Watu wengi wanaweza kuwa na ugonjwa wa kisukari pasipo wao kutambua sababu ikiwa ni pamoja na kutofahamu dalili za awali za ugonjwa wa kisukari lakini pia dalili hizo huonekana zisizo na madhara kwao. Kutokana na kuongezeka kwa huduma za uchunguzi nyakati hizi, watu wamekuwa wakigundulika na ugonjwa huu hata kabla ya dalili, hii imesaidia kupungua kwa madhara yatokanayo na ugonjwa wa Kisukari ambao haudhibitiwi. Baadhi ya dalili zinazoweza kuashiria ugonjwa wa Kisukari ni pamoja na;
1. Kukojoa mara kwa mara
-Inapotokea hitilafu katika homoni ya Insulini kiasi cha kushindwa kufanya kazi vizuri hupelekea sukari nyingi katika damu kuliko kawaida. Hii hupelekea mwili kutoa sukari nje kwa njia ya mfumo wa mkojo. Ikumbukwe si kila anayekojoa mara kwa mara ana ugonjwa Kisukari.
2. Kupatwa na kiu sana
3. Kupatwa na njaa kali
4. Kuchoka mara kwa mara
5. Kupungua kwa uzito wa mwili
6. Kupungua kwa uwezo wa macho kuona
7. Kupata ganzi katika mikono na miguu
Mishipa ya damu pamoja na mishipa ya fahamu katika mikono na miguu huathiriwa na sukari nyingi mwilini na hivyo kusababisha hali ya ganzi maeneo hayo.
Magonjwa mengine tofauti na kisukari yanaweza kupelekea dalili tajwa hapo juu . Hivyo, ni muhimu kutambua kuwa dalili tu haitoshi kusema mtu ana ugonjwa wa Kisukari, ni vyema kufika katika kituo cha afya na kuonana na mtaalam kwa uchunguzi na vipimo zaidi kudhibitisha tatizo hili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni