BAADHI YA MADHARA YA DAWA (SINDANO) YA INSULINI YANAYOWEZA KUTOKEA KWA MGONJWA MWENYE KISUKARI.

 Sindano ya Insulini ni moja ya dawa muhimu sana katika matibabu ya ugonjwa wa kisukari. Sindano hii huanzishwa kutokana na sababu mbalimbali kulingana na daktari alivyofanya tathmini. Insulini kama dawa zingine nayo ina madhara kadhaa kipindi mtu anaitumia ingawa faida ya dawa ni nyingi kuliko madhara yake. Ni vema kujua madhara haya ili usipatwe na wasiwasi. 

1. Kushusha sukari katika damu kuliko kawaida.

-Hii ni hali hatari sana ambayo imekuwa ikijitokeza miongoni mwa wangonjwa wanaotumia insulini. Mambo mbalimbali yameweza kuchangia kwa tatizo hili ikiwemo kutumia dozi kubwa sana ya dawa, kufanya mazoezi magumu sana baada ya kutumia Insulini,  kutopata "snacks " katikati ya milo mikubwa n.k

-Ushukaji huu wa sukari zaidi kwenye damu hupelekea mgonjwa kupatwa na dalili kama kuchoka sana, kizunguzungu, kutokwa na jasho jingi, kutetemeka, kukosa umakini n.k

2. Kuvimba na kuwasha eneo la sindano.

-Uchomaji wa sindano ya insulini unaweza kupelekea mzio(allergy) katika eneo la mwili (ngozi) linalochomwa na hivyo kupatwa na hali ya muwasho, kuvimba na hali ya wekundu eneo hilo

-Hali hii huweza kutokea ndani ya muda mfupi baada ya kuchoma sindano na huisha taratibu, huweza kuchukua hadi wiki 1.

3. Kusinyaa au kuvimba kwa ngozi

-Endapo sindano ya Insulini huchomwa eneo moja kwa muda mrefu bila ya kubadili eneo jingine , hii hupelekea kwa mabadiliko ya ngozi ambayo ni kuvimba au kusinyaa kwa ngozi eneo hilo. 

-Hali husababisha muonekano mbaya wa ngozi ya mgonjwa. 

4. Kuongezeka uzito.

-Matumizi ya sindano kwa wagonjwa wengi yameonekana kupelekea ongezeko la uzito huku sababu kamili ya tatizo hili halijapata majibu ya moja kwa moja.

-Hivyo wagonjwa ambayo wako kwenye Insulini wanatakiwa kuongeza umakini katika kudhibiti uzito wao kupitia vyakula wanavyokula na mazoezi.

5. Mzio (Allergy) wa mwili mzima

-Hali hii si rahisi na kawaida kutokea ingawa inaweza kutokea. Endapo inatokea hupelekea hali mbaya  sana na kusababisha dalili mbalimbali kwa mgojwa kama kupumua kwa shida, kutoka jasho kwa wingi, kuhisi kupoteza fahamu, mapigo ya moyo kwenda harakaharaka n.k

-Ikitokea hali hii inabidi ukimbizwe katika kituo cha afya cha karibu kwa matibabu ya haraka.

Ni muhimu sana kufuata maelekezo ya daktari kuhusiana na dawa ya Insulini lakini pia inashauriwa kuonana na daktari au mtaaalmu wa afya unapopatwa na shida au wasiwasi wowote katika utumiaji wa sindano ya Insulini.


Share:

Maoni 1 :

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.