UNAHITAJI KUJUA MAMBO KUMI NA MOJA (11) YANAYOWEZA KUPELEKEA KWA UGONJWA WA KISUKARI AINA YA PILI

 Kisukari ni ugonjwa ambao hujidhihirisha kwa kiwango kikubwa cha sukari katika damu kuliko kawaida. Hii inatoakana na hitilafu katika uzalishaji wa homoni ya Insulin katika kongosho au ukinzania wa homoni hii kwenye tishu mbalimbali za mwili. Aina ya pili ya ugonjwa wa kisukari umehusishwa na vihatarishi mbalimbali ambavyo vinaweza kubadilishwa na visivyoweza kubadilishwa. 

1. Kutofanya mazoezi

-Kushindwa kufanya mazoezi ya mwili hupelekea nguvu nyingiya chakula kutotumika na hivyo kuhifadhiwa katika mwili kama mafuta. 

-Mafuta mengi mwilini huongeza ukinzani katika tishu dhidi ya homoni ya Insulini lakini pia mafuta mengi mwili hupelekea ongezeko kubwa la uzito au unene ambavyo huchangia Insulini kushindwa kufanya kazi.

2. Ulaji usio bora

-Ongezeko kubwa la matumizi ya vyakula vyenye sukari nyingi sana hasa juisi za viwandani, soda, biskuiti, pipi, n.k pamoja na mafuta mengi (hasa mafuta kutoka kwa wanyama)

-Kupunguza ulaji wa mboga mboga za majani, matunda na nafaka isiyokobolewa

-Haya yote hupelekea ongezeko la uzito au unene na kuchangia maradhi ya kisukari.

3. Uzito uliopitiliza au unene.

-Matokeo ya kutofanya mazoezi na ulaji usio bora hupelekea uzito uliopitiliza, hii inatokana na mkusanyiko wa mafuta ndani ya mwili hasa kwenye viungo vya ndani (ini, moyo n.k) na chini ya ngozi.

-Mafuta haya huchangia kwa Insulini kushindwa kufanya kazi ya kuchukua virutubisho (sukari) kutoka kwenye damu kwenda tishu za mwili.

4. Uvutaji wa sigara

-Sigara ni kihatarishi kibaya kutoakana na kemikali ambazo si nzuri zinazotoka katika moshi. 

-Sigara huepelelea kupunguza ufanisi wa kazi wa homoni ya insulini na pia huchangia kusambaa kwa mafuta yaliyozidi mwilini. Hali hii huweza kupelekea ugonjwa wa kisukari

5. Madawa 

-Kuna madawa mbalimbali yanayotibu maradhi mengine huweza kukuweka katika mazingira hatarishi ya ugonjwa wa kisukari endapo utayatumia kwa muda mrefu. Mfano wa dawa hizo ni pamoja na steroidi (kama prednisolone n.k)

-Ni vyema kujadiliana na daktari wako dawa mbalimbali unapoandikiwa hospitalini.

6. Kemikali za kwenye mazingira

-Kemikali hizi huweza kuchangia tatizo hili mara baada ya muda mrefu kupita huku mwili ukiwa katika mazingira yenye kemikali hizo.

-Baadhi ya kemikali zinapatikana kwenye maji (arseniki), kemikali za viwanda hasa vya plastiki na kemikali za madawa ya shambani na nyumbani.

7. Kutopata usingizi wa kutosha.

-Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa kuna uhusiano kati ya kutopata muda wa usingizi wa kutosha ambapo ni masaa 6 au chini na matatizo ya kiafya kama unene na ugonjwa wa kisukari.

-Hali hii imeonekana kuchangiwa na mabadiliko mbalimbali ya mwili  kwa mtu anayekosa muda wa kutosha wa usingizi.

-Inashauri kwa mtu mzima kupata angalau masaa 7 ya usingizi huku watoto wakipata muda zaidi.

 8. Magonjwa kadhaa.

-Baadhi ya magonjwa yamekuwa yakichangia kwa kuibuka kwa aina hii ya kisukari mfano ni pamoja na maradhi ya wanawake kutoka na kukosekana kwa uwiano wa homoni (Polycystic Ovarian Syndrome) na hata kisukari cha ujauzito

9. Histori ya ugonjwa wa kisukari katika familia.

-Inapotokea katika familia kuna mzazi au ndungu wa tumbo moja ana ugonjwa wa kisukari, hii inaongeza uwezekano mkubwa kwa ndugu (mzao) mwingine kupata kisukari kwa siku za mbeleni. 

-Hii imehusishwa na mchango wa vinasaba kwa ugonjwa wa kisukari.

10. Umri

- Nafasi ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari aina hii hongezeka kadiri ya umri unavyosonga. Watu wenye umri zaidi ya miaka 45 wako kwenye hatari zaidi. 

-Kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha na ulaji kwa watoto imepelekea vijana wadogo pia kuathiriwa na kisukari aina hii.

11. Asili ya jamii.

-Aina hii ya kisukari imeonekana kuathiri sana watu wenye asili ya afrika, hispania na hata waamerika kuliko watu wenye asili tofauti na hizi.

Ni vizuri kuchukua tahadhari mapema kwa mambo ambayo yako ndani ya uwezo(jambo la 1 hadi 8) kuliko kusubiria mpaka tatizo likukute. Jitahidi kufanya uchunguzi katika vituo vya afya kila baada ya muda fulani endapo utakuwa na vihatarishi vingine.


Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.