MAMBO KUMI NA MOJA (11) YANAYOWEZA KUPELEKEA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

 -Saratani ya shingo ya kizazi ni moja ya saratani inayoathiri wanawake wengi, ikishika nafasi ya tatu (3) duniani na nafasi ya kwanza (1)kuathiri wanawake nchini Tanzania miongoni mwa saratani zote.  Shingo ya kizazi ni mojawapo ya viungo wa uzazi ambayo ni sehemu ya mfuko/tumbo la uzazi inayotokelezea kwenye uke. Seli za eneo hili ziko kwenye uhatari wa kupata mabadiliko hasi yanayoweza kupelekea saratani endapo mambo yafuatayo yataweza kuhusika kwa kipindi fulani katika maisha ya mwanamke, mambo hayo ni pamoja na

1. Maambukizi ya virusi aina ya HPV (Human Papilloma Virus)

-Hiki ni kihatarishi kikubwa sana kwani maambukizi ya muda mrefu ya virusi hivi ndio imehusishwa kwa asilimia 90 kama chanzo cha saratani hii.  Virusi hivi huweza kuvipata kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye maambukizi ya virusi hivi. Kuna aina zaidi ya 100 ya virusi hivi ambapo si wote ni hatarishi kwa saratani hii bali aina ya HPV16 na HPV18 ndio vimehusishwa zaidi.

-Watu wengi wameweza kudhibiti maambukizi haya kutoka na kinga ya mwili kuwa bora lakini inapotokea maambukizi haya yanadumu kwa muda mrefu basi ndio nafasi ya mlango huu wa uzazi unazidi kupata mabadiliko ya saratani.

2.Umri mdogo wa kuanza ngono zembe.

-Tafiti zimeonesha kuwa wagonjwa wengi ambao wanasumbuliwa na saratani ya shingo ya kizazi walianza kujamiiana mapema zaidi (katika umri mdogo) ukilinganisha na kundi jingine. Na hii imeelezwa ni kwasababu shingo ya kizazi katika umri mdogo huwa na ukuta ambao haujakomaa vizuri hivyo kuufanya uweze kuathiriwa kirahisi na virusi hivi.

3. Upungufu wa kinga mwilini

-Mwili kukosa kinga ya kutosha ni tatizo kubwa kwa virusi hivi kwani  hupelekea kuathiri na kushambulia mwili kirahisi. Mambo mablimbali yanayoweza kupelekea upungufu wa kinga mwilini ni pamoja na maradhi kama UKIMWI, saratani zingine, madawa kama steroidi, utapiamlo n.k

4. Kuwa na wapenzi wengi 

-Mwanamke kuwa na wapenzi wengi wa kiume au kuwa na mwenza wa kiume wenye wapenzi wengi ni hatari kwani huongeza nafasi ya kupata saratani hii taratibu kadiri muda unavyokwenda.

5. Historia ya magonjwa ya zinaa

-Magonjwa ya zinaa kama kaswende, kisonono, UKIMWI, n.k yameonekana kuongeza nafasi ya mwanamke kupata saratani kwani maradhi haya yanaweza kuwa njia ya virusi vya HPV kupitia.

6. Uvutaji wa sigara

-Uvutaji wa sigara huchangia kutokea kwa saratani hii kutoka na ukweli kuwa kemikali mbalimbali ambazo ziko kwenye moshi wa sigara si salama na huweza kusababisha mabadiliko katika seli za mwili.

7. Kujifungua mara nyingi (uzao)

-Kujifungua watoto angalau 3 imeonekana kuongeza nafasi ya kupata saratani ya shingo ya uzazi kutokana na eneo hili kufikiwa na homoni ya kike (estrogeni) mara kwa mara , hii inaweza kupelekea mabadiliko katika ukanda wa shingo ya uzazi.                                    

8. Matumizi ya vidonge vya uzazi

-Kutumia vidonge vya uzazi kwa muda mrefu (angalau kwa miaka 5) huweza kupelekea kupata saratani hii huku homoni ya estrogen ambayo ni sehemu ya vidonge hivyo imeonekana kuhusika zaidi kwa kuwa na athari katika mlango wa uzazi huo.

-Athari hii ya vidonde vya uzazi imeonekana kuwa na athari zaidi kwa wale ambao wanakuwa tayari na maambukizi ya virusi vya HPV.

- Hivyo kuzingatia muda wa matumizi ya njia hii ya uzazi ni muhimu sana

9. Historia ya familia ya saratani 

-Tafiti zinaonesha kuwa nafasi ya kupata saratani hii inaongezekana endapo kama mmoja katika familia aidha mama au dada amewahi kupata ukilinganisha na familia ambayo hakuna hata mmoja amewahi kupata ugonjwa huu.

10. Ulaji usio bora

-Imeonekana kuwa kutotumia mboga za majani na matunda katika milo ya kila siku huongeza nafasi ya kupata saratani hii miongoni mwa wanawake wengi.

11. Hali duni ya uchumi

-Kutoka na uchumi mdogo wa watu wengi, hii hupelekea watu kukosa vipimo vya mapema na hivyo saratani kutogundulika katika hatua za awali.

Kigezo hiki cha uchumi ndio kinaepelekea utofauti wa idadi kubwa ya saratani ya shingo ya uzazi kwa nchi zinazoendelea ukilinganisha na nchi za ulaya.

Saratani ya shingo ya kizazi inazuilika na kutibika endapo itangundulika ikiwa katika hatua za awali. Hii itawezekana tu endapo wanawake wengi watafika katika vituo vya afya kwa ajili ya upimaji wa afya zao. Hakuna haja ya kusubiria dalili zote kwani katika hatua za mwanzoni saratani hii inakuwa haina dalili.

Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.