Dawa (sindano) ya Insulini imekuwa ikitumika katika hali mbalimbali kwa mgonjwa wa kisukari na hii yote ikiwa ni kufanikisha kiwango stahiki cha sukari mwilini, dawa hii hutumika kwa;
1. Mgonjwa wa kisukari aina ya kwanza (I)
-Wagonjwa wote wenye aina hii ya kisukari hutegemea sindano ya insulini katika kudhibiti sukari yako kwani kongosho yao haizalishi kabisa hompni ya Insulini. Hivyo wagonjwa hawa hutumia sindano hii siku zote katika maisha yao huku wakiendelea kufuata mtindo bola wa maisha.
2. Kushindwa kudhibiti sukari kwa kutumia dawa za kumeza
Kwa wagonjwa wenye kisukari aina ya pili, sindano ya Insulini hutumika endapo;
-Inapotokea dawa za kumeza zaidi ya moja katika dozi za kiwango cha juu kabisa zinashindwa kudhibiti kiwango cha sukari katika damu kwa muda wa miezi 2 had 3, inashauri kuanzisha sindano ya Insulini.
-Hii husaidia kumuepusha mgonjwa huyu katika kipindi kirefu cha sukari ya juu ambapo anaweza kuanza kupata madhara zaidi.
3. Hali ya mgonjwa isiyomruhusu dawa za kumeza
-Kutoka na tathmini kutoka kwa daktari mgonjwa anaweza asiruhusiwe kutumia dawa za kumeza na akatakiwa kutumia sindano ya Insulini.
-Inawezekana mgonjwa akawa na hali zisizomruhusu kutumia dawa za kumeza kama; uzio (allergy) ya dawa, madhara makali ya dawa, maradhi makubwa kama figo kushindwa kufanya kazi n.k
4. Kipindi cha upasuaji
-Inapotokea kuna upasuaji mkubwa au wa dhararu basi mgonjwa atapaswa kutumia sindano ya Insulini kipindi hiki ili kuweza kudhibiti sukari kwa hali ya juu kwani kipindi hiki mwili huwa kwenye hali ya "stress"
-"Stress" inapelekea sukari kuongezeka na hata kuleta shida kuidhibiti kwa njia ya dawa za kumeza.5. Kuibuka kwa madhara ya kisukari kwa mgonjwa
-Madhara ya kisukari hutokea haswa kwa sababu ya kutodhibiti sukari vizuri mwilini, madhara hayo ni pamoja na vidonda sugu katika miguu, figo kushindwa kufanya kazi n.k
-Inapotokea hali kama hizi zinazohitaji udhibiti imara wa sukari mwilini basi sindano ya Insulini itaanzishwa.6. Mgonjwa mwenye kiwango cha sukari cha juu mno
-Kuna wagonjwa wanakutwa na kiwango kikubwa cha sukari kuanzia milimol kwa lita 33.3 au mashine ya kupima sukari inasoma "high", hawa wanahitaji kuanzishwa sindano ya insulini ili kusaidia kwa urahisi kushusha sukari. Hali hii inaweza kuchangiwa na maambukizi ya vimelea mwilini au hata kutokutumia dawa za kisukari
-Viwango kama hivi vya sukari hupelekea wagonjwa wengine kupoteza hadi fahamu wakati kufikishwa hospitalini.
Matibabu ya ugonjwa wa kisukari yana lengo kuu ya kuidhibiti sukari katika kiwango cha kawaida katika damu na dawa (sindano) ya insulini ni moja ya tiba bora kwa ugonjwa. Tafiti nyingi zimeonesha ufanisi mkubwa wa dawa ya `insulini katika udhibiti wa sukari mwili. Hakuna haja ya kuoga kutumia dawa hii pale inapokuhitaji kutumia kwa manufaa ya afya yako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni