Unapofanya mazoezi kwa utaratibu maalum kuna mabadiliko mbalimbali yanayotokea katika mfumo wa moyo, mishipa ya damu, mfumo wa upumuaji, mfumo wa misuli na mifupa n.k Mabadiliko haya hupelekea mwili kuwa fiti kiafya kwa kukupatia matokeo yafuatayo ;
1. Kuimarika kwa mfumo wa moyo, hewa na mishipa ya damu
-Mtu huwa fiti ni matokeo ya kuimarika kwa mfumo wa moyo kwani huongeza uwezo wake wa kusukuma damu sehemu mbalimbali katika mwili na kuondoa uchafu katika damu kwa urahisi kwa kusaidiana na mfumo wa hewa.
2. Kuongezeka kwa nguvu katika misuli
-Kujihusisha na mazeozi kwa muda mrefu hukuletea matokeo ya kupata nguvu katika misuli tofauti na kipindi kabla kuanza mazoezi. Hali hii huufanya mwili kuwa mwenye nguvu kwa ujumla na husaidia sana katika kumpa mtu balansi au stamina.
3. Uimarikaji na ustahimilivu wa misuli.
-Moja ya muitiko wa mwili mara baada ya kujikita katika programu bora ya mazoezi kwa muda mrefu ni misuli ya mwili kuwa imara na stahimilivu kwa muda mrefu kipindi cha shughuli mbalimbali.
-Hii ni sehemu inayomfanya mwanamazoezi aweze kuwa fiti kwa kufanya shughuli fulani bila ya mwili kuchoka.
4. Uwezo wa kunyumbulika kwa maungio ya mwili.
-Mazoezi sahihi yenye kufuata utaratibu huweza kumpatia mtu uwezo wa maungo ya mabega, nyonga na shingo kubadilikabadilika kwa urahisi zaidi
-Hii husaidia katika kuepukana na athari ndogo ndogo wakati wa mazoezi mengine
5. Uwiano bora wa mwili.
-Mfanya mazoezi utaweza kumtambua kirahisi kwa kumtazama tu. Mazoezi humfanya mtu kuwa na uwiano mzuri wa mafuta mwilini (ndani na chini ya ngozi), misuli na mifupa.
-Haitakiwi mafuta kuwa mengi kuliko misuli kwa si salama kwa afya.
Kupata matokeo haya bora yanayoweka mwili wa mwana mazoezi fiti ni lazima kuzingatia programu maalumu ya mazoezi kutoka kwa mkufunzi au mtaalamu wa afya. Hii ni kutokana na ukweli kwamba sio kila anayefanya mazoezi yuko fiti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni