HAYA NDIO MAMBO YANAYOCHANGIA KUPELEKEA AINA HII YA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU (PRIMARY)

Ni kweli kwamba watu wengi wengi wamekuwa wakiathiriwa na shinikizo la juu la damu (Primary hypertension) pasipokujua chanzo ni nini. Tafiti mbalimbali za kisayansi zinaonesha kuwa chanzo halisi  cha shinikizo la juu la damu aina ya "primary" hakijajulikana huku mambo kadhaa yakihusishwa kuchangia kwa tatizo hili. Haya mambo ni pamoja na


1. Vyakula/mlo wenye chumvi nyingi.

Ulaji wa chumvi nyingi sana yani zaidi ya gramu 3 kwa siku (sawa na takribani nusu ya kijiko cha chai) huongeza hatari ya kushambuliwa na tatizo la shinikizo la juu la damu. 

Matumizi ya chumvi nyingi hutokea wakati wa kuunga chakula kinachopikwa, kwenye kuchovya chumvi moja kwa moja wakati wa kula baadhi ya vyakula au kuongeza chumvi moja kwa moja wakati wa kula.

2. Uzito uliopitiliza/unene

Hii imekuwa moja ya kihatarishi kikubwa cha kupata shinikizo la juu la damu kutoka na watu wengi kuwa na ulaji wa vyakula usio sahihi lakini pia kushindwa kufanya mazoezi. Moja ya njia ya kupata matokeo bora ya kudhibiti shinikizo la juu la damu ni kupunguza uzito.

3. Kutofanya mazoezi

Maisha ya kukaa bila ya kuufanyisha mwili mazoezi yanaambatana na ongezeko la juu la shinikizo la damu. Ukuaji wa sayansi na teknolojia ambapo uwepo wa magari, remoti kontro za maredio na televisheni vimechangia kwa kiasi kikubwa watu kushindwa kufanya mazoeezi.

4. Unywaji wa pombe kupitiliza.

Matumizi ya pombe kupita kiasi yameonekana kuchangia kwa tatizo la shinikizo la juu la damu kwa baadhi ya watu na kupelekea maradhi ya moyo. Kutokunywa pombe kabisa au kunywa kwa kiwango unachoshauri wa daktari kumesaidia sana katika kudhibiti kiwango cha shinikizo la juu la damu.

5. Uvutaji wa sigara au tumbaku.

Utumiaji wa sigara au tumbaku umeonekana kuchangia pia kwa kuibuka kwa tatizo la shinikizo la juu la damu. Hii ni kutoka na madhara ya moja kwa moja ya sigara kwenye kuta za mishipa ya damu lakini pia huathiri ufanyaji kazi wa moyo.

6. Umri

Kadiri umri unavyoongezeka ndio nafasi ya mtu kupatwa na tatizo la shinikizo la juu la damu huongezeka. Hii inachangiwa kutokana na mabadiliko katika mishipa ya damu kwa kuwa migumu kutanuka na miembamba na hivyo kuongeza ukinzani wa damu wakati wa kusambaa mwilini. 

Asilimia kubwa ya watu wamekutwa na tatizo la shinikizo kubwa la damu kuanzia miaka 50-59.

7. Historia ya shinikizo la juu la damu katika familia.

Tafiti zinaonesha kuwa nafasi ya kupata tatizo hili huwa ni mara mbili kwa watu ambao wana mzazi mmoja au wawili ambaye ana tatizo hili au aliwahi kuwa na tatizo hili la shinikizo la juu la damu. Hali hii inapelekea ugonjwa huu kuhusishwa na kigezo cha vinasaba.

8. Asili ya jamii.

Imeonekana katika tafiti mbalimbali kuwa jamii ya watu wenye asili ya weusi huathirika mapema  zaidi na tatizo hili ukilinganisha na asili ya jamii zingine.

Kinga ni bora kuliko tiba, hivyo hatuna budi kuzingatia ushauri wa kitaalamu kuhusiana na namna ya mtindo bora wa maisha ili kuepukana na tatizo hili. Maradha ya tatizo hili ni makubwa sana kuliko watu wengi wanavyofikiria. Kumbuka kupima kiwango chako cha shinikizo la damu kila mara uendapo hospitalini.



Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.