NI MUHIMU KUFAHAMU VIRUTUBISHO SITA (6) VINAVYOPATIKANA KWENYE VYAKULA MBALIMBALI.

Virutubisho ni viini-lishe ambavyo viko kwenye vyakula ambapo mwili huvitumia kufanya kazi mbalimbali. Viini-lishe hivi husaidiana kwa pamoja kujenga mwili wenye afya imara na ukosefu au upungufu wa virutubisho hivi nje ya kiasi kinachotakiwa hupelekea  maradhi mbalimbali mwilini. Virutubisho hivyo ni pamoja na;

1. Wanga

Hiki ni kiini-lishe kinachohitajika kwa kiasi kikubwa sana kwani asilimia 45-65 ya nguvu mwilini hutokana na kirutubisho hiki. Wanga ipo katika namna tofauti tofauti kulingana na aina ya chakula.

Wanga iliyopo kwenye viazi na mihogo (wanga tete) ni tofuati na wanga iliyopo kwenye matunda na mboga za maji. 

Kazi kuu ya wanga ni kuupatia mwili nguvu kufanya kazi mbalimbali. Mfano wa vyakula vyenye wanga ni pamoja na Ngano, Mtama, Uwele, Mahindi, Viazi , Mihogo n.k 

    
2. Protini
Kiini-lishe hiki ni sehemu muhimu sana ya mwili kwani huchangia asilimia 10-35 ya nguvu itokanayo ni virutubisho vyote.  
Protini huundwa na molekyuli ziitwazo amino asidi ambazo zipo zinazotengenezwa na mwili na ambazo haziwezi kutengenezwa na mwili (hutoka kwenye vyakula tunavyokula).
Protini hupatikana kwenye vyakula vya wanyama na mimea huku kazi yake kubwa ikiwa ni kujenga mwili.
Mfano : Mayai, samaki, nyama, maziwa, mboga jamii ya kunde n.k
3. Mafuta
Mafuta ni kiini-lishe nambari mbili cha nishati mwilini ikichangia asilimia 20-35 ya nishati yote mwilini.
Kuna aina mbili za mafuta ambazo ni mafuta kifu na mafuta yasiyokifu.
Aina ya mafuta tunayotumia kwenye milo yetu yana mchango mkubwa sana kwenye afya ya binadamu.
Mafuta kifu (hasa kutoka kwa wanyama) yamekuwa yakihusishwa kwa kuchangia maradhi mbalimbali kama ya moyo na mishipa ya damu.
Mfano; karanga, mbegu za mimea kama alizeti,nazi, michikichi pia nyama, samaki n.k
4. Makapi-mlo

Hii ni sehemu ya virutubisho vya wanga ambayo haimeng'enywi katika mfumo wa chakula. Makapi-mlo ni muhimu sana katika mwilini kwani yameonekana kuwa na faida nyingi kiafya pamoja na kuzuia magonjwa ya moyo, saratani, kisukari n.k

Mfano; Nafaka zisizokobolewa (mtama, uwele, mihogo, Mahindi n.k), matunda, mboga za majani n.k

5. Vitamini 

Kuna takribani aina kumi na moja (11) za vitamini ambapo kila aina ya vitamini ina umuhimu wake mwilini. Virutubisho hivi huhitajika kwa kiasi kidogo mwilini

Vitamini hizo ni pamoja na; Vitamin A, Vitamin B (B1,B2,B3,B6,B12, Folic asidi), Vitamin C, Vitamin D na Vitamin K

Mfano;  Mboga za majani, matunda, nyama, samaki n.k

6. Madini 

Hivi ni virutubisho ambavyo vinahitajika na mwili kwa kiwango kidogo ili kusaidia mwili kufanya kazi zake mbalimbali.

Madini haya yanahitajika kaktika kiwango sahihi ili kuepukana na maradhi yoyote yatokanayo na kuzidi au kupungua kwa madini mwilini.

Mfano wa madini hayo mwilini ni pamoja na sodiamu(Na), magnesium (Mg), potashiamu (K), Calcium (Ca), Chuma (Fe), chloride (Cl) n.k

Vyanzo vya madini haya ni pamoja na ; chumvi, nyama, maini, dagaa, samaki, mboga za majani, maziwa, matunda n.k

Mara zote ununuapo au unapoanda mlo wako ni muhimu kuzingatia uwepo wa vyakula vyenye virutubisho vyote vilivyotajwa hapo juu katika kiwango sahihi kulingana na jinsi (maumbile), umri, shughuli pamoja na afya yako kwa ujumla.  Hii husaidia kujenga afya bora ya mwili wako.

Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.