NAMNA UGONJWA WA SELIMUNDU UNAVYOHATARISHA MFUMO WA MIFUPA NA MISULI MWILINI

 -Ugonjwa wa selimundu huathiri mifumo mbalimbali katika mwili ikiwemo mfumo wa misuli na mifupa. Hii hutokana na kuwa selimundu hupelekea athari katika mishipa ya damu  kama kuziba kwa mishipa ya damu pamoja na urahisi wa wagonjwa hawa kupatwa na maradhi kutoka na kinga kupungua.  Matatizo ya ugonjwa huu katika mfumo wa mifupa na misuli ni ;

1. Maumivu makali sana katika maungio na mifupa

Moja ya shida kubwa inayowapata wagonjwa wenye selimundu ni maumivu makali katika mifupa na maungio. Hii ni sababu kubwa ya watu wengi kupelekwa hospitali mara kwa mara kwa ajili ya tiba. 

Mifupa kama ya miguu, mbavu, mgongo na kichwa huhusishwa sana. Hali hii pia huweza kuendana na kuvimba kwa maungio ya mikono na miguu hasa kwa watoto.

2. Maambukizi ya mifupa

Mbali na maumivu ya mifupa, wagonjwa wenye selimundu huwa katika uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya mifupa kutoka kwa vimelea hasa bakteria. Hii huweza kuanzia nje (kwenye ngozi) na kufika hadi ndani (kwenye mifupa)

3. Maambukizi kwenye maungio

Maungio ambapo ni sehemu mifupa miwili au zaidi hukutana huweza kushambuliwa na vimelea vya magonjwa hasa bakteria na hivyo kupelekea sehemu hizo kuwa na maumivu makali pamoja na kuvimba. Hali hii huweza kumfanya mtu ashindwe kutumia maungio hayo (kama vile bega , goti n.k)

4. Vidonda sugu katika miguu

Kuziba kwa mishipa ya damu kutoka na uwepo wa selimundu katika mishipa hiyo hupelekea damu kushindwa kufika maeneo mbalimbali  ikiwemo miguuni. Hii hupeleka kufa kwa tishu mbalimbali na kisha kuibuka kwa kidonda ambacho kinachukua muda mrefu sana kupona.

5. Kuharibika kwa vichwa vya mifupa ya maungio ya nyonga na bega.

Vichwa vya mifupa mirefu ya kwenye nyonga na bega huathirika taratibu na ni ngumu kufahamu katika hatua za awali ila athari ikiwa hatua ya mwisho basi ni rahisi kutambua. 

Dalili kubwa ya tatizo hili ni pamoja na maumivu endelevu sehemu hizo ambayo huambatana na kupungua kwa mzunguko wa maungio hayo na mwisho wa siku maungio haya kutofanya kazi kabisa.

6. Kuvunjika kwa mifupa

Mabadiliko mbalimbali hutokea katika uroto mwekundu kutokana na mchakato wa kufidia chembechembe nyekundu(selimundu) zinazovunjwa kila muda. Hii hupelekea kudhoofisha mifupa na kuiweka katika uhatari wa kuvunjika kirahisi.

Kugundua na kutibu tatizo mapema ni mwanzo mzuri wa kuzuia madhara mbalimbali yatokanayo na ugonjwa huu wa selimundu. Ni vyema kuonana na mtaalamu mara kwa mara (kliniki) ili kuweza kupata tathimini ya maendeleo ya ugonjwa na hivyo kuwa salama zaidi.

Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.