HIZI NDIO SABABU ZA KWANINI ONGEZEKO LA SARATANI KWA UJUMLA NI KUBWA SANA SIKU HIZI

Saratani ni ugonjwa ambao hutokana na hitilafu katika seli za mwili ambapo hupoteza uwezo wao kwa kugawanyika, kujizalisha na kuongezeka bila kikomo na hivyo hupelekea sehemu husika kupata mabadiliko yasiyo ya kawaida.

Seli hizi zenye hitilafu zinaweza kusambaa  kutoka sehemu ya chanzo na kwenda sehemu zingine tofauti za mwili  kupitia tishu za eneo la karibu, njia ya damu au kimiminika kiitwacho " lymph".

Saratani inaweza kutokea sehemu mbalimbali za mwili kama tezi dume, mapafu, shingo la uzazi, matiti, koo, n.k

Zaidi ya watu milioni 14 duniani huathirika na saratani na waathirika zaidi ya milioni 8 hupoteza maisha.

Saratani imekuwa ni tatizo kubwa sana kwa sasa kutoka na ongezeko la vihatarishi vinavyoweza kubadilika ukiachia pembeni sababu za vinasaba, vihatarishi hivyo ni;

1. Uvutaji wa tumbaku/sigara

Matumizi ya tumbaku na sigara yameongezekana sana miongoni wa watu (vijana na watu wazima). Utumiaji wa tumbaku/ sigara huchangia kwa saratani nyingi zikiwemo za mapafu, tezi dume, shingo la uzazi, koo, tumbo n.k

Hii inatokana na kuwa moshi wa sigara una zaidi ya kemikali 200 ambazo baadhi huathiri seli za mwili taratibu na kupelekea kwa saratani


 2. Unywaji wa pombe kupitiliza

Matumizi ya pombe yameongezeka sana miongoni wa vijana na watu wazima huku madhara ya kiafya ya pombe hizo yakisahaulika. 

Kunywa pombe kupitiliza kiwango hupelekea saratani hasa za ini, umio, koo, rektamu na hata matiti.

Hivyo kunywa kwa kiwango kinachotakiwa au kuacha kabisa ni bora zaidi.

3.  Ulaji horera

Matumizi ya chakula bila ya kuzingatia ubora wa mlo imekuwa changamoto kubwa sana miongoni mwa watu siku hizi kutokana na sababu mbalimbali kama vile ubize wa kazi na ukosefu wa maarifa. 

Hii imepelekea watu wengi wakutumia vyakula vya "fast food" ambavyo vimekuwa na kiwango kikubwa cha mafuta, chumvi na hata sukari huku ulaji wa mboga mboga za majani na matunda vikipungua.

Hali hii ni hatari kwa afya na huweza kupelekwa saratani kadhaa kama za utumbo na tezi dume.

4. Kutofanya mazoezi ya mwili

Uwepo wa nyenzo nyingi za usafiri ikiwemo magari pamoja na matumizi ya vifaa kama "remote control" yamepelekea watu wengi kushindwa kuufanyishwa mwili mazoezi hivyo kukosa uwiano sawia wa chakula kinachoingia mwilini na nguvu inayotumika.  Hii huhatarisha sana saratani za utumbo, matiti, ini, kongosho na tumbo

5. Uzito uliopitiliza/unene

Asilimia 20 ya kansa zote huchangiwa na uzito uliopitiliza katika kiwango cha BMI ya 30 au zaidi. Hii hutokana na mwili kuwa na mafuta mengi sana ambayo ni hatarishi kwa magonjwa ya saratani. 

 Hivyo unene sio sifa wala sio mafanikio bali ni kujichimbia kaburi mwenyewe. 

 6. Vimelea vya magonjwa

Vimealea mbalimbali vimekuwa vikihusishwa na kutokea kwa saratani kadhaa. Vimelea hivyo ni pamoja na virusi na bakteria

Virusi (VVU-hupelekea saratani iitwayo kaposi n.k, Virusi vya homa ya ini-HBV, HCV hupelekea saratani ya ini, virusi vya HPV hupelekea saratani ya shingo la uzazi)

Bakteria kama H.pylori wanaweza kupelekea saratani ya tumbo

                                    

 7. Uchafuzi wa hali ya hewa

Gesi hatari kutoka katika magari na zile za viwandani zimekuwa zikichafua anga na hivyo watu kuvuta hewa chafu ambayo ni hatari kwa mwili kwani huweza kupelekea saratani ya mapafu

8.  Mionzi mikali ya jua

Jua ni kitu muhimu katika maisha ya kila siku lakini kwa upande wa pili mionzi hatari ya jua imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa ongezekeo la saratani hasa ya ngozi. Uchafuzi wa hali ya hewa imepelekea mionzi hii hatari kutoka kwenye jua huweza kufikia watu kutokana na kuharibika kwa tabaka la kuchuja mionzi ya jua (Ozoni).

9.  Ongezekeo la kemikali hatari

Baadhi ya kemikali mbalimbali kama radoni, arsenita n.k ambazo zinapatikana katika ardhi na miamba  zimekuwa zikihusishwa na kuchangia kwa saratani kama vile ya mapafu na  ya kibofu cha mkojo

Jitihada za kupambana na saratani karne hii ni za muhimu sana kwani watu wengi wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na maradhi haya. Hivyo ni vyema  kufuata mtindo bora wa maisha, kuepukana na vihatarishi tajwa hapo juu na bila ya kusahau kuonana na wataalamu wa afya mara kadhaa kwa ajili ya uchunguzi, tiba na ushauri.

Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.