Mlo kamili ni ule ambao hutokana na chakula mchanganyiko kutoka katika makundi yote ya chakula na una virutubishi vyote muhimu kwa ajili ya lishe na afya bora. Ili kupata mlo kamili inafaa kuchangua angalau chakula kimoja katika kila kundi, hii husaidia moja kwa moja kupata virutubisho vyote mwilini. Makundi haya huusisha vyakula mbalimbali ambayo huwa na virutubisho husika katika kila kundi, makundi hayo ;
1. Nafaka
-Hili ni kundi la chakula ambalo hujumuisha ngano, mchele, shayairi, mahindi, mtama n.k
-Vyakula hivi vya nafaka vinaweza kutumika moja kwa moja au kusagwa na kutumika kuandalia vyakula vingine kama chapati, maandazi, tambi, mkate, keki, biskuti , ugali , wali n.k
-Nafaka bora kiafaya siku zote ni zile ambazo hazijakobolewa kwani hubaki na virutubisho muhimu sana kuliko nafaka zilizokobolewa.
-Nafaka zisizokobolewa huwa na wingi wa makapi-mlo,vitamini na madini ambayo hayapatikani kwenye nafaka iliyokobolewa.
-Hivyo nafaka iliyokobolewa ni muhimu kuiongezea virutubisho.
2. Mboga za majani
-Hili ni kundi kubwa la jamii ya aina mbalimbali za mboga za majani. Vyakula katika kundi hili vinatoka katika sehemu tofauti tofauti za mmea kama vile kwenye maji, shina, mbegu na mizizi
-Ni kweli kabisa tafiti zimeonesha ulaji wa mboga za majani kila siku huzuia magonjwa sugu yasiyoambukizwa kama saratani, kisukari n.k
-Baadhi ya makundi ya mboga za majani ni pamoja na;
- Mboga zenye majani ya kijana; spinach, brocolli, kabeji, mchicha n.k
- Mboga zenye majani mekundu na njano; karoti, nyanya,maboga, pilipili n.k
- Mboga jamii ya kunde; njegere, maharagwe; kunde, dengu, jugu mawe
- Mboga za jamii ya mizizi;Vitunguu, Bieetroot, tangawizi, karoti
- Nyama -Inaweza kuwa ya ng'ombe, mbuzi, kuku n.k
- Samaki na jamii ya vyakula vya majini- Pweza, kaa, prawn n.k
- Mayai
- Karanga na mbegu
- Mboga jamii ya kund-Kundi hili huingia pia kwenye mboga za majani kwani huwa na virutubisho sawa na nyama, kuku samaki,na mayai.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni