NJIA SITA (6) ZA KUFANYA ILI USIPUNGUKIWE NA MAJI MWILINI

Maji ni uhai kwa mwanadamu kwani bila ya maji mwili hauwezi kufanya kazi zake inavyotakiwa. Kuna namna tofauti tofauti ambazo mwili hupoteza maji yake mwili ikiwa ni pamoja na ; kupitia mkojo, hewa ya unyevunyevu kutoka mapafuni, jasho na haja kubwa.

Ukosefu wa maji mwilini huweza kupelekea madhara makubwa mno ikiwemo kifo endapo kiasi cha maji kinachotoka ni kikubwa kuliko kinachoingia mwilini. Hii ndio namna ya kuufanya mwili kuwa na maji ya kutosha muda wote

1. Usisubiri mpaka upate kiu

-Takribani 2% ya uzito wote wa maji mwilini huwa umepotea kipindi usikiapo kiu. Hii si sawa na haishauriwi kwani hadi mtu anasikia kiu unakuta kiasi kingi cha maji kinakuwa kimeshapotea. 

-Kunywa maji muda wowote katika siku pasipokusubiria hadi kiu.

2. Kunywa maji kidogo kidogo

-Mtu mzima kulingana  shughuli na uzito wake hushauriwa kunywa maji mengi sana angalau lita 2. Ni ngumu kunywa lita hizi nyingi sana kwa wakati mmoja hivyo inashauriwa kutumia maji kidogo kidogo katika nyakati tofauti tofauti.

-Mfano unaweza kuzigawa lita unazotakiwa kunywa kwa siku katika majira ya asubuhi, mchana na jioni.

-Kwa kufanya hivi utajikuta mwili unakuwa na maji muda wote.

3. Beba chupa lako la maji muda wote.

-Kuwa na chupa lako la maji litakujengea tabia ya kunywa maji ya kutosha.Ni jambo zuri kubeba chupa yenye maji na kuwa nalo karibu wakati wa shughuli zako mafo; kazi, mazoezini, unapojisomea, kwenye gari n.k

4. Jiepushe na vinywaji vyenye kahawa au pombe.

-Takribani 80% ya maji mwilini tunatakiwa kuyapata kupitia maji safi na vinywaji vingine ispokuwa vinjwaji vyenye kahawa au pombe.

-Vinjwaji hivi hukufanya ukojea mara kwa mara na hivyo akupunguza maji zaidi. Hivyo vinywaji vyenye kahawa na pombe havihesabiki kama vyanzo vya maji yanayohitajika mwilini.

5. Kunywa maji kabla, wakati na baada ya mazoezi.

-Mazoezi ni moja ya shughuli ambazo hupelekea mwili kupoteza maji mengi sana hasa yanapochukua muda mrefu (zaidi ya saa 1) na kwenye kipindi cha joto

-Ni vizuri kunywa maji ya uvuguvugu angalau 1/2 ya kikombe mpaka vikombe viwili kila baada ya dk 15 -20 wakati wa mazoezi

6. Kuwa na maji katika kila mlo wako.

-Jenga utamaduni ambao utafanya kuwa na maji ya kunywa wakati wa kila mlo na inaweza kuwa pia maziwa, juisi n.k

-Hii husaidia kuongeza maji mwilini wakati wa mlo wa asubhi, mchana na usiku.

Maji mwilini yana kazi nyingi mno kiasi kwamba pasipo maji kazi hazifanyi na hupelekea mtu kuanza kulalamika baadhi ya dalili kama kuchoka choka, kichwa kuuma, n.k   

Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.