Shinikizo la damu la kawaida kwa mtu mzima inatakiwa isizidi milimita za Mekyuri 139/89 na isipungue milimita za Mekyuri 90/60. Namba ya juu ikisimama kama mgandamizo wakati moyo unatanuka kusukuma damu sehemu mbalimbali za mwili na namba ya chini ikisimama kama mgandamizo wakati moyo ukisinyaa kuingiza damu.
Shinikizo la damu hupimwa kwa kifaa maalumu kiitwacho sphygnomanomita ambacho kinaweza kuwa aina ya kile unachopimwa na mtu mwingine (manual) au kile unachoweza kujipima mwenyewe hata ukiwa nyumbani(automatic) .
Shinikizo la damu hudhibitika mpaka pale mtu atakapopimwa angalau mara vitatu (3) na kipimo kikawa kinasoma milimita za Mekyuri 140/90 au zaidi kila mara apimwapo.
Hizi ndio aina za shinikizo la juu la damu zinazowaathiri watu wengi katika jamii
1. Shinikizo la juu la damu-Primary
Takribani asilimia 95 ya wagonjwa wenye shinikizo la juu la damu hugundulika wakiwa na aina hii, huku chanzo cha shinikizo hili la damu kikiwa hakijafahamika kitaalamu.
Mbali na chanzo kutofahamika, tafiti zinaonesha uwepo wa mambo hatarishi kwa shinikizo hili la damu ikiwemo matumizi ya chumvi nyingi, umri, historia ya familia n.k
2. Shinikizo la juu la damu-Secondary
Aina hii ya shinikizo la damu huwakumba watu wachache katika jamii yani takribani asilimia 5-10 ya wagonjwa wenye shinikizo la juu la damu.
Mambo mbalimbali yameripotiwa na kuhusishwa kama vyanzo(visababishi) mbalimbali ya shinikizo hili la damu ikiwa ni pamoja na;
-Madawa mbalimali ya hospitalini na yale ya kujinunulia wenyewe madukani, mfano; dawa za uzazi wa mpango, steroidi, asprini n.k
-madawa ya kulevya kama kokeini
-magonjwa ya figo
-maradhi ya mishipa ya damu
-matatizo ya homoni mbalimbali katika mwili.
Shinikizo la juu la damu limekuwa ni tatizo linaloongezeka kwa kasi sana hasa miongo mwa watu wazima, na hii imepelekea madhara makubwa yatokanana na ugonjwa huu. Ni vizuri kupima kiwango cha shinikizo la damu kila mara uendapo kuonana na mtaalamu wa afya hospitalini na kufuata ushauri wa kitaalamu kuepukana na ugonjwa huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni