• This is default featured slide 1 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 2 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 3 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 4 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 5 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

MAMBO SABA(7) YANAYOONGEZA UHATARISHI WA SARATANI YA TEZI DEMU KWA WANAUME.

Saratani ya tezi dume ni saratani ambayo inayoathiri kiungo kidogo cha uzazi wa mwanaume kiitwacho tezi dume, tezi hii hupatikana maeneo ya chini ya kibofu lakini kwa juu ya puru (rectum). Tezi dume inasaidia katika kutengeneza kimiminika kinachotumika kusafirishia shahawa wakati kutoa shawaha nje.

Saratani ya tezi inashika nafasi ya pili duniani miongoni mwa saratani zote zinazoathiri sana wanaume huku ikishika nafasi ya kwanza kuathiri na kusababisha vifo kwa wanaume nchini Tanzania.  Saratani hii huibuka taratibu taratibu kiasi cha kwamba watu wengi hupoteza maisha hata kabla ya kugundulika. Mambo ambayo yameonekana kuwa hatarishi kwa saratani hii ni pamoja na 

1.Umri 

-Wanaume wote wapo kwenye nafasi ya kupata saratani hii lakini nafasi ya kupata tatizo hili huongezeka kadiri ya umri unavyoongezeka. Tafiti nyingi zimeonesha kuwa watu wengi kuanzi umri wa miaka 50 wamekuwa wakiathiriwa na ugonjwa huu huku wachache sana na sana wakiwa chini ya miaka 50 kipindi wanagundulika na saratani hii.

2. Asili ya mtu(Chimbuko) 

-Wanaume wenye asili ya weusi wamekuwa wakiathiriwa zaidi na saratani hii kuliko wanaume wa jamii nyingine yoyote lakini pia wanaume hawa weusi wamekuwa wakipoteza maisha zaidi kutokana na saratani ya tezi dume kuliko wanaume wa jamii zingine

3. Historia ya saratani kwenye familia

-Mwanaume ambaye ana ndugu wa kiume katika familia kama vile baba au kaka ambaye ana saratani hii au amewahi kupata saratani hii basi ana nafasi kubwa sana kwa baadae kuathiriwa nayo

-Pia mwanume ambaye dada yake ana historia ya saratani ya matiti anaweza kupatwa na tatizo hili.

-Imeonekana kuwa kuna uhusiano wa saratani ya tezi dume pamoja na vinasaba(mambo ya urithi)

4. Ulaji usio sahihi

-Ulaji wa mafuta sana hasa yanayotokana na vyanzo vya wanyama pamoja na kutokula mboga za majani na matunda ( vyakula vyenye madini ya kutosha na vitamini) huchangia kujengeka kwa saratani hii.

5. Uvutaji wa sigara

-Matumizi ya sigara yamekuwa makubwa sana miongoni mwa wanaume kati ya umri 24-65 huku saratani hii ya tezi dume ikionekana kuathiri zaidi wanaume ambao ni wavuta sigara kuliko ambao hawavuti sigara.

6. Unene

-Hiki ni moja ya kitu kinachochangia kutokea kwa saratani ya tezi dume miongoni mwa wanaume kutoka kwenye tafiti mbalimbali zilizoweza kufanyika na wataalamu wa afya


7. Kutofanya mazoezi

-Tafiti tofauti tofauti zimeweza kutoa taarifa kuwa watu wengi ambao wamekuwa wakifanya mazoezi mepesi hadi ya wastani wameonekana kuwa na uwezekano mdogo mno wa kupata saratan hii.

Saratani ya tezi dume ni moja ya saratani ambayo inatakiwa kutiiliwa maanani miongoni mwa wanaume wengi sana kwa kuzingatia kuwa ni saratani ambayo unaweza kuifanyia uchunguzi wa mapema kabla haijafika mbali na kupata tiba ya mapema. Muda ni sasa onana na daktari kwa uchunguz zaidi.

Share:

GAWA PROGRAMU YAKO YOYOTE YA MAZOEZI KATIKA SEHEMU HIZI KUU TATU (3)

 Ufanyaji wa mazoezi kiholela husababisha watu wengi kujikuta katika matatizo hasa ya kuumia wakati wa mazoezi, kutopata matokeo sahihi na kushindwa kuendelea na mazoezi. Hii hutokana na watu wengi kutofahamu mtiririko sahihi wa programu ya mazoezi na umuhimu wake katika kupata matokeo bora,kwa kufuata mtiririko huu utafurahia mazoezi yako;

1. Pasha mwili kwanza

-Umakini katika mazoezi ni pamoja na kuuandaa mwili wako kwa kufanya mazoezi mepesi kwa angalau dk 5 mpaka 10. 

-Hii hupunguza uwezekano wa kujiumiza kipindi cha mazoezi yenyewe lakini pia husaidia kuuandaa mwili kufanya mazoezi makubwa zaidi.

-Kipengele hiki husahaulika na wafanya mazoezi wengi sana na kujikuta wanakimbilia mazoezi makubwa bila ya kupasha mwili.

2. Anza kufanya mazoezi husika

-Hapa ndio watu wengi hupenda kukimbilia huku wakiwa wameruka hatua ya kwanza juu. Ni muhimu sana katika kipengele hiki kufanya mazoezi ya aina tofautitofauti ili kunogesha na kufurahia mazoezi

-Mazoezi haya tofauti tofauti ni pamoja na;

  • Mazoezi ya nguvu na ustahimilivu wa misuli.
-Haya ni mazoezi pendwa na watu wengi wanaoenda gym ingawa si lazima uwe gym ili uweze kufanya mazoezi haya.

-Ni mazoezi ambayo unaweza kuyafanya kwa kutumia uzito wa mwili wako kama pushaps, kutumia vyuma (kilo 5, 10, 20 n.k), kutumia mashine au kamba zenye ukinzani.

-Mazoezi yanayohusisha misuli mingi hushauriwa zaidi kama vile (squats, deadlift, press n.k) kwani ni mazuri kwa malengo haya.

-Fanya mazoezi haya angalau mara 2-3 kwa wiki

  • Mazoezi ya aerobiki
-Haya huimarisha moyo, mishipa ya damu na mapafu, mifano ni pamoja na kukimbia kwenye treadmill, kuogelea, kukimbia pembezoni mwa barabara

-Ni vizuri kubadilisha mazoezi haya ili kupunguza athari zitokanazo na kurudiarudia mazoezi.

  • Mazoezi ya unyumbufu
-Mazoezi haya hupanua wigo wa mwili kubadilikabadilika kwani huusisha maungio na uvutajiwa misuli.

-Mazoezi haya ni vizuri kuyafanya mwishoni mwa mazoezi ya juu kwani maungio na misuli vinakuwa tayari vimepashwa sana.

3. Poza mwili wako 

-Baada ya mazoezi ya muda mrefu, mwili inatakiwa upoe kwa kushusha mapigo ya moyo mpaka kiwango cha kawaida (60-100 kwa dk 1) na jasho kuacha kutoka tena. 

-Hii ni hatua ya mwisho katika kipindi cha mazoezi ambayo hufanyika kwa kupunguza kasi na uzito wa mazoezi taratibu taratibu hadi mwili unapoa kabisa. Hii husaidia mwili kujisikia vizuri na hivyo kuendelea na mazoezi siku nyingine. 

Mwili ukishapoa basi unaweza kupata nafasi ya kuoga, kunywa maji ya kutosha na chakula safi kabisa na kisha kupata mapumziko kwa siku inayofuata. Mtiririko huu wa mazoezi ni mzuri, salama na wenye mashiko kiafya kwani hukupatia matokeo ya uhakika.

Share:

MAMBO SABA (7) MUHIMU YA KUFANYIA UCHUNGUZI KWENYE KLINIKI YA WAGONJWA WA KISUKARI

Mifumo mbalimbali huweza kuathiriwa na ugonjwa wa kisukari endapo kiwango cha sukari hakitaweza kudhibitiwa vizuri katika damu, huku mifumo mingine huweza kuathiriwa kutokana na usugu wa ugonjwa huu. Hivyo uchunguzi ni muhimu katika kuzuia madhara yasitokee au yaliyotokea yasiendelee, kwa kufanya mambo haya kutakuwa na mchango mkubwa kwa afya yako;

1. Kupima kipimo kiitwacho "HbA1C"

-Kipimo hiki hutumia sampuli ya damu ili kuangalia kiwango cha "HbA1C" ambacho hutoa picha ya ujumla ya udhibiti wa sukari katika mwili kwa muda wa miezi mitatu (3) iliyopita.

-Endapo kiwango hiki kitatoa taswira ya udhibiti hafifu wa sukari basi hapo mgonjwa atakuwa kwenye nafasi ya kuongeza jitihada kudhibiti sukari na kuchukua tahadhari mbalimbali.

-Jadiliana na daktari na uweza kufanyiwa kipimo hiki.  

2. Uchunguzi wa miguu

-Kutokana na athari ya sukari kwenye mishipa ya damu na fahamu hasa katika miguu ingawa hata mikono huweza kuathirika. Hali hii inaweza kupelekea kutokea kwa vidonda sugu kwenye miguu 

-Onana na mtaalamu angalau mara moja kwa mwaka kwa ajili ya kuchunguzwa  wa kina wa maendeleo ya miguu yako.

3. Uchunguzi wa figo

-Ni muhimu kuonana na daktari kwa ajili ya uchunguzi wa ufanyaji kazi wa figo zako kupitia vipimo mbalimbali. 

-Figo ni moja ya viungo vya mwili ambavyo huathiriwa sana na kisukari na inaweza kupunguza ufanisi wa figo kuchuja damu.

-Kama una ugonjwa wa kisukari kwa miaka mitano (5) au zaidi ni vyema kuonana na daktari kila mwaka kwa uchunguzi.

4. Uchunguzi wa macho

-Inashauriwa angalau kila mwaka kuonana na daktari wa macho kwa ajili ya uchunguzi wa macho kwani sukari ya juu sana katika damu kwa muda mrefu huweza kupelekea madhara katika macho na hivyo kusababisha upofu.

5. Upimaji wa shinikizo la damu(presha)

-Kisukari ni moja ya ugonjwa hatari kwa mtu kupata tatizo la shinikizo la juu la damu ambapo kwa pamoja matatizo haya huweza kuleta athari kubwa zaidi mwilini.

-Inashauriwa kupima shinikizo la damu kila baada ya miezi mitatu (3) kwenye kituo cha afya au hospitali.

6. Upimaji wa mafuta mwilini.

-Mgonjwa wa kisukari anakuwa kwenye uhatari wa kuwa na mafuta mengi mwilini hasa lehemu mbaya (LDL) ambapo inakuwa ni hatari kwa afya ya moyo, ubongo, figo n.k

-Hivyo ni vyema kuonana na mtaalamu wa afya angalau kila baada ya miaka 3 hadi 5 endapo mafuta yako kiwango cha kawaida katika damu au kila mwaka endapo mafuta ni mengi.

7. Uchunguzi wa afya ya akili. 

-Magonjwa sugu kama ya kisukari na mengine mara nyingi huathiri wagonjwa kiakili kama vile sonona hasa wakifikiria msaada wa kifedha wa matibabu, matumizi ya dawa kwa muda mrefu, udhibiti imara wa sukari mwilini n.k

-Kuonana na mtaalamu wa afya ya akili kwa ajili ya tathmini ya afya yako kwa jumla ni suala muhimu sana.

Ugonjwa wa kisukari unahitaji ufuatiliaji wa karibu sana na sana ili kuweza kuishi maisha yenye ubora na kuepuka misukosuko ya kwenda hospitali mara kwa mara. Kikubwa ni kujitahidi kuonana na daktari wako katika kliniki bila ya kukosa ili kupata tiba stahiki

Share:

MADHARA KUMI NA TATU (13) YA TATIZO LA KIHARUSI (STROKE) KWA MGONJWA.

 Mtu aliyepatwa na tatizo la kiharusi anaweza kuibukiwa na madhara mengi sana katika mwili na madhara haya huzidisha udhaifu wa afya ya mgonjwa na hutoa taswira mbaya ya maendeleo ya mgonjwa. Kiharusi huathiri takribani mifumo yote mwilini na kusababisha madhara kama ifuatavyo;

1.Maambukizi katika mapafu

-Nimonia ni ugonjwa wa maambukizi ya mapafu (kutokana na bakteria au virusi) ambao huathiri wagonjwa wengi wenye tatizo la kiharusi .

-Mara nyingi ugonjwa huu huwapata ndani ya masaa 48 tangu apate tatizo la kiharusi kutokana na  kupaliwa na chakula au matapishi katika mfumo wa hewa. 

2. Shida (Ugumu) ya kumeza chakula

-Moja ya matokeo ya kiharusi ni pamoja na kuweza kudhoofisha misuli ya kusaidia umezaji wa chakula. Halii hupelekea mgonjwa kushindwa kumeza chakula vizuri na huweza kuchangia katika kupaliwa pia

-Hivyo ni muhimu kumjaribisha mgonjwa uwezo wake wa kumeza vyakula au vimiminika kabla ya kuendelea na ulishaji wa kawaida.

3. Shambulizi la moyo

-Kiharusi huweza kupelekea madhara kwenye moyo kwa kuathiri mfumo wa umeme kwenye moyo au kuathiri mishipa ya damu kwenye moyo na kusababisha shambulizi la moyo

-Madhara haya huchangiwa na mambo kadhaa kwa mtu mwenye kiharusi ikiwemo mabonge ya damu katika mishipa ya damu.

4. Damu kuganda katika mishipa 

-Tatizo la kiharusi huweza kumpelekea mgonjwa kukaa kitandani kwa muda mrefu sana, hii hupunguza msukumo wa damu katika mishipa na hivyo damu kuanza kutengeneza mabonge mabonge hasa katika mishipa iitwayo veini. Mgonjwa huanza kupata dalili za miguu kuvimba na kuuma 

-Hali hi ni hatari sana kwani mabonge haya ya damu huweza kuziba mishipa ya damu kwenye mapafu na ubongo na kusababisha kifo cha ghafla.

-Inashauri mgonjwa kufanyiwa mazoezi mapema inasaidia katika kuzuia hali hii kutokea na wagonjwa wengine hupewa dawa kabisa za kuzuia hali hii isitokee.

5. Maambukizi ya njia ya mkojo

-Takribani 15% ya wagonjwa wenye kiharusi wana uwezekano wa kupata maambukizi haya katika miezi mitatu (3) ya mwanzo.

-Maambukizi haya huchangiwa na matumizi ya mpira wa mkojo kwa muda mrefu na hii hupelekea vimelea vya magonjwa hasa bakteria kupanda kwenye mfumo wa mkojo

 -Kwa maana hiyo si vema mgonjwa akakaa na mpira wa kukojelea zaidi ya siku 14 bila ya kubadilishiwa.

6. Kushindwa kuzui mkojo (kujikojolea)

-Inapotekea tatizo hili kuathiri misuli ya kibofu cha mkojo basi mgonjwa hujikuta akishindwa kuzuia mkojo unapojaa au kumbana na hivyo kujikojolea

-Hii ni ishara ambayo si nzuri kwa maendeleo ya kiafya ya mgonjwa mwenye kiharusi.

7. Matatizo katika tendo la ndoa

-Matatizo makubwa ya tendo la ndoa ni pamoja na; kukosa hamu ya tendo la ndoa, kushindwa kumwaga mbegu za kiume na kushindwa kusimamisha uume wakati wa tendo la ndoa

-Mabadiliko katika uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa wagonjwa wenye tatizo la kiharusi hutokana na  sababu mbalimbali zikiwepo;

  • Uoga wa shambulio jingine la kiharusi
  • Madhara ya baadhi ya madawa anazotumia katika tatizo la kiharusi
  • Ulemavu wa aina yoyote alioupata mtu kutokana na kiharusi
  • Kupoteza uwezo wa kuhisi au utambuzi
8. Vidonda vya tumbo

-Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula huathiri kipindi cha shambulizi la tatizo hili kiasi cha kwamba kuta za tumbo na utumbo huchimbika na kuanza kusababisha vidonda ambavyo huwa na maumivu makali sana tumboni na hata damu kuvuja katika mfumo wa chakula (kutapika damu, kujisaidia damu haja kubwa)
-Na hii ndio sababu ya wagonjwa wenye kiharusi kupewa dawa kwa ajili ya kuzuia hali hii kutotokea.
9. Mifupa kuvunjika
-Kitendo cha mgonjwa mwenye kiharusi kukaa kitandani kwa muda mrefu kutokana na kupooza kwa viungo vya mwili husababisha mifupa kupoteza uimara wao na hivyo kuwa katika uhatari wa kuvunjika kwa urahis sana hasa ya upande uliopooza.

10. Vidonda kwenye ngozi
-Kiharusi hupelekea wagonjwa wengi kushindwa kutembea na kubaki wameshinda kwenye vitanda kwa muda mrefu. 
-Hali hii hupelekea kutokwa na vidonda kwenye ngozi hasa sehemu za matakoni, mgongoni, kwenye nyonga, visiginoni n.k, pia wale wanaotumia viti vya matairi nao huathirika na tatizo hili. 
11. Kukakamaa kwa maungio 
-Hii ni changamoto nyingine kubwa ambayo inatokea kutokana na wagonjwa hawa kukaa muda mrefu kitandani bila ya kuchezeshwa kwa maungio yao ya kwenye mikono na miguu.
-Hali hii hupelekea maungio haya kuanza kukaza na kushindwa kufanya kazi kama mwanzo. Hapa ndio umuhimu wa tiba mazoezi ya mapema huanza kuonekana.
12. Sonona
-Ugonjwa huu wa akili huweza kuwapata wagonjwa hawa wenye kiharusi kutokana na wasiwasi wao wa hali ya afya kama ulemavu wa viungo, kujikojolea na kukosa hamu ya tendo la ndoa n.k
-Hali hii huchangia matatizo mengine zaidi na zaidi kuendelea kuibuka kwa mgonjwa huu na kuwa na matarajio yasiyoridhisha kwa mgonjwa. 
13. Kifo 
-Tatizo la kiharusi limekuwa likichangia kwa kiasi kikubwa ulemavu na maradhi mbalimbali kwa wagonjwa. Madhara haya ya kiharusi ndio huchangia kuongezeka kwa vifo vya wagonjwa hawa. Hivyo huduma bora ya kiafya kwa wagonjwa hawa huwasaidia kuongeza ubora wa maisha yao na hivyo kuongeza muda wa kuishi.

Kumuhudumia mgonjwa mwenye kiharusi ni jukumu la wataalamu wa kada mbalimbali za afya pamoja na familia kuanzia mgonjwa anapokuwa hospitalini hadi anaporuhusiwa kwenda nyumbani.
Matatizo ya kiharusi ni lazima yapewe uzito katika kipindi chote cha matatibu ya mgonjwa kwani ndio yamekuwa chanzo cha vifo vya wagonjwa hawa.
Share:

MATOKEO MATANO (5) YANAYOKUFANYA UWE FITI KATIKA PROGRAMU YAKO YA MAZOEZI

 Si kila anayefanya mazoezi anakuwa fiti la hasah! Na hii inatokana na watu wengi hufanya mazoezi pasipokujua aina gani ya mazoezi wanafanya, umuhimu wake, wakati gani yafanyike, na kwa namna gani. Unapofanya mazoezi mara zote lenga kufanikiwa katika mambo haya kwani ndio vipimo vya uimara wako katika mazoezi.

1. Wepesi wa mwili

-Haijalishi ukubwa wa mwili, jinsi au umri mazoezi hutakiwa kuufanya mwili kuwa na uwezo wa kunyumbuka au kubadilika haraka sana na kwa usahihi katika uelekeo wowote . 

-Wepesi si kuwa na uzito mdogo bali ni uwezo uliojengeka kutokana na mazoezi.

2. Uwezo wa kufanya kazi(shughuli).

-Mazoezi hutakiwa kukupatia uwezo wa kufanya kazi kubwa ndani ya muda mfupi yani kazi ya saa 1 unaweza kuifanya dk 20. Hii inaletwa kutokana na ukomavu wa mifumo ya moyo, upumuaji na mishipa ya damu kutokana na mazoezi

-Matokeo haya huleta mtazamo mzuri sana wa mtu kuwa fiti.

3. Msawazo wa mwili

-Mwili kuwa katika hali ya usawa kuanzia juu hadi chini humfanya mtu kuwa fiti kwani anakuwa na uwiano mzuri wakati wa kusimama au wakati wa kutembea.

-Matokeo haya hukufanya pia kuwa bora katika aina zingeine za mazoezi kama ya aerobiki, ya nguvu za misuli na ya unyumbufu wa mwili.

4. Uwezo wa kuutawala mwili

-Mfanya mazoezi hujengeka vizuri katika mazoezi kwa kupata uwezo wa kutumia milango ya fahamu kama macho,ngozi, masikio n.k katika kufanya kazi zake kirahisi na kwa usahihi.

-Mazoezi yanajenga akili kufanya mambo kwa usahihi na hii inaweza kukuepusha na  kuepukana na athari.

5. Uharaka kwenye muitiko

-Moja ya sifa kubwa jeshini ni pamoja na kuitikia haraka kwenye jambo au kitu chochote kutoka katika mazingira ya nje.

-Mazoezi yenye tija yatakupatia uwezo huu kwani yatakusaidia katika shughuli za kila siku na hata kukuepusha na mazingira hatari.

Kama umekuwa ukifanya mazoezi bila ya kupata matokeo tajwa hapo juu basi jua kuwa kuna sehemu unakosea. Ni bora kupata mkufunzi wa mazoezi atakayekusaidia kupata matokeo sahihi katika programu yako.

Share:

UWEZEKANO WA KUPATWA NA VIDONDA SUGU VYA MIGUU KUTOKANA NA UGONJWA WA KISUKARI HUCHANGIWA NA MAMBO HAYA

 Ugonjwa wa kisukari ndio huongoza kwa kupelekea watu wengi kupoteza viungo vyao hasa vidole na miguu kwa kukatwa. Hii hutokana na madhara ya muda mrefu ya ugonjwa wa kisukari ikiwemo kuharibika kwa mishipa ya fahamu na damu shemu za miguu. Athari ya sukari mwilini huchangia katika kuchelewa kupona kwa vidonda na hivyo kuleta usugu huu hali hii ikichochewa zaidi na mambo haya;

1. Kuwa na ugonjwa wa kisukari kwa zaidi ya miaka 10

- Tafiti zimeonesha kuwa uwezekano wa kupatwa na tatizo la vidonda sugu vya miguu huendana sambamba na muda wa ugonjwa wa kisukari tangu kugundulika.

-Kama moja ya madhara ya kisukari hutokea mara baada ya muda mrefu wa ugonjwa huu.

2. Udhibiti hafifu wa kiwango cha sukari katika damu.

-Athari ya ugonjwa wa kisukari katika mwili ni sambamba na uwepo wa kiwango cha juu cha sukari kwenye damu kwa muda mrefu. Hii hupelekea sukari kuathiri mishipa ya damu na mishipa ya fahamu taratibu na kuongeza uhatari katika mguu 

3.Ganzi kali katika miguu.

-Hali hii ya ganzi kali humfanya mtu kupunguza uwezo wa kuhisi maumivu endapo atajikwaa au kujiumiza.

-Pia huweza kupelekea kukauka kwa miguu na hivyo kujenga nyufa kirahisi kwa vimelea kupita

4.Uvutaji wa sigara.

-Kuna uhusiano wa sigara na  mishipa ya damu kutokana na ukweli kuwa sigara huathiri mishipa ya famahu na ya damu.Athari hii hupelekea mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri kwenda kwenye miguu na hivyo kusababisha vidonda kwa kwa miguu kukosa damu.

-Lakini pia sigara hupelekea kuchelewa kupona kwa vidonda vya kisukari.

5.Mabadiliko ya maumbile ya miguu.

-Kutokana na maradhi ya mishipa ya fahamu, mguu huu huwa na vidole vilivyopinda, kutanuka kwa miguu n.k, mabadiliko haya yote yamehusihwa na kupata vidonda.

6. Uonaji hafifu wa macho.

-Hali hii inaweza ikawa inatokana na ugonjwa wa kisukari wenyewe au ugonjwa mwingine na kusababisha kujiumiza kwa kujigonga sehemu za miguu na kupelekea kidonda.

7. Historia ya kidonda katika mguu au kukatwa kwa kidole au mguu.

-Mambo haya yote huchangia kwa uwezekano mkubwa wa kupatwa na vidonda sugu kwa baadae endapo mambo mengine hayatazingatiwa katika kudhibiti ugonjwa huu.

Utambuzi na matatibabu ya mapema ya ugonjwa wa kisukari husaidia katika kupunguza madhara ya muda mrefu na kisha kuboresha maisha ya mgonjwa.



Share:

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.