Maambukizi katika miguu pamoja na vidonda vinavyochelewa kupona ni madhara makubwa wanayoyapata watu wenye ugonjwa wa kisukari endapo hawatochukua hatua mapema. Hali hii inaweza kupelekea viungo kama vidole vya miguu au mguu wenyewe kukatwa. Kujiepusha na yote haya ni vema kuzingatia masuala haya kuhusu miguu yako
1. Dhibiti sukari yako kwenye damu.
Ukifanikiwa kudhibiti na kuendeleza kiwango kinachostahili cha sukari katika damu basi itasaidia kukuepusha na matatizo haya.
Kadiri kiwango cha sukari kinapokuwa juu (hakidhibitiwi inavyotakiwa) ndio hata matatizo ya vidonda vya miguu huongezeka.
Uchunguzi wa miguu inatakiwa liwe suala endelevu ili kufahamu kinachoendelea katika miguu. Ni vizuri kuoanana na daktari kwa ajili ya kupata tathmini ya miguu yako.
3. Toa taarifa kwa daktari wako.
Endapo utaona mabadiliko yoyote katika miguu yako kama vile; kupungua kwa hisia ya maaumivu, kuguswa au joto, kupungua kwa misuli ya miguu, ngozi kuwa kavu, mabadiliko ya maumbile ya miguu na vidole, michubuko n.k
Mabadiliko hayo usiyapuuze, fika hospitalini mara moja kuonana na daktari.
4. Fanya uchaguzi mzuri wa viatu.
Unashariwa kuvaa viatu ambavyo vinatakiwa kukutosha, vyenye uwezo wa kutanuka kulingana na mguu wako , vyenye sole laini kwa ndani. Epuka sana viatu vinavyobana
Hivyo kuwa makini kabla ya kununua viatu na ikiwezekana nunua viatu vilivyotengenezwa maalamu kwa watu wenye kisukari
5. Jichunguze miguu yako wewe mwenyewe kila siku.Ukiwa nyumbani , chunguza miguu yako kuona mabadiliko yoyote yanayotokea na hivyo kutoa taarifa mapema kwa daktari.Usipuuzie mabadiliko yoyote yameyojitokea hata kama ni madogo, ni vyema kupata ushauri wa daktari.
6. Fanya usafi wa miguu yakoNi muhimu sana kujiepusha na maambukizi ya miguu kwa kusafisha miguu vizuri wakati wa kuoga, kuikausha na kupaka mafuta kulainisha ngozi.
7. Kujiepusha kwa kutembea bila viatu.
Hii ni hatari sana kwani unaweza kujiumiza miguu kwa kujikwaa(kujigonga) au kukanyaga kitu chenye ncha kali hivyo kupelekea michubuko na vidonda vinavyochelewa kupona.
8. Kupunguza urefu wa kucha.Kuepukana na athari zozote za kucha ndefu kama michubuko, ni vyema kuzipunguza kucha mara tu zinapokuwa ndefu.
Kuwa makini unapotumia wembe wako kukata kucha
9. Epuka kujitibu mwenyewe matatizo yoyote ya miguuSi jambo zuri kuchukua hatua ya kujitu mwenyewe bila ya kufahamu kitu unachokitibu. Hii hupelekea madhara makubwa sana endapo mguu utapata maambukizi
Hakikisha unamuona daktari haraka sana kwa ajili ya tiba sahihi.
Kufanikisha mambo yote hayo hutokana na mtu kukubali ahli yake ya ugonjwa wa kisukari na kutekeleza ushauri tajwa. Kwa kufanya hivyo maradhi ya miguu yatokanayo na kisukari yatakuwa historia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni