FAHAMU KWA KIASI GANI UNAFANYA MAZOEZI KWA KUTUMIA MAPIGO YA MOYO NA MAONGEZI

 Kiasi cha mazoezi yanayotakiwa kufanyika ni muhimu sana katika programu yeyote ile ya mazoezi ukizingatia umri, malengo ya mazoezi, usalama na afya ya mwili kwa ujumla miongoni mwa watu. Mbali na umuhimu huu, kumekuwa na changamoto kwa watu wengi kuhusiana na kipimo (kwa kiasi gani ) cha mazoezi yanayofanywa. Hiki ndio kiasi cha mazeozi unachoweza kufanya;

1. Mazoezi mepesi

-Haya ni mazeozi ambayo huhitaji nguvu kidogo kufanyika na ni mazoezi ambayo hayatoi jasho ikiwa hali ya hewani si ya joto kali.

-Mapigo ya moyo huenda kawaida na unapumua kwa urahisi (kawaida).

-Unaweza kuongea vizuri kabisa hata kuimba 😂kama una kipaji wakati wa mazoezi haya.

-Mfano wa mazoezi haya ni; kutembea taratibu (kilomita 3 ndani ya saa 1), kufanya shughuli ndogo ndogo za nyumbani kama kupika, kudeki

2. Mazoezi ya wastani

-Haya ni mazeozi ambayo hukufanya utumie nguvu kiasi ili kufanikisha na ni mazoezi ambayo hukutoa jasho mara baada ya muda mfupi angalau dk 10

-Hufanya mapigo ya moyo kuongezeka zaidi na hata kasi ya kupumua huongezeka pia.

-Mazoezi haya hukufanya uweze kuongea lakini hutoweza kuimba kama ni mpenzi wa muziki.

-Mfano; kutembea harakaharaka (kilomita 4-6 ndani ya saa 1), kuendesha baiskeli n.k

3. Mazoezi ya magumu

-Haya ni mazoezi ambayo hutumia nguvu kubwa kuyafanya na hukutoa jasho jingi sana ndani ya muda mfupi sana wastani wa dk 4.

-Hufanya mapigo ya moyo kuongezeka sana huku ukipumua kwa haraka sana.

-Mazoezi haya hukufanya kuongea maneno machache /sentensi fupi fupi huku ukisimama kuvuta hewa (kuongea sentensi nzima ni kazi kwenye mazoezi haya)

-Mfano; kukimbia, kuruka kamba, mazoezi ya kubeba vyuma vizito, mazoezi ya jimnastiki kama vile pushups, kujivuta kwenye viunzi n.k

Mazoezi ni afya, vema kuanza leo mazoezi hatua kwa hatua kuliko kutofanya kabisa. Panga malengo yako, onana na daktari kabla ya kuanza mazoezi ili kujua afya yako na kisha kiwango chako cha mazoezi ili kuepusha athari zozote kujitokeza wakati wa mazoezi.

Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.