Mtu aliyepatwa na tatizo la kiharusi anaweza kuibukiwa na madhara mengi sana katika mwili na madhara haya huzidisha udhaifu wa afya ya mgonjwa na hutoa taswira mbaya ya maendeleo ya mgonjwa. Kiharusi huathiri takribani mifumo yote mwilini na kusababisha madhara kama ifuatavyo;
1.Maambukizi katika mapafu
-Nimonia ni ugonjwa wa maambukizi ya mapafu (kutokana na bakteria au virusi) ambao huathiri wagonjwa wengi wenye tatizo la kiharusi .
-Mara nyingi ugonjwa huu huwapata ndani ya masaa 48 tangu apate tatizo la kiharusi kutokana na kupaliwa na chakula au matapishi katika mfumo wa hewa.
2. Shida (Ugumu) ya kumeza chakula
-Moja ya matokeo ya kiharusi ni pamoja na kuweza kudhoofisha misuli ya kusaidia umezaji wa chakula. Halii hupelekea mgonjwa kushindwa kumeza chakula vizuri na huweza kuchangia katika kupaliwa pia
-Hivyo ni muhimu kumjaribisha mgonjwa uwezo wake wa kumeza vyakula au vimiminika kabla ya kuendelea na ulishaji wa kawaida.
3. Shambulizi la moyo-Kiharusi huweza kupelekea madhara kwenye moyo kwa kuathiri mfumo wa umeme kwenye moyo au kuathiri mishipa ya damu kwenye moyo na kusababisha shambulizi la moyo
-Madhara haya huchangiwa na mambo kadhaa kwa mtu mwenye kiharusi ikiwemo mabonge ya damu katika mishipa ya damu.
4. Damu kuganda katika mishipa-Tatizo la kiharusi huweza kumpelekea mgonjwa kukaa kitandani kwa muda mrefu sana, hii hupunguza msukumo wa damu katika mishipa na hivyo damu kuanza kutengeneza mabonge mabonge hasa katika mishipa iitwayo veini. Mgonjwa huanza kupata dalili za miguu kuvimba na kuuma
-Hali hi ni hatari sana kwani mabonge haya ya damu huweza kuziba mishipa ya damu kwenye mapafu na ubongo na kusababisha kifo cha ghafla.
-Inashauri mgonjwa kufanyiwa mazoezi mapema inasaidia katika kuzuia hali hii kutokea na wagonjwa wengine hupewa dawa kabisa za kuzuia hali hii isitokee.
5. Maambukizi ya njia ya mkojo
-Takribani 15% ya wagonjwa wenye kiharusi wana uwezekano wa kupata maambukizi haya katika miezi mitatu (3) ya mwanzo.
-Maambukizi haya huchangiwa na matumizi ya mpira wa mkojo kwa muda mrefu na hii hupelekea vimelea vya magonjwa hasa bakteria kupanda kwenye mfumo wa mkojo
-Kwa maana hiyo si vema mgonjwa akakaa na mpira wa kukojelea zaidi ya siku 14 bila ya kubadilishiwa.
6. Kushindwa kuzui mkojo (kujikojolea)-Inapotekea tatizo hili kuathiri misuli ya kibofu cha mkojo basi mgonjwa hujikuta akishindwa kuzuia mkojo unapojaa au kumbana na hivyo kujikojolea
-Hii ni ishara ambayo si nzuri kwa maendeleo ya kiafya ya mgonjwa mwenye kiharusi.
7. Matatizo katika tendo la ndoa-Matatizo makubwa ya tendo la ndoa ni pamoja na; kukosa hamu ya tendo la ndoa, kushindwa kumwaga mbegu za kiume na kushindwa kusimamisha uume wakati wa tendo la ndoa
-Mabadiliko katika uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa wagonjwa wenye tatizo la kiharusi hutokana na sababu mbalimbali zikiwepo;
- Uoga wa shambulio jingine la kiharusi
- Madhara ya baadhi ya madawa anazotumia katika tatizo la kiharusi
- Ulemavu wa aina yoyote alioupata mtu kutokana na kiharusi
- Kupoteza uwezo wa kuhisi au utambuzi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni