FANYA MAMBO HAYA SABA(7) KUZUIA NA KUDHIBITI SHINIKIZO LA JUU LA DAMU.

 Shinikizo la juu la damu ni tatizo la siku zote endapo utagundulika na kudhibitishwa nao. Tatizo hili hupelekea madhara mengi sana mwili kama halitadhibitiwa ipasavyo. Njia mbalimbali za kitaalamu zimeonekana zikifanya kazi nzuri sana ya kuzuia na kudhibiti kiwango cha juu cha shinikizo la damu mbali na kutumia dawa, mambo hayo ni pamoja na;

1. Kupunguza uzito uliopitiliza au unene.

-Tafiti zimeonesha kuwa kwa kila kilo 1 ya uzito uliopungua hupelekea punguzo la presha kwa milimita za Mekyuri 0.5 mpaka 2. Hii inaleta matumaini kwa watu ambao wameshagundulika na tatizo hii na wameshaanza mazoezi

-Ni muhimu kutambua kuwa ongezeko la BMI ya 25 au zaidi pamoja na ongezeko la ukubwa wa kiuno huambatana na tatizo la shinikizo la juu la damu

-Namna nzuri ya kupunguza unene ni pamoja na kufanya mazoezi, ulaji bora wa chakula kwa kupunguza kiwango cha wanga na pia kuhamasika katika mtindo huu wa maisha.

Jenga mazoea ya kupima uzito wako kila baada ya mwezi na kuweka kumbukumbu endapo utaanza program ya kupunguza uzito.

2. Punguza kiwango cha chumvi kwenye chakula kwa siku

Hii ni muhimu sana kwani kupitia utumiaji wa chumvi mwili hupokea madini ya sodium ambayo huwa na athari kubwa kwenye shinikizo la damu.

Kiwango kinachoshauriwa na Shirika la Afya duniani ni gramu 2 au chini ya madini ya sodium katika chumvi ambapo ni sawa na kijiko kimoja cha chai au pungufu kwa siku.

Ili kujiepusha na ulaji wa chumvi zaidi ya kiwango kinachotakiwa basi;

i. Epuka kuongeza chumvi wakati unakula chakula

ii. Epuka ulaji hovyo wa hovyo wa vyakula vilivyopakiwa bila ya kusoma lebo

iii. Jitahidi kupika chakula chako kwa kutumia viungo tofauti vyenye kuleta radha mbadala wa chumvi.

3. Kuongeza ulaji wa vyakula vyenye madini ya potashiamu

-Tafiti zinaonesha kuwa madini ya potashiamu mwili katika kiwango sahihi kusaidia katika kupunguza shinikizo la juu la damu na endapo yatapungua basi si salama.

-Vyanzo bora vya madini ya potashiamu ni pamoja na ndizi mbivu, maji ya madafu, parachichi, spinachi, matikiti maji n.k

-Haishauriwi kutumia suplimenti za potashiamu kwa watu wenye matatizo ya figo au wenye kutumia baadhi ya dawa kwani wanaweza kupelekea kiwango cha potashiamu kuwa juu sana na kuathiri moyo.

4. Hakikisha unapata mlo bora (DASH)

-Aina hii ya mlo uitwao DASH (Dietary Approches to Stop Hypertension) umewekwa na wataalamu wa Afya husasi kwa ajili ya kuzuia shinikizo la juu la damu. Mlo huu hujumuisha mambo yafuatayo;

i. Wingi wa mbogamboga na matunda

ii. Maziwa na zao mbalimbali kutokana na maziwa

iii. Nafaka isiyokobolewa + nyama ya kuku, samaki na karanga

iv. Uchache wa vinywaji vyenye sukari sana na nyama nyekundu.

-Umuhimu wa mlo huu ni kuwa una virutubisho vingi vya potashiamu, calcium, protini, na makapi-mlo huku mafuta na lehemu vikiwa kidogo sana.

5. Fanya mazoezi

-Mazoezi ya aerobiki pamoja na mazoezi ya kuimarisha misuli hupunguza shinikizo la juu la damu kwa milimita za Mekyuri 4-6  kwa sistoliki na milimita za Mekyuri 3 kwa diastoliki.

-Jambo la msingi ni kuweka jitihada katika mazoezi bila ya kukata tamaa kila wiki angalau siku 3 hadi 4 za mazoezi huku ukiendelea kufuata ushauri mwingine.

6. Kudhibiti kiwango cha unywaji wa pombe.

-Inashauri kutumia pombe kwa kiwango cha wastani kama ni mnywaji wa pombe au kuacha kabisa kama utaamua na kuhamasika. Endapo hujawahi kutumia pombe basi ni vyema usitumie kabisa

-Kiwango cha pombe kinachoshauri kiafya na kimeonekana kutoleta madhara kwenye shinikizo la damu ni kutumia uniti 14 katika wiki kwa jinsi zote mbili aidha wanaume au mwanamke.

Uniti moja (1) hii hutofautiana katika kiwango kulingana na aina ya pombe. Ongea na daktari uweze kupata ushauri kulingana na matumizi yako

7. Epuka uvutaji wa sigara

-Uvutaji wa sigara umehusishwa kwa karibu sana kuchochea tatizo hili la shinikizo la juu la damu kutoka na athari yake kwenye mishipa ya damu

-Inashauriwa kuachana kabisa na uvutaji wa sigara kama ni mtumiaji na kuepuka kabisa kujihusisha na uvutaji wa sigara endapo hujawahi kutumia kwa si salama kabisa.

Pamoja na njia nzuri zilizotajwa hapo juu, umuhimu wa kutumia dawa pia bado upo kama njia moja wapo ya kudhibiti shinikizo la juu la damu endapo daktari ameshakuanzishia dawa.

Ifahamike kuwa sio kila mtu mwenye shinikizo la juu la damu atahitaji matibabu ya dawa bali kila kila mwenye shinikizo la juu la damu atahitaji kufanya mambo aliyoelezewa juu.

Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.