelekea vifo vingi mno kwa wagonjwa. Unaweza kupunguza kiwango cha chumvi katika chakula chako kwa kuwa chini ya gramu 5 (sawa na kijiko kimoja cha chai kwa siku) kwa mbinu hizi;

1. Andaa chakula chako nyumbani.

-Kuandaa chakula nyumbani husaidia sana kuliko kula vyakula kutoka kwenye migahawa na ambavyo tayari vimeandaliwa kiwandani.

-Ukipika chakula nyumbani utaweza kudhbiti kiwango chako kwa njia kama za kutumia baadhi ya viungo vya chakula vyenye kuleta radha ya chakula kuliko kutumia chumvi.

-Kumbuka tu takribani 80% ya chumvi inayoingia mwilini hutoka kwenye vyakula vya mahoteli na vyakula vilivyosindikwa.

2. Epuka vyakula vilivyo tayari kutoka viwandani.

-Vyakula hivi ni hatari kwa kiwango kikubwa cha chumvi kwani uwepo wa chumvi nyingi katika vyakula vya viwandani ni moja vya njia ya kuhifadhi vyakula hivyo. 

-Kama unajali afya yako basi ni muda sahihi wa kuepuka vyakula hivi na kuweza kuanda chakula mwenyewe ambapo ndio njia bora zaidi. 

3. Soma vizuri maandishi ya lishe katika vyakula vya madukani au "supermarkets" kabla ya kununua.

-Kutoka na ubize wa kazi watu wengi wamejikuta wakinunua vyakula katika maduka na kutumia huku vikiwa ndio vyanzo vya chumvi nyingi. 

-Ni muhimu kusoma maandishi katika vyakula na kununua vile tu ambavyo vinakuwa na chumvi kidogo (low sodium) au hakuna kabisa (no salt added) na ni jambo la busara kutonunua endapo hakuna maandishe ya lishe katika chakula hicho.

4.  Tumia zaidi mboga za majani na matunda yaliyo freshi.

-Utumiaji wa viu hivi kusaidia sana kupunguza matumizi ya kila siku kwenye vyakula vyenye chumvi nyingi na hivyo kuweza kuendelea kudhibiti shinikizo lako la damu

-Kula mboga za majani na matunda angalau mara 5 katika nyakati tofauti za milo yako, hii ni muhimu kwa afya yako.

-Epuka matunda na mboga za majani zilizotuzwa toka viwandani.

5. Toa taarifa chakula chako kisiongezewe chumvi unapokula hotelini.

-Ni muhimu sana kwa watu wanaokwenda kula chakula kwenye hoteli au migahawa kuwa wazi kwa kutoa taarifa ya kutoongezewa chumvi katika chakula chako. Hii ni namna nzuri ya kujiepusha na matumizi ya chumvi nyingi.

-Hii ni pamoja nakuweza kutoa taarifa katika baadhi ya namna ya uandaaji wa vyakula mfano nyama au samaki iliyochomwa , kuokwa n.k ni za kuepuka huku ukihitaji zaidi chakula kikiwa freshi.

6. Kuwa tayari kukubali kutumia kiwango kidogo cha chumvi.

-Ni muhimu kujenga akili/ utashi wako kukubaliana na hali ya kupunguza matumizi ya chumvi kwa kutambua athari zake kiafya katika mwili. 

-Kwa kufanya hivi itakuwa ni rahisi kwa mambo yote yaliyotajwa hapo juu kuweza kutekelezeka na kuendeleza tabia hiyo pasipo kuona ni adhabu.

Kuzingatia matumizi ya chumvi katika kipindi hiki ambacho magonjwa yasiyoambukizwa yanazidi kuongeza ni suala la kuzingatia sana ili kuweza kupunguza maradhi haya hasa ya moyo. Jamii ni lazima ihimizwe kila siku kuhusia na kupunguza matumizi ya chumvi kutoka kwa wataalamu wa afya lakini pia serikali nayo izidi kuweka sera nzuri ambazo zinasaidia katika kupunguza viwango vya chumvi katika vyakula vya kutoka viwandani.

Share:

MAMBO KUMI NA MOJA (11) YANAYOCHANGIA NA KUONGEZA UWEZEKANO WA MTU KUPATA SARATANI YA MATITI

 Saratani ya matiti n moja ya saratani ambazo zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa kudhoofisha afya pamoja na kupelekea vifo miongoni mwa wanawake wengi duniani. Kwa Tanzania saratani hii hushika nafasi ya pili baada ya saratani ya shingo ya uzazi kwa kusababisha vifo miongoni mwa wagonjwa wenye saratani mbalimbali. Inakadiriwa mpaka kufikia mwaka 2030, idadi ya waathirika itakuwa imefika mpaka 82% hivyo ni muhimu sana kwa watu kufahamu mambo ambayo ni hatarishi na kuweza kuchukua tahadhari mapema. Mambo haya yanayochangia ni pamoja na; 

1. Kuongezeka umri
-Hii ni sababu ambayo ni kubwa na haiwezekana kuizuia. Kadiri umri unavyoongezekana tangu kuzaliwa ndio nafasi ya kupata saratani hii nayo huongezeka. 
-Tafiti nyingi zimeonesha kuwa wanawake wengi wanakuwa kwenye nafasi kubwa ya kupata saratani hii katika umri wa miaka 40 hadi 60.
-Hivyo ni muhimu kufanya uchunguzi wa matiti inapofika umri wa miaka 40 na kuendelea ili kuweza kujua afya yako mapema.
2. Jinsi ya kike
-Kuwa mwanamke ni kihatarishi cha moja kwa moja kwani imeonakena kuwa saratani hii ya matiti huwaathiri wanawake mara 100 za wanaume. 
-Kitu cha kukumbuka hapa ni kuwa hata wanaume wanaweza kupata saratani hii ingawa tu nafasi ya wanaume ni ndogo
3.Asili ya watu weupe(wazungu).
-Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa asili ya watu weupe wamekuwa katika nafasi kubwa ya kupatwa na saratani hii ukilinganisha na watu wenye asili ya weusi.
-Hii haina maana kuwa watu weusi hawapati, wanapata saratani hii pia lakini katika kiwango tofauti kidogo na watu wenye asili ya weupe (wazungu)
4. Historia ya saratani katika familia.

-Uwepo wa historia ya saratani ya matiti miongoni mwa wanafamilia kama baba, mama au watoto huongeza nafasi kubwa kwa mtu mwingine kupata saratani hii kwa baadae.

-Kadiri idadi ya waathirika katika familia inavyokuwa kubwa ndio na nafasi ya kupata saratani ya matiti inaongezeka.

-Mbali na historia ya saratani ya matiti, kuna historia ya saratani ya ovari nayo huongeza nafasi ya mwanafamilia kuathirika na saratani ya matiti

5. Historia binafsi ya saratani au maradhi ya titi ambayo si saratani.

-Mwanamke ambaye ana historia ya saratani ya titi wakati fulani anakuwa katika uwezekano mkubwa na kupata tena saratani hii miaka ya mbeleni katika titi lile lile au jingine.

-Lakini pia kuna maradhi ya matiti ambayo si saratani mwanamke anaweza akawa nayo yakamuongezeka nafasi ya kupata saratani ya matiti kwa miaka ya mbeleni.


6. Kupata hedhi ya kwanza katika umri mdogo au kuchelewa kufunga mzunguko.

-Tafiti nyingi zimeonesha kuwa kupata hedhi ya kwanza katika umri mdogo hasa kabla ya miaka 13 huweza kuchangia kwa saratani hii baadae ukilingani na kupata hedhi ya kwanza baada ya miaka 15.

-Suala hili limekuwa likihusishwa na athari ya muda mrefu ya homoni ya estrogeni kwa makundi haya mawili.

7. Mwili kupata tiba mionzi kabla ya miaka 30.

-Kupata tiba inayohusisha mionzi hasa katika maeneo ya kifua na hata matiti kutoka na sababu zingine za kiafya huweza kuchangia kutokea kwa saratani hii.

-Hii hutokana na uwezekano wa mionzi hiyo mikali na yenye nguvu kuathiri seli ya mwili katika eneo husika.

8. Kuchelewa kupata ujauzito wa kwanza au kutozaa kabisa.

-Kutozaa au kuchelewa kupata ujauzito katika umri mkubwa hasa kuanzia miaka 35 na kuendelea huongeza uwezekana wa kupata saratani ya matiti.

-Kuzaa kumeonekana kuwa na msaada kwa kipindi dhidi ya saratani ya matiti.  

-Suala hili huenda sambamba na kutonyonyesha wa mtoto ambapo huongeza nafasi ya saratani hii.

9.  Matumizi ya madawa ya uzazi 

-Dawa za uzazi wa mpango za kumeza ambazo ndani yake huwa na homoni ya estrogeni huchangia kutokea kwa saratani hii ikiwa zitatumika kwa zaidia ya miaka mitano

-Matumizi ya dawa za homoni (estrogeni na progesteroni) kwa akina mama baada ya kufunga mzunguko ni hatari kwani kuweza kupelekea saratani ya matiti pia.

10. Unene 

-Mbali na vihatarishi vingine, nafasi ya kupata saratani ya matiti imeonekana kuongezeka miongoni mwa wanaake ambao ni wa nene ukilinganisha na ambao wako kwenye uzito wa kawaida.

-Jambo hili limeonekana likiathiri zaidi wanawake ambao wamefunga mzunguko wa hedhi huku uzito wa kawaida kwa wanawake ambao bado hawajafunga mzunguko huwapunguzia nafasi ya saratani hii.

11. Utumiaji wa pombe na sigara

-Matumizi ya vitu hivi huchangia kwa wanawake wengi kuathirika na saratani hii ya matiti na hapa ni aidha unatumia kimoja wapo au vyote bado uwezekano upo pale pale kuliko ambaye hatumii kabisa.

Ufahamu wa mambo haya hatarishi kwa saratani ya matiti ni muhimu kwani unaweza ukafanya tathimini mwenyewe na kujua wapi pa kurekebisha hasa kwa mambo ambayo yanaweza kudhibitika. Kwa kufanya hivi basi unapata nafasi ya kuendelea kujiwekea mazingira salama kwa afya bora. 

Share:

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.