Ni ukweli usiopingika kuwa matumizi ya kiwango kikubwa cha chumvi miongoni wa watu yamechangia kwa kiasi kikubwa ongezekeo la shinikizo la damu. Na zaidi ni kuwa matumizi haya makubwa yamekuwa yakichangia katika udhibiti hafifu wa tatizo la shinikizo la juu la damu kwa wagonjwa wengi aidha walioko katika tiba ya mtindo bora wa maisha au katika tiba ya dawa na mtindo bora wa maisha. Ikumbukwe kuwa shinikizo la juu la damu ni moja ya sababu kuwa ya maradhi ya moyo ambayo hupelekea vifo vingi mno kwa wagonjwa. Unaweza kupunguza kiwango cha chumvi katika chakula chako kwa kuwa chini ya gramu 5 (sawa na kijiko kimoja cha chai kwa siku) kwa mbinu hizi;
1. Andaa chakula chako nyumbani.
-Kuandaa chakula nyumbani husaidia sana kuliko kula vyakula kutoka kwenye migahawa na ambavyo tayari vimeandaliwa kiwandani.
-Ukipika chakula nyumbani utaweza kudhbiti kiwango chako kwa njia kama za kutumia baadhi ya viungo vya chakula vyenye kuleta radha ya chakula kuliko kutumia chumvi.
-Kumbuka tu takribani 80% ya chumvi inayoingia mwilini hutoka kwenye vyakula vya mahoteli na vyakula vilivyosindikwa.
2. Epuka vyakula vilivyo tayari kutoka viwandani.
-Vyakula hivi ni hatari kwa kiwango kikubwa cha chumvi kwani uwepo wa chumvi nyingi katika vyakula vya viwandani ni moja vya njia ya kuhifadhi vyakula hivyo.
-Kama unajali afya yako basi ni muda sahihi wa kuepuka vyakula hivi na kuweza kuanda chakula mwenyewe ambapo ndio njia bora zaidi.
3. Soma vizuri maandishi ya lishe katika vyakula vya madukani au "supermarkets" kabla ya kununua.
-Kutoka na ubize wa kazi watu wengi wamejikuta wakinunua vyakula katika maduka na kutumia huku vikiwa ndio vyanzo vya chumvi nyingi.
-Ni muhimu kusoma maandishi katika vyakula na kununua vile tu ambavyo vinakuwa na chumvi kidogo (low sodium) au hakuna kabisa (no salt added) na ni jambo la busara kutonunua endapo hakuna maandishe ya lishe katika chakula hicho.
4. Tumia zaidi mboga za majani na matunda yaliyo freshi.
-Utumiaji wa viu hivi kusaidia sana kupunguza matumizi ya kila siku kwenye vyakula vyenye chumvi nyingi na hivyo kuweza kuendelea kudhibiti shinikizo lako la damu
-Kula mboga za majani na matunda angalau mara 5 katika nyakati tofauti za milo yako, hii ni muhimu kwa afya yako.
-Epuka matunda na mboga za majani zilizotuzwa toka viwandani.
5. Toa taarifa chakula chako kisiongezewe chumvi unapokula hotelini.
-Ni muhimu sana kwa watu wanaokwenda kula chakula kwenye hoteli au migahawa kuwa wazi kwa kutoa taarifa ya kutoongezewa chumvi katika chakula chako. Hii ni namna nzuri ya kujiepusha na matumizi ya chumvi nyingi.
-Hii ni pamoja nakuweza kutoa taarifa katika baadhi ya namna ya uandaaji wa vyakula mfano nyama au samaki iliyochomwa , kuokwa n.k ni za kuepuka huku ukihitaji zaidi chakula kikiwa freshi.
6. Kuwa tayari kukubali kutumia kiwango kidogo cha chumvi.
-Ni muhimu kujenga akili/ utashi wako kukubaliana na hali ya kupunguza matumizi ya chumvi kwa kutambua athari zake kiafya katika mwili.
-Kwa kufanya hivi itakuwa ni rahisi kwa mambo yote yaliyotajwa hapo juu kuweza kutekelezeka na kuendeleza tabia hiyo pasipo kuona ni adhabu.
Kuzingatia matumizi ya chumvi katika kipindi hiki ambacho magonjwa yasiyoambukizwa yanazidi kuongeza ni suala la kuzingatia sana ili kuweza kupunguza maradhi haya hasa ya moyo. Jamii ni lazima ihimizwe kila siku kuhusia na kupunguza matumizi ya chumvi kutoka kwa wataalamu wa afya lakini pia serikali nayo izidi kuweka sera nzuri ambazo zinasaidia katika kupunguza viwango vya chumvi katika vyakula vya kutoka viwandani.