Si kila anayefanya mazoezi anakuwa fiti la hasah! Na hii inatokana na watu wengi hufanya mazoezi pasipokujua aina gani ya mazoezi wanafanya, umuhimu wake, wakati gani yafanyike, na kwa namna gani. Unapofanya mazoezi mara zote lenga kufanikiwa katika mambo haya kwani ndio vipimo vya uimara wako katika mazoezi.
1. Wepesi wa mwili
-Haijalishi ukubwa wa mwili, jinsi au umri mazoezi hutakiwa kuufanya mwili kuwa na uwezo wa kunyumbuka au kubadilika haraka sana na kwa usahihi katika uelekeo wowote .
-Wepesi si kuwa na uzito mdogo bali ni uwezo uliojengeka kutokana na mazoezi.
2. Uwezo wa kufanya kazi(shughuli).
-Mazoezi hutakiwa kukupatia uwezo wa kufanya kazi kubwa ndani ya muda mfupi yani kazi ya saa 1 unaweza kuifanya dk 20. Hii inaletwa kutokana na ukomavu wa mifumo ya moyo, upumuaji na mishipa ya damu kutokana na mazoezi
-Matokeo haya huleta mtazamo mzuri sana wa mtu kuwa fiti.
3. Msawazo wa mwili
-Mwili kuwa katika hali ya usawa kuanzia juu hadi chini humfanya mtu kuwa fiti kwani anakuwa na uwiano mzuri wakati wa kusimama au wakati wa kutembea.
-Matokeo haya hukufanya pia kuwa bora katika aina zingeine za mazoezi kama ya aerobiki, ya nguvu za misuli na ya unyumbufu wa mwili.
4. Uwezo wa kuutawala mwili
-Mfanya mazoezi hujengeka vizuri katika mazoezi kwa kupata uwezo wa kutumia milango ya fahamu kama macho,ngozi, masikio n.k katika kufanya kazi zake kirahisi na kwa usahihi.
-Mazoezi yanajenga akili kufanya mambo kwa usahihi na hii inaweza kukuepusha na kuepukana na athari.
5. Uharaka kwenye muitiko
-Moja ya sifa kubwa jeshini ni pamoja na kuitikia haraka kwenye jambo au kitu chochote kutoka katika mazingira ya nje.
-Mazoezi yenye tija yatakupatia uwezo huu kwani yatakusaidia katika shughuli za kila siku na hata kukuepusha na mazingira hatari.
Kama umekuwa ukifanya mazoezi bila ya kupata matokeo tajwa hapo juu basi jua kuwa kuna sehemu unakosea. Ni bora kupata mkufunzi wa mazoezi atakayekusaidia kupata matokeo sahihi katika programu yako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni