JIEPUSHE NA MADHARA YA UGONJWA WA SELIMUNDU KWA KUZINGATIA MAMBO YAFUATAYO

 Maradha ya mara kwa mara yatokanayo na ugonjwa wa Selimundu hudhoofisha afya ya mtu na hata huweza kupelekea kifo. Kinga ni bora kuliko tiba, hivyo ni muhimu sana kuzingatia mambo yafuatayo ili kujiepusha na matatizo ya ugonjwa huu yanayoweza kusababisha kulazwa mara kwa mara,kukuingiza gharama ambazo hukutaraji na hata kuhatarisha maisha.

1. Kunywa maji ya kutosha kila siku

-Ni lazima kuzingatia unywaji wa maji ya kutosha ambayo ni safi na salama kila siku kulingana na uzito wako, shughuli na hali ya hewa.  Hii husaidia kuepusha visa vya mara kwa mara vya maumivu ya mwili kwenye mifupa, maungio, tumbo na kifua.

-Unywaji wa maji mengi husaidia kuzuia chembechembe za selimundu kuziba katika mishipa ya damu.

2. Kutumia vidonge vya Folic acid kila siku.

-Kutokana na kiasi ulichoambiwa na mtaalam wa afya, hautakiwi kuacha kutumia vidonge vya Folic acid hata siku moja. Vidonge hivi husaidia katika utengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu ambazo hupungua kila siku kwa kuvunjwavunjwa (selimundu) na mwili.

3. Epuka hali ya hewa ya ubaridi sana au joto sana.

-Aidha ubaridi sana au joto sana huweza kuchangia kwa visa vya mara kwa mara vya maumivu makali ya viungo vya mwili na kupelekea kwenda hospitali kila baada ya muda mfupi.

-Majira ya badiri inashauri mgonjwa kujifunika kwa nguo nzito kama sweta au koti

4. Kunawa mikono yako kwa maji salama.

-Suala hii ni muhimu kwa wagonjwa hawa ukizingatia kuwa kinga ya mwili iko chini na hivyo wako kwenye uhatari wa kupata vimelea vya maambukizi kirahisi kutokana na mikono michafu.

5. Zingatia ulaji wa mlo kamili

-Ugonjwa wa selimundu husababisha kudhoofisha mwili, hivyo ni muhimu kuzingatia ulaji wa mlo wenye virutubisho vyote katika kiwango kilicho sahihi ili kuweza kujenga mwili na kuimarisha kinga ya mwili.

6. Epuka kuishi maeneo ya miinuko.

-Maeneo haya yaliyoinuka sana kutoka usawa wa bahari (mita 1900) huwa na kiasi kidogo cha oksijeni hivyo huchochea chembechembe za selimundu kuzidi kuleta hitilafu katika mishipa ya damu na hivyo kupelekea maumivu makali.

-Endapo utaenda katika mazingira haya basi jitahidi kunywa maji ya kutosha kuepuka na tatizo hili.

7. Zingatia  chanjo 

-Wagonjwa wengi wenye ugonjwa huu huwa kwenye uhatarishi wa maambukizi ya bakteri mwilini. Hivyo chanjo hushauri ili kuwakinga dhidi ya maradhi yatokanayo na bakteri hawa.

-Chanjo hizi ziko za aina mbili (PCV-13 na PPSV-23) ambazo hutakiwa kutolewa kwa wagonjwa hawa katika nyakti tofauti tofauti. Jitahidi kufika kituo cha afya kupata huduma hii

8. Epuka kufanya mazeozi magumu

-Mazoezi ni muhimu kwa watu wote hata walio na ugonjwa huu. Jambo la msingi ni kujitahidi kufanya mazoezi mepesi (wastani) na kuepuka mazoezi magumu ambayo ni yale yanayokufanya ushindwe kukamilisha sentensi pale unapojaribu kuongea na kufanya mapigo ya moyo kwenda haraka sana. 

-Mazoezi haya magumu huchochea maumivu ya mwili.

9. Kutumia dawa iitwayo Penicillin V ipasavyo

-Mgonjwa wa selimundu anatakiwa kutumia  dozi ya dawa hii kulingana na umri wake ili kujikiepusha na maradhi yatokanayo na vimelea vya bakteria. 

-Dawa hii hutumiwa na mgonjwa mpaka pale mgonjwa atakapofikisha umri wa miaka mitano (5). Ni muhimu kufuata maagizo ya daktari

10. Hudhuria kliniki mara kwa mara.

-Mgonjwa mwenye selimundu anashauri kuonana na mtaalamu (daktari) mara kwa mara ili kuweza kupata tathmini ya afya yake kwa kufanyiwa vipimo, kupata tiba na ushauri bora. 

Hutakiwi kusubiria tatizo kutokea ndipo unaenda kuonana na mtaalam wa afya. 

Mgonjwa wa selimundu anastahili maisha bora na salama kama watu wengine. Hii inawezekana kwa kufuata mambo yote yaliyoelezewa na mengi ambayo wataalamu wa afya wanaendelea kushauri. 

Share:

Maoni 1 :

  1. Kazi nzuri ya kuelimisha kwa ugonjwa wa selimundo..muendelee kwa upana zaidi muweze kuwafikia wananchi wa hali us chini wapate elimu hii

    JibuFuta

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.