-Kisukari ni ugonjwa sugu ambao hupelekea kiwango cha sukari katika damu kuwa kikubwa zaidi ya kawaida kutokana na aidha homoni ya Insulini haizalishwi kabisa au huzalishwa isiyojitosheleza au kuwepo kwa ukinzani mkubwa wa homoni ya insulini katika seli mbalimbali mwili au vyote kwa pamoja. Hitilafu hii hupelekea mgonjwa kupata hali ya kukojoa mara kwa mara, kuhisi kiu sana na kupatwa na njaa kali sana.
Kuna aina mbalimbali za ugonjwa wa kisukari ambazo mtu anaweza kupata ila katika hizo zifuatazo ni muhimu sana kuzifahamu;
1. KISUKARI AINA YA KWANZA (I)
Aina hii huathiri takriban asilimia 10 ya wagonjwa wote wenye kisukari. Mgonjwa mwenye aina hii huwa na hitilafu katika uzalishaji wa homoni ya Insulini na hivyo kupewa jina la ' Kisukari kitegemeacho Insulini ' au 'Kisukari cha mapema' kwa kuwa huathiri watu wengi wangali katika umri mdogo (yani chini ya miaka 40). Chanzo cha ina hii kimekuwa kikihusishwa na mabadiliko katika vina saba, mwili kushambulia seli zake pamoja na mazingira
2. KISUKARI AINA YA PILI (II)
-Takribani asilimia 98 ya watu wenye Kisukari huathiriwa na aina hii. Kuwepo kwa ukinzani mkubwa zidi ya homoni ya Insulini katika seli za mwili hupelekea hitilafu katika mwili ambapo sukari katika damu hushindwa kuchukuliwa ipasavyo kwa matumizi.
-Watu wengi wanaoathiriwa na aina hii huwa ni kuanzia miaka 40 ila kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha hasa uzito uliopitiliza au unene pamoja na ulaji usio bora, watu hata chini ya miaka 40 siku hizi hupata aina hii.
-Aina hii ya kisukari imekuwa ikihusishwa na vihatarishi mbalimbali kama uzito uliopitiliza, unene, kutofanya mazoezi, utumiaji mkubwa wa vyakula vyenye sukari sana, umri na historia ya ugonjwa katika familia.
-Ugonjwa huu ni endelevu hivyo watu wengine hufanikiwa kuudhibiti kwa kuishi mtindo bora wa maisha bila ya kutumia dawa na huku wengine huishia kutumia dawa aidha za kumeza au sindano maisha yote.
3. KISUKARI CHA UJAUZITO
-Aina hii huathiri asiliamia chache ya wanawake kipindi cha ujauzito. Chanzo kikisemekana kuwa ni kutokana na homoni ya insulin kutojitosheleza kwa matumizi ya mama na mototo lakini pia ukinzani mkubwa zidi ya Insulini kutoka kwa homoni mbalimbali zinazozalishwa kipindi cha ujauzito.
-Wanawake wengi wajawazito hugundulika na ugonjwa huu kati ya wiki ya 24 hadi 28, hivyo uchunguzi wa Kisukari katika kipindi hiki ni wa muhimu sana
-Kisukari hiki huweza kuondoka au kuendelea kuwepo mara baada ya kujifungua (wiki 6 baada ya kujifungua)
-Tafiti zimeonyesha kuwa kuna uwezekano mtu mwenye kisukari cha ujauzito kilichoondoka kuweza kupata ugonjwa wa Kisukari kwa miaka ya mbeleni.
Ni muhimu kufanya uchunguzajiwa wa afya yako kwa kufika katika kituo cha afya. Ugonjwa huu umekuwa ukija kwa kasi katika kipindi hiki kutoka na mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia ambayo yamepelekea mfumo wa maisha kubadilika kuanzia ulaji, unywaji na shughuli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni