1. Fanya aina hususani ya mazoezi. (Specificity)
-Kila unapofanya mazoezi ni vema kulenga mazoezi moja kwa moja yanakupatia matokeo husika na si vinginevyo.
- Kama uko katika darasa la mazoezi na unataka kufanya mazoezi ya kuimarisha mfumo wa moyo na pumzi basi inatakiwa ujikite moja kwa moja katika mazoezi ya aerobiki ndani ya muda fulani.
-Na kama unataka kujenga misuli basi ni vyema ukafanya mazoezi husika moja kwa moja (pushups, kunyanyua vyuma n.k) na ukaenda zaidi katika kila misuli na muda wake.
-Kanuni hii husaidia sana kupata matokeo kwa uhakika zaidi na ndani ya muda mfupi kuliko kuwa na tabia ya kuchanganyachanganya mazoezi ambacho ndio kinafanywa na watu wengi. Tabia kama hii imewafanya watu wengi kutopata matokeo sahihi.2. Fanyisha mwili mazoezi kuliko kawaida yake. (Overload)
-Kila mara unapofanya mazoezi ni lazima kuongeza jitihada ya kuufanyisha mwili zaidi na zaidi kuliko wakati kawaida yake kwani mwili hubadilika kila siku kulingana na uzito wa kazi unavyoongezeka ili kwenda sambamba.
-Mifupa huwa imara zaidi unapotembea umbali mrefu zaidi na hata unapoubebesha vitu vizito kuliko mwili ukiwa haufanyi chochote na vilevile mfumo wa moyo, mapafu na mishipa ya damu huimarika zaidi unapokimbia umbali mrefu zaidi kuliko kukimbia umbali mfupi au kutokimbia kabisa.
-Kama unanyanyua vyuma basi ni vyema kujitahidi kuongeza namba ya "Reps" au "Sets" au uzito ili kuupa shuruba mwili na hivyo kuwa imara taratibu.
-Kuna watu ndani ya mwaka mzima wao hukimbia kilomita 1 au kama ananyanyua vyuma basi wao ni kilo 20 tu siku zote, hii si sawa kabisa kwa matokeo bora ya mazoezi.
3. Fanyisha mwili mazoezi zaidi leo kuliko jana.(Progression)
-Ni muhimu sana kuwa na namna bora ya kuweza kuufanyisha mwili mazoezi kuliko kawaida yake ili kupata matokeo mazuri zaidi.
-Kadiri unavyoufanyisha mwili mazoezi fulani hufikia hatua huzoea mazoezi hayo hivyo kuna haja ya kuwa na muendeleo chanya katika maeneo ya idadi ya vipindi vya mazoezi, aina ya mazoezi na muda kwa ujumla vipindi vya mazoezi husika.
-Kama leo umekimbia kilomita 1 basi kesho nenda asilimia 10 zaidi ya jana kisha kesho kutwa ongeza 10% zaidi hivyo hivyo, hapo mwili utaimarika na kukufanya uwe fiti.
4. Tenga siku za kupumzika
-Mapumzisho ya mwili ni sehemu muhimu sana katika mazoezi kwani husaidi mwili kujengeka na kurudisha nguvu iliyopotea katika vipindi vya mazoezi yalipita.
-Baadhi ya vigezo vya kuzingatia katika mapumziko ni pamoja na umri, hali ya hewa na aina ya mazoezi
- Vijana zaidi ya miaka 25 wanahitaji muda mwingi wa kupumzika baada ya mazoezi
- Mazoezi katika hali ya joto kali huhitaji pia muda mwingi wa mapumziko
-Kwa mazoezi ambayo yanahusisha kurarua misuli kwa kunyanyua vyuma vizito sana basi angalau masaa 24 mpaka 48 ya kupumzisha misuli husika inafaa zaidi.
-Katika kipindi hiki ni muhimu kupata usingizi wa kutosha angalau masaa 7-8, kupata mlo kamili na maji ya kutosha huku ukiepuka matumizi ya sigara, pombe, na madawa yasiyofaa kama steroids.
-Kufanya mazoezi kila siku bila ya kupumzika huambatana na madhara mengi ikiwepo kupata athari za kujiumiza, mwili kutopata nafasi ya kujijenga na hivyo kutopata matokeo sahihi.
Kanuni hizi ni kubwa mno katika mazoezi na zinaweza kukuleta mabadiliko unayoyahitaji endapo tu utaweka utayapenda mazoezi, utaweka jitihada na kuwa mvumilivu katika kipindi chote cha mazoezi. Jitahidi kufikia malengo yako ya mazoezi na kuweza kudumisha malengo hayo kila siku. Ukiacha mazoezi nayo yatakuacha
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni