Ugonjwa wa kisukari huathiri takribani mifumo yote mwili huku macho yakiwa ni moja ya viungo ambavyo huathiriwa sana na sukari. Uwezekano wa macho ya mgonjwa mwenye kisukari kuathiriwa ni mara 25 zaidi ya mtu asiye na kisukari. Matatizo ya macho kwa mgonjwa mwenye kisukari yanaweza kuwa ya kupungua uwezo wa kuona (kuona ukungu ukungu) hadi kushindwa kuona kabisa (upofu). Sehemu mbalimbali katika jicho huathirika zikiwemo lensi ya jicho, mishipa ya damu kwenye jicho n.k
Baadhi ya mambo ya kuzingatia ili kuweza kuepusha macho yako kutokana na ugonjwa huu ni
1.Kudhibiti kiwango chako cha sukari kwenye damu.
-Hili ni jambo la kwanza na la muhimu kabisa kulifanya ili usipatwe na maradhi haya ya macho. Kufanikisha udhibiti wa sukari mwili ni pamoja na ;
- Kuzingatia mtindo bora wa maisha yani kufanya mazoezi kila siku inavyoshuriwa, kuzingatia taratibu za ulaji wa chakula, kuepuka sigara na pombe
- Kutumia dawa za ugonjwa wa kisukari kadiri ya maelekezo ya daktari
-Shinikizo la juu la damu pamoja na ugonjwa wa kisukari ni matatizo ambayo huwa yanaendana kwa karibu sana huku ugonjwa wa kisukari ukiwa ni kihatarishi kikubwa cha tatizo la shinikizo la juu la damu.
-Matatizo haya yote mawili kwa pamoja huathiri mishipa ya damu katika jicho na hivyo kufanya athari kuwa kubwa zaidi na kushamiri kwa haraka zaidi.
-Mgonjwa mwenye Kisukari anatakiwa kudhibiti kiwango chake cha shinikizo la damu kwa kiasi cha milimita za Mekyuri 130/80 au chini ya hapo ili kuwa katika mazingira salama zaidi.
3. Kuzingatia uchunguzi wa macho kadiri inavyotakiwa.
-Mgonjwa wa kisukari ni muhimu sana kufanya uchunguzi wa macho kila baada ya muda flani kwani kwa kufanya hivi husaidia kugundua hali ya jicho mapema kama tatizo limeshaanza au la na kujua hatua ya kufanya.
- Fanya uchunguzi wa macho mara moja kila mwaka endapo tu udhibiti wa sukari uko vizuri kama inavyotakiwa
- Fanya uchunguzi wa macho angalau kila baada ya miezi 3-6 endapo udhibiti wa sukari ni hafifu
- Fanya uchunguzi wa macho angalau kila baada ya miezi 6 endapo tayari kuna athari kidogo ya macho kutokana na sukari + udhibiti wa sukari unaenda vizuri.
-Tiba ya mapema ya macho endapo kuna hitilaju tayari husaidia katika kuboresha uwezo wa macho kuona lakizi pia husaida katika kupunguza kuendelea kwa madhara zaidi.
-Kuchelewa kwa matibabu ya macho katika hatua za awali ni hatari kwani taratibu unaweza kupatwa na upofu kabisa.
-Fika katika hospitali na uweze kuonana na wataalamu wa macho kwa tiba sahihi.
Kisukari bila upofu inawezekana, suala la msingi ni kuzingatia mambo yote yaliyoelezewa na pia kujenga utamaduni wa kuonana na mtaalamu wa afya kwa ushauri zaidi. Unapoona utofauti wa uonaji wako usisite kufika hospitalini mara moja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni