MBINU 14 ZITAKAZOKUFANYA UENDELEE KUFANYA MAZOEZI BILA YA KUACHA

Moja ya changamoto kubwa sana ya mtu anayeanza mazoezi ni kukata tamaa na kushindwa kuendelea kufikia malengo yake. Hii inachangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa muda, kukosa hamasa n.k.

Ili kupata matokeo mazuri ya mazoezi ni vizuri kuwa na mahudhurio ya mazoezi yaliyonyooka, kwa kuzingatia haya yafutayo unaweza kuwa katika mstari mzuri wa mazoezi bila ya kuacha.

1. Gawa muda wako wa mazoezi katika sehemu ndogo ndogo

-Inaweza kuwa ngumu kwa mtu kufanya mazoezi ya wastani kwa dk 30 ndani ya kipindi kimoja hasa wanaoanza au ambao wanaenda kazini.

-Dk 30 unaweza kuigawa katika dk 10 mara tatu katika siku nzima ili kupata nafasi ya kuzoea tararibu mazoezi yako mpaka utakapoweza kufanya dk 30 kwa pamoja.

 2. Anza kufanya mazoezi mepesi kama ni mgeni

-Kama ndio unaanza programu ya mazoezi basi anza mazoezi mepesi taratibu ili kuuzoesha mwili kwani kuanzia mazoezi magumu huongeza uwezekano wa kujiumiza mwili siku za mwanzoni hivyo kushindwa kuendelea na mazoezi siku za mbeleni.

3. Fanya mazoezi siku za wikiendi

-Hakuna haja ya kuweza visingizio ili tu usifanye mazoezi. Kufanya mazoezi wikiendi inashauriwa sana kwa watu ambao ni wafanyakazi kwani siku hizi wengi wao hawaendi kazini.

4. Tafuta rafiki wa kufanya nae mazoezi

-Kufanya mazoezi peke yako kunaweza kukufanya ukata tamaa mapema au kupoteza hamu/morale ya mazoezi haraka.

-Rafiki ni muhimu sana kwani atakupa hamasa na matumaini ya kuendelea kufanya mazoezi.

-Tafuta rafiki mwenye malengo sawa na mpange ratiba kwa pamoja.

5. Jiunge na jimu (gym) iliyo karibu yako.

-Mbali na gym kuwa sehemu rafiki kwa kufanya mazoezi(kwasabbu ya uwepo wa vifaa mbalimbali na eneo la kutosha) pia gym husaidia kukukutanisha na watu tofauti tofauti wenye malengo sawa. 

-Hii husaidia sana katika kupeana hamasa ya kutoacha mazoezi kuliko ukiwa mwenyewe

6. Fanya mzaoezi hata nyumbani.

-Kukosa muda wa kwenda gym sio kigezo cha kutofanya mazoezi na mazoezi si kwenda gym tu. 

-Unaweza kufanya mazoezi hata nyumbani kuokoa muda utakoutumia kwenda gym. Siku hizi kuna vifaa ambavyo unaweza kuvitumia ukiwa nyumbani na ukawa fiti vilevile.

7. Fanya mazoezi pamoja na mkufunzi wa mazoezi

-Kufanya mazoezi bila ya kujua kanuni na taratibu za mazoezi inaweza kukupelekea kukosa matokeo unayoyataka na hivyo kukukatisha tamaa mapema ya kuendelea na mazoezi. 

-Mkufunzi anakuwa na utalaamu na uzoefu utakao kusaidia kufikia malengo yako ya mazoezi, pia kukupa hamasa kubwa.

8. Fanya mazoezi tofauti tofauti

-Kufanya zoezi la aina moja kwa muda mrefu kila wakati unapofanya mazoezi inapunguza hamasa na kukufanya usiendelee na mazeozi, hii huchangiwa zaidi na kutofahamu aina mbalimbali za mazoezi.

-Kuchangaza mazoezi ni muhimu na husaidia kukupa morale wa kuendelea kufanya mazoezi.

9. Sikiliza muziki wakati wa mazoezi

-Jiburudishe na muziki wakati wa mazoezi kwani hutoa hamasa sana na hii ndio sababu ambayo imepelekea gym nyingi kuwa na vyanzo vya muziki ndani (redio, televesheni n.k)

-Pia siku hizi vifaa vingi vimetengenezwa ambavyo vitakusaidia kukupa burudani wakati wa mazoezi kama vile simu za mikono, saa zenye muziki, earphones n.k     

10. Weka malengo yako ya mazoezi sehemu inayoonekana.

-Kutimiza malengo yako ya mazoezi kila siku hutia hamasa kubwa sana ya kuendelea kufanya mazoezi.

-Mfano unaweza kubandika malengo yako ukutani-chumbani, kwenye jokofu, kwenye kompyuta yako, kwenye simu, kwenye diary n.k

-Kuna malengo mbalimbali ya mazoezi ikiwepo ya kupunguza uzito, kujenga mwili, kuimarisha afya n.k, usifanye mazoezi bila ya malengo.

11. Fuatilia mafaniko ya mazoezi yako mara kwa mara

-Unapofuatilia mafanikio yako hii inakupa hamasa ya kuweza kuendelea zaidi na zaidi na njia bora ya kufuatilia mafanikio yako ni kuweka kumbukumbu katika vitabu maalum.

-Mfano; -kiasi gani cha uzito unaweza kubeba kwenye benchi

              -Muda gani unatumia kukimbia kilomita 1

              -Kiasi gani cha mafuta nimepunguza n.k 

             -Check presha na mapigo yako ya moyo

12. Shiriki katika matukio (maadhimisho) mbalimbali ya mazoezi.

-Kuna maadhimisho mbalimbali ambayo unaweza kuwa unashiriki mara kwa mara kila mwaka na hivyo kukujengea mazoea ya kufanya mazoezi.

-Mfano wa maadhimisho hayo ni pamoja na; Kilimanjaro Marathon, Heart Day Marathon n.k

13. Jenga tabia ya kujipongeza kila baada ya hatua fulani.

-Moja ya mambo yatakayokupa hamasa ni pamoja na kujipongeza unapotimiza lengo fulani la mzoezi yako.

-Kujipongeza huko kunaweza kuwa kama; kujinunulia nguo unayoipenda baada ya kupunguza uzito fulani, kutembelea mbugani, kununua vitabu unavyopenda n.k

14. Soma habari za watu waliofanikiwa katika mazoezi

-Kufuatilia habari za watu waliofanikiwa katika moja ya malengo yako katika mazoezi ni jambo zuri na linatolia hamasa na kutokata tamaa.

-Hii huonesha kuwa kila kitu kinawezekana endapo utaamua na kuweka jitihada.

-Kupitia mazoezi watu wengi wameweza kufanikiwa kwa kuwa matajiri, na wengine wameingia kwenye tasnia za uigizaji, maonyesho ya fasheni, urembo n,k na kupata pesa nyingi.

Kupata matokeo mazuri ya mazoezi sio suala la siku moja bali ni mchakato wa muda mrefu, hivyo inatakiwa kutokata tamaa na kusonga mbele kila siku. "Watu wengi hawafurahi mazoezi bali wanafurahia matokeo yake"

Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.