HUWEZI KUACHA KUFANYA MAZOEZI UKIZIFAHAMU FAIDA HIZI ZA KIAFYA ZA MAZOEZI

Ufanyaji wa mazoezi ni muhimu sana kwenye maisha ya kila siku kama inavyoshauriwa na wataalamu mbalimbali wa afya. Uzembe wa kutofanya mazoezi unaweza kuchangiwa na kutokuwa na ufahamu wa faida unazozipata kutoka kwenye mazoezi. Ukweli ni kuwa ukizifahamu faida hizi hutaweza kuacha kufanya mazoezi 

1. Huimarisha ubongo.

-Ufanyaji wa mazoezi inavyotakiwa husaidia kuimarisha seli za ubongo na hivyo kuboresha uwezo wa kufanya maamuzi, kufikiria, na kujifunza.

2. Hupunguza msongo wa mawazo na wasiwasi.

-Mabdiliko mbalimbali yanayotokea katika mfumo wa fahamu, mfumo wa homoni kipindi mtu anafanya mazoezi husaidia sana kukuondoka katika wasiwasi na msongo wa mawazo.

-Pamoja na hayo, mazoezi hsaidia kukutana na marafiki na pia huuchosha mwili, haya yote huchangia katika kukupatia faida hii.

3. Kuimarisha misuli na mifupa.

-Mazoezi ya aerobiki na ya kuimarisha misuli hupelekea kupunguza matatizo ya maumivu ya mgongo, nyonga, misuli na pia hupunguza mivunjiko ya mifupa hasa kwenye nyonga kwa watu wenye umri mkubwa.

4. Hukufanya uwe mwenye furaha

-Moja ya mambo mtu mwenye huzuni au sonona anashauri kufanya ni pamoja na mazoezi. Kemikali mbalimbali(kama endorphins) hutolewa kipindi cha mazoezi na husaidia kuleta hali ya furaha na hivyo kuendelea kufurahia mazoezi zaidi na zaidi.

5. Kuimarisha kumbukumbu

-Mazoezi ya mara kwa mara husaidia kuongeza uwezo wa kumbukumbu na kujifunza vitu vipya, hii inatokana na mabadiliko yanayoletwa na mazoezi katika sehemu husika za ubongo.

6. Huzuia maradhi ya moyo

-Mazoezi ya aerobiki yana faida kubwa kwa moyo kwani husaidia kuimarisha uwezo wa moyo kusukuma damu zaidi, hudhibiti kiwango cha mafuta katika mishipa ya damu, na pia kusaidia kudhibiti kiwango cha shinikizo la damu.

-Haya yote kwa ujumla huuweka moyo katika hali ya salama.

7. Huzuia unene au uzito uliopitiliza.

-Kwa kufanya mazoezi bila kusahau ulaji bora, uzito mkubwa au unene huweza kuzuilika na hata kudhibiti uzito wa kawaida kwa muda mrefu kwa matokeo bora ya kiafya.

-Kuna faida nyingi sana za kuwa na uzito wa kiwango cha kawaida na kuna hasara kama zote kuwa na unene au uzito uliopitiliza.

8. Kuzuia maradhi ya kisukari

-Kutofanya mazoezi ni moja ya mambo makubwa yanayochangia kutokea kwa ugonjwa wa kisukari aina ya pia na ndio maana huwezi kutenganisha mazoezi na ugonjwa wa kisukari kwani mazoezi ni shemu muhimu ya matibabu ya kisukari. 

-Mazoezi husaidia sana katika ufanisi wa kazi ya insulini mwilini kwa kupunguza ukinzani katika tishu mbalimbali.

9. Kuzuia magonjwa ya saratani

-Kumekuwa na uhusiano wa karibu sana wa maisha ya ubwenyenye kupelekea saratani mbalimbali.

-Na kwa kufanya mazeozi  imeonekana kuwa sehemu ya kuzuia kujitokeza kwa saratani hizo lakini pia ni sehemu ya muhimu ya matibabu ya saratani.

10. Kupata usingizi bora

-Kutoka na mazoezi, watu wengi wameweza kupata usingizi wenye ubora wa hali ya juu ukilinganisha wa watu ambao hawafanyi mazoezi kabisa. Usingizi bora ni sehemu muhimu ya mtindo bora wa maisha.

11. Kuwezesha mchakato wa uachaji wa kuvuta sigara

-Muunganiko wa tiba ya kisaikolojia pamoja na mazoezi mepesi au wastani imeonekana kusaidia sana katika programu nzima ya kuachana na uvutaji wa sigara.

-Lakini pia mazoezi magumu baada ya kuacha uvutaji wa sigara yameonekana kuwa na msaada wa kuzuia uzito mkubwa.

Fanya maamuzi, anza sasa kwani faida za mazoezi ni nyingi mno kuliko hasara.  Mazoezi ni tiba ya asili kwa magonjwa mengi hasa ya kisukari, saratani, moyo na ya mfumo wa hewa.  Angalau dk 30 za mazoezi katika siku 3 hadi 4 katika wiki zitakutosha kupata faida hizi za kifaya. 

Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Translate/tafsiri

Kunihusu

Picha yangu
KUWA MWENYE AFYA BORA NI JAMBO LA MSINGI SANA.BINAFSI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI NAJITAHIDI KULA MLO KAMILI,KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU ANGALAU KWA MUDA WA DAKIKA 30 NA PIA KUJENGA MUDA WA KUTOSHA KUUPUMZISHA MWILI BY DR FRANK

Lebo

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.