MADHARA ISHIRINI NA MOJA (21) YA KIAFYA YATOKANAYO NA UNENE AU UZITO ULIPITILIZA.

 Unene ni tatizo sugu hivi karibuni ambalo linaongezeka kwa kasi sana miongoni mwa watu. Limekuwa tatizo kutokana na athari katika afya kwa watu mwengi, likiathiri wakubwa kwa wadogo.

Tatizo hili limetokana na kukosekana kwa uwiano wa nguvu ya chakula inayoingia ndani (kwa kula vyakula mbalimbali hasa wanga) na ile inayotumika (kwa kuushughulisha mwili), hivyo hupelekea mkusanyiko wa mafuta mengi mwilini na kupata unene au uzito uliopitiliza. Haya ndio madhara;

1. Kisukari aina ya pili

-Zaidi ya 80% ya ugonjwa wa kisukari huchangiwa na unene ambao hutokana na mafuta yaliyozidi mwilini.  Mafuta haya huathiri utendaji wa homoni ya Insulini na hivyo kushindwa kufanya kazi vizuri.

2. Shinikizo la juu la damu

-Unene huchangia kutokea kwa tatizo hili huku ikionekana kuongeza shindikizo la damu zaidi kwa ambaye tayari ana tatizo  hili.

-Tafiti zimeonyesha kuwa kupunguza 10% ya uzito hupunguza shinikizo la damu kwa kiasi kikubwa, ndio maana wagonjwa wote wenye tatizo hili husisitizwa kufanya mazoezi na kuzingatia ulaji bora ili kudhibiti uzito wao.

3. Kuongezeka kwa lehemu mbaya

-Lehemu (cholesterol) ni moja ya mafuta ambayo huongezeka mwilini kwa wingi hasa kwa watu wenye unene. Mafuta haya kwenye damu huweza kuathiri moyo, ubongo, mishipa ya damu, ini n.k

4. Shambulizi la moyo

-Wingi wa lehemu nyingi kwenye damu kuliko kawaida huweza kupelekea utengenezwaji wa uzio katika mishipa ya damu ya kwenye moyo ambao huzui mtiririko wa damu na kuasabaisha shambulizi la moyo na hivyo moyo kushindwa kufanya kazi.

5. Kiharusi

-Athari ya mafuta mengi mwilini katika moyo na mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye ubongo(kwa kuchangia utengenezwaji wa uzio) husababisha damu kutofika huko vizuri na hivyo kupata tatizo hili.

6. Kuharibu mzunguko wa hedhi

-Kwa wanawake tatizo hili hupelekea hedhi kutokwenda kwa utaratibu sahihi au huweza kusababisha hedhi kukosekana kabisa na hivyo huweza kuchangia katika shida ya kushika mimba kwa wanawake wengi wanene.

7. Kupunguza hamu ya tendo la ndoa

-Uzito uliopitiliza au unene umechangia kwa kiasi kikubwa kwa watu wengi kukosa hamu ya tendo la ndoa na pia hunguza mshindo wakati wa tendo hili. 

-Kukosekana kwa uwiano wa homoni za uzazi huchangia kwa tatizo hili.

8. Kupunguza nguvu za kiume.

-Hii ni changamoto kwa watu wengi siku hizi ikiwa inasababishwa na mambo tofauti tofauti ikiwemo ya unene au uzito uliopitiliza kutoka na athari katika mishipa ya damu 

-Tatizo hili huweza kupelekea mizozo miongoni mwa wapenzi.

9. Saratani

-Unene huchangia sana kwa saratani nyingi katika mwili kutokea ikiwa ni pamoja na saratani ya tumbo la uzazi, saratani ya matiti, saratani ya ini, saratani ya utumbo mapana, saratani ya tezi dume, saratani ya ovari n.k

10. Mawe kwenye mfuko wa nyongo

-Mbali na vihatarishi vingine kama miaka zaidi ya 40, ujauzito, kuwa wanamke, n.k, unene umechagia kwa sehemu kubwa kutokea kwa tatizo hili ambalo hupelekea maumivu makali upande wa kulia wa tumbo kwa juu.

11. Kupatwa na kiungulia

-Hali hii husababisha hisia ya kitu kinachopanda kutokea usawa wa tumbo kwenda kwenye koo kutokana na mgandamizo wa tumbo  kuwa mkubwa na kupelekea asidi ya tumbo kupanda juu.

12. Kukoroma

-Unene hupelekea hali ya kukoroma kwa watu nyakati za usiku kutokana na athari za uzito mkubwa katika njia ya hewa.

13. Maumivu sugu ya magoti na mgongo

-Kutokana na ukweli kuwa magoti na mgongo hubeba uzito mkubwa wa mwili basi hupelekea maeneo haya kupata maumivu ya mara kwa mara kwasababu ya msuguano wa mifupa katika maungio.

14. Damu kuganda katika mishipa ya damu ya miguu.

-`Athari ya unene ni kufanya damu kushindwa kusafiri vizuri katika mishipa ya damu iitwayo veini kutokana na damu kutengeneza hali ya mabonge mabonge.

-Hatimaye miguu huanza kuvimba ikiambatana, maumivu makali sana na wakati mwingine ganzi.

15. Mawe katika figo

-Utengenezaji wa mawe madogo madogo katika mafigo kutokana na uzito uliopitilza au unene huweza kupelekea athari zingine kama figo kujaa maji na  maambukizi ya vimelea katika mfumo wa mkojo.

16. Kujikojolea

-Hali hii inaweza ikawatokea zaidi wanawake kutokana na mgandamizo mkubwa kwenye mfumo wa mkojo na hivyo kupelekea kushindwa kujizuia wanapokuwa wamebana.

-Ikumbukwe kuwa mfumo wa mkojo wa mwanamke ni mfupi kutokea nje kuliko ule wa mwanaume.

17. Sonona

-Hali hii ya kisaikolojia ambayo humfanya mtu kuwa na huzuni muda mwingi katika siku huweza kumtokea mtu mwenye unene

-Mambo yanaweza kuchangia hali hii ni pamoja na mtu mwenyewe kutofurahiswa na muonekana wa mwili wake lakini kuzungumziwa vibaya na watu wengine juu ya uenene wake.

18. Matatizo kipindi cha ujauzito

-Inapofika wakati wa kujifungua inaweza ikawa changamoto kwa mwanamke kujifungua kwa njia ya kawaida kutoka na unene kusababisha njia ya mtoto kupita kutotosha na hivyo kupelekea kujifungua kwa njia ya upasuaji.

19. Michirizi na weusi wa ngozi.

-Michirizi katika ngozi huashiria wingi wa mafuta chini ya ngozi na hali ya weusi katika maeneo ya shingo, makwapani na kwenye vidole hutokea.

20. Mafuta mengi katika ini

-Ufanisi wa kazi ya ini huweza kupungua kutokana na mafuta mengi yanayozunguka ini na kupelekea maumivu ya tumbo ya mara kwa mara.

21. Ngiri

-Tatizo hili hutokanana mgandamizo mkubwa wa mwili na hivyo kupelekea maeneo dhaifu ya mwili kuanza kujaribu kutoa vitu nje ya mwili (kama utumbo n.k)

-Maeneo ya mara kwa mara yanayopatwa na tatizo hili ni pamoja na kwenye kitovu, juu ya kitovu, katikati ya paja na via vya uzazi vya nje n.k

Haya ni baadhi ya athari tu za unene katika mwili wa binadamu. Hivyo unene au uzito uliopitiliza sio jambo la kulichukulia kawaida, muhimu kuanza jitihada ili kuwa na uzito bora kiafya.

Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.