Ufanyaji wa mazoezi kiholela husababisha watu wengi kujikuta katika matatizo hasa ya kuumia wakati wa mazoezi, kutopata matokeo sahihi na kushindwa kuendelea na mazoezi. Hii hutokana na watu wengi kutofahamu mtiririko sahihi wa programu ya mazoezi na umuhimu wake katika kupata matokeo bora,kwa kufuata mtiririko huu utafurahia mazoezi yako;
1. Pasha mwili kwanza
-Umakini katika mazoezi ni pamoja na kuuandaa mwili wako kwa kufanya mazoezi mepesi kwa angalau dk 5 mpaka 10.
-Hii hupunguza uwezekano wa kujiumiza kipindi cha mazoezi yenyewe lakini pia husaidia kuuandaa mwili kufanya mazoezi makubwa zaidi.
-Kipengele hiki husahaulika na wafanya mazoezi wengi sana na kujikuta wanakimbilia mazoezi makubwa bila ya kupasha mwili.
2. Anza kufanya mazoezi husika-Hapa ndio watu wengi hupenda kukimbilia huku wakiwa wameruka hatua ya kwanza juu. Ni muhimu sana katika kipengele hiki kufanya mazoezi ya aina tofautitofauti ili kunogesha na kufurahia mazoezi
-Mazoezi haya tofauti tofauti ni pamoja na;
- Mazoezi ya nguvu na ustahimilivu wa misuli.
-Ni mazoezi ambayo unaweza kuyafanya kwa kutumia uzito wa mwili wako kama pushaps, kutumia vyuma (kilo 5, 10, 20 n.k), kutumia mashine au kamba zenye ukinzani.
-Mazoezi yanayohusisha misuli mingi hushauriwa zaidi kama vile (squats, deadlift, press n.k) kwani ni mazuri kwa malengo haya.
-Fanya mazoezi haya angalau mara 2-3 kwa wiki
- Mazoezi ya aerobiki
-Ni vizuri kubadilisha mazoezi haya ili kupunguza athari zitokanazo na kurudiarudia mazoezi.
- Mazoezi ya unyumbufu
-Mazoezi haya ni vizuri kuyafanya mwishoni mwa mazoezi ya juu kwani maungio na misuli vinakuwa tayari vimepashwa sana.
3. Poza mwili wako
-Baada ya mazoezi ya muda mrefu, mwili inatakiwa upoe kwa kushusha mapigo ya moyo mpaka kiwango cha kawaida (60-100 kwa dk 1) na jasho kuacha kutoka tena.
-Hii ni hatua ya mwisho katika kipindi cha mazoezi ambayo hufanyika kwa kupunguza kasi na uzito wa mazoezi taratibu taratibu hadi mwili unapoa kabisa. Hii husaidia mwili kujisikia vizuri na hivyo kuendelea na mazoezi siku nyingine.
Mwili ukishapoa basi unaweza kupata nafasi ya kuoga, kunywa maji ya kutosha na chakula safi kabisa na kisha kupata mapumziko kwa siku inayofuata. Mtiririko huu wa mazoezi ni mzuri, salama na wenye mashiko kiafya kwani hukupatia matokeo ya uhakika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni