Ugonjwa wa kisukari ndio huongoza kwa kupelekea watu wengi kupoteza viungo vyao hasa vidole na miguu kwa kukatwa. Hii hutokana na madhara ya muda mrefu ya ugonjwa wa kisukari ikiwemo kuharibika kwa mishipa ya fahamu na damu shemu za miguu. Athari ya sukari mwilini huchangia katika kuchelewa kupona kwa vidonda na hivyo kuleta usugu huu hali hii ikichochewa zaidi na mambo haya;
1. Kuwa na ugonjwa wa kisukari kwa zaidi ya miaka 10
- Tafiti zimeonesha kuwa uwezekano wa kupatwa na tatizo la vidonda sugu vya miguu huendana sambamba na muda wa ugonjwa wa kisukari tangu kugundulika.
-Kama moja ya madhara ya kisukari hutokea mara baada ya muda mrefu wa ugonjwa huu.
2. Udhibiti hafifu wa kiwango cha sukari katika damu.
-Athari ya ugonjwa wa kisukari katika mwili ni sambamba na uwepo wa kiwango cha juu cha sukari kwenye damu kwa muda mrefu. Hii hupelekea sukari kuathiri mishipa ya damu na mishipa ya fahamu taratibu na kuongeza uhatari katika mguu
3.Ganzi kali katika miguu.
-Hali hii ya ganzi kali humfanya mtu kupunguza uwezo wa kuhisi maumivu endapo atajikwaa au kujiumiza.
-Pia huweza kupelekea kukauka kwa miguu na hivyo kujenga nyufa kirahisi kwa vimelea kupita
4.Uvutaji wa sigara.
-Kuna uhusiano wa sigara na mishipa ya damu kutokana na ukweli kuwa sigara huathiri mishipa ya famahu na ya damu.Athari hii hupelekea mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri kwenda kwenye miguu na hivyo kusababisha vidonda kwa kwa miguu kukosa damu.
-Lakini pia sigara hupelekea kuchelewa kupona kwa vidonda vya kisukari.
5.Mabadiliko ya maumbile ya miguu.
-Kutokana na maradhi ya mishipa ya fahamu, mguu huu huwa na vidole vilivyopinda, kutanuka kwa miguu n.k, mabadiliko haya yote yamehusihwa na kupata vidonda.
6. Uonaji hafifu wa macho.
-Hali hii inaweza ikawa inatokana na ugonjwa wa kisukari wenyewe au ugonjwa mwingine na kusababisha kujiumiza kwa kujigonga sehemu za miguu na kupelekea kidonda.
7. Historia ya kidonda katika mguu au kukatwa kwa kidole au mguu.
-Mambo haya yote huchangia kwa uwezekano mkubwa wa kupatwa na vidonda sugu kwa baadae endapo mambo mengine hayatazingatiwa katika kudhibiti ugonjwa huu.
Utambuzi na matatibabu ya mapema ya ugonjwa wa kisukari husaidia katika kupunguza madhara ya muda mrefu na kisha kuboresha maisha ya mgonjwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni