Saratani ya matiti n moja ya saratani ambazo zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa kudhoofisha afya pamoja na kupelekea vifo miongoni mwa wanawake wengi duniani. Kwa Tanzania saratani hii hushika nafasi ya pili baada ya saratani ya shingo ya uzazi kwa kusababisha vifo miongoni mwa wagonjwa wenye saratani mbalimbali. Inakadiriwa mpaka kufikia mwaka 2030, idadi ya waathirika itakuwa imefika mpaka 82% hivyo ni muhimu sana kwa watu kufahamu mambo ambayo ni hatarishi na kuweza kuchukua tahadhari mapema. Mambo haya yanayochangia ni pamoja na;
-Uwepo wa historia ya saratani ya matiti miongoni mwa wanafamilia kama baba, mama au watoto huongeza nafasi kubwa kwa mtu mwingine kupata saratani hii kwa baadae.
-Kadiri idadi ya waathirika katika familia inavyokuwa kubwa ndio na nafasi ya kupata saratani ya matiti inaongezeka.
-Mbali na historia ya saratani ya matiti, kuna historia ya saratani ya ovari nayo huongeza nafasi ya mwanafamilia kuathirika na saratani ya matiti
5. Historia binafsi ya saratani au maradhi ya titi ambayo si saratani.-Mwanamke ambaye ana historia ya saratani ya titi wakati fulani anakuwa katika uwezekano mkubwa na kupata tena saratani hii miaka ya mbeleni katika titi lile lile au jingine.
-Lakini pia kuna maradhi ya matiti ambayo si saratani mwanamke anaweza akawa nayo yakamuongezeka nafasi ya kupata saratani ya matiti kwa miaka ya mbeleni.
6. Kupata hedhi ya kwanza katika umri mdogo au kuchelewa kufunga mzunguko.
-Tafiti nyingi zimeonesha kuwa kupata hedhi ya kwanza katika umri mdogo hasa kabla ya miaka 13 huweza kuchangia kwa saratani hii baadae ukilingani na kupata hedhi ya kwanza baada ya miaka 15.
-Suala hili limekuwa likihusishwa na athari ya muda mrefu ya homoni ya estrogeni kwa makundi haya mawili.
7. Mwili kupata tiba mionzi kabla ya miaka 30.
-Kupata tiba inayohusisha mionzi hasa katika maeneo ya kifua na hata matiti kutoka na sababu zingine za kiafya huweza kuchangia kutokea kwa saratani hii.
-Hii hutokana na uwezekano wa mionzi hiyo mikali na yenye nguvu kuathiri seli ya mwili katika eneo husika.
8. Kuchelewa kupata ujauzito wa kwanza au kutozaa kabisa.-Kutozaa au kuchelewa kupata ujauzito katika umri mkubwa hasa kuanzia miaka 35 na kuendelea huongeza uwezekana wa kupata saratani ya matiti.
-Kuzaa kumeonekana kuwa na msaada kwa kipindi dhidi ya saratani ya matiti.
-Suala hili huenda sambamba na kutonyonyesha wa mtoto ambapo huongeza nafasi ya saratani hii.
9. Matumizi ya madawa ya uzazi-Dawa za uzazi wa mpango za kumeza ambazo ndani yake huwa na homoni ya estrogeni huchangia kutokea kwa saratani hii ikiwa zitatumika kwa zaidia ya miaka mitano
-Matumizi ya dawa za homoni (estrogeni na progesteroni) kwa akina mama baada ya kufunga mzunguko ni hatari kwani kuweza kupelekea saratani ya matiti pia.
10. Unene
-Mbali na vihatarishi vingine, nafasi ya kupata saratani ya matiti imeonekana kuongezeka miongoni mwa wanaake ambao ni wa nene ukilinganisha na ambao wako kwenye uzito wa kawaida.
-Jambo hili limeonekana likiathiri zaidi wanawake ambao wamefunga mzunguko wa hedhi huku uzito wa kawaida kwa wanawake ambao bado hawajafunga mzunguko huwapunguzia nafasi ya saratani hii.
11. Utumiaji wa pombe na sigara
-Matumizi ya vitu hivi huchangia kwa wanawake wengi kuathirika na saratani hii ya matiti na hapa ni aidha unatumia kimoja wapo au vyote bado uwezekano upo pale pale kuliko ambaye hatumii kabisa.
Ufahamu wa mambo haya hatarishi kwa saratani ya matiti ni muhimu kwani unaweza ukafanya tathimini mwenyewe na kujua wapi pa kurekebisha hasa kwa mambo ambayo yanaweza kudhibitika. Kwa kufanya hivi basi unapata nafasi ya kuendelea kujiwekea mazingira salama kwa afya bora.
Elimu kubwa sana tunapata , ubarikiwe kiongozi
JibuFutaNi kweli pombe kali yani spirit ,zinapunguza unseen?
JibuFuta